RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

RC Makala amesema wafanyabiashara ndogondogo jijini Dar es salaam wamekaa bila utaratibu maalumu na barabara zimezibwa na sasa wanalikaribia geti la Ikulu.

Makala amesema hali hii haikubaliki na ni lazima wafanyabiashara hao wapangwe upya katika utaratibu rasmi kwenye maeneo yote ya mkoa na waliopo barabarani na mbele ya maduka au ofisi za watu wengine wataondolewa.

Source: ITV habari!
Hii ingefanyika Tanzania nzima.Hawa wapangishe frame ya duka,ili kuingiza mapato ya serekali kwenye kodi ya zuio(with holding Tax)Frem nyingi kwenye miji,zimejengwa,hazina wapangaji,wakipatikana wapangaji na kodi ya zuio,imepatikana.Wengi wanaingiza faida kubwa,lakini hawalipi kodi.
 
Tulio ndani ndio tunajua haya... wengi huleta ushabiki eti ni wale ni MACHINGA.
 
Leo RC Makalla amekaa na madiwani kuwaelezea nia yake ya kuwapanga upya wamachinga ktk jiji hili la kibiashara (Source ITV habari).

Wamachinga walipewa Uhuru usiyokuwa na mipanga kiasi kwamba waligeuka kuwa kero kwa kila mtu.

Uamuzi wa RC Makalla uungwe mkono ili hawa wanyonge wafuate utaratibu. Na wawe na maeneo maalumu ya kufanyia kazi zao. Wasizagae hovyo.
Hii ingefanyika Tanzania nzima,Hawa wapangishe Frem,wenye Frem,watalipa kodi ya zuio(withholding Tax).

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
RC Makala amesema wafanyabiashara ndogondogo jijini Dar es salaam wamekaa bila utaratibu maalumu na barabara zimezibwa na sasa wanalikaribia geti la Ikulu.

Makala amesema hali hii haikubaliki na ni lazima wafanyabiashara hao wapangwe upya katika utaratibu rasmi kwenye maeneo yote ya mkoa na waliopo barabarani na mbele ya maduka au ofisi za watu wengine wataondolewa.

Chanzo: ITV habari!
Naunga mkono hoja, Asante sana Makalla kwa kuliona hili nililisema hili.

Kwa hili la Kuwaondoa wamachinga mjini naungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar. Kwa hali iliyopo Dar ya sasa imekuwa vurugu bidhaa zimepangwa hadi barabani. Serikali inakosa mapato mengi sana kuendelea kuweka vibanda kila sehemu. Sehemu nyingine zilikuwa zinatumika kwa ajili ya parking ya magari sasa kuna vubanda. Inashangaza zaidi hadi maeneo yote ya posta yamezagaa vibanda vya wamachinga. this not right kwa kweli..
 
Chadema wanashangilia machinga wakikosa pa kufanyia baishara zao ili wapate wateja kwenye mikutano Yao ya siasa.
Siasa ndiyo imechangia kuliharibu jiji..wanasiasa wenye mawazo muflisi kama haya ndio wamesababisha jiji limekuwa la vibanda kile sehemu. Huwezi kutofautisha manzese na posta. Na hii imezagaa maeneo yote,...Mwanza kule ndio kabisa hata gari haliwezi kupita.
 
RC Makala amesema wafanyabiashara ndogondogo jijini Dar es salaam wamekaa bila utaratibu maalumu na barabara zimezibwa na sasa wanalikaribia geti la Ikulu.

Makala amesema hali hii haikubaliki na ni lazima wafanyabiashara hao wapangwe upya katika utaratibu rasmi kwenye maeneo yote ya mkoa na waliopo barabarani na mbele ya maduka au ofisi za watu wengine wataondolewa.

Chanzo: ITV habari!
Zoezi gumu hili. Ajira hakuna, kila kijana kaamua kuwa mmachinga. Hayo maeneo ya kuwapeleka yako wapi?
 
Tungeomba hata Mwanza pia waangalie upya maana dah! Ni zaid ya kero
 
Back
Top Bottom