RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

RC Makala: Wafanyabiashara ndogo ndogo kupangwa upya Dar es Salaam, walioko barabarani kuondolewa

Leo RC Makalla amekaa na madiwani kuwaelezea nia yake ya kuwapanga upya wamachinga ktk jiji hili la kibiashara

Chanzo: ITV habari

Wamachinga walipewa Uhuru usiyokuwa na mipanga kiasi kwamba waligeuka kuwa kero kwa kila mtu.

Uamuzi wa RC Makalla uungwe mkono ili hawa wanyonge wafuate utaratibu. Na wawe na maeneo maalumu ya kufanyia kazi zao. Wasizagae hovyo.
Mh Makala, tunaomba pia mfukuze Bashite hapo dsm aende koromije, hana kazi na haijulikani anachokitafuta dsm hadi sasa.tafadhali aongozane na ombaomba watakaoshushwa pale Dodoma.
 
Mbna mlikuwa mkitetea kila alichokuwa akifanya mwendazake?????naww ukaamua kuweka na picha yake kabsa
Naunga hoja,na hili lisiishie Dar pekee,lisambae majiji yote,mwaka huu kidogo nigongwe na coster nikiwa Mwanza maeneo ya Natta kisa vibanda vya machinga maaana sikuweza kuona gari lililokuwa upande wangu kwenye Kona

Mungu alikuwa upande wangu ,nashukuru Niko mzima lakini Hawa watu ni hatari Sana kwa afya za biniadamu wenzao
 
Wengine wanapikia majiko ya gas Kando ya barabara, pembeni kuna majiko ya mkaa au moto wa kuni karibu na mtungi wa gas
 
Mji mzima umejaa vibanda
Mji unaonekana kama vijiji vya Vietnam
Zamani

Ova
 
Kuna machinga wamejenga mabanda yaani utadhani maduka ya nguo baadhi ya maeneo, leo hapo ubungo darajani upande wa msikiti nimekuta ugomvi jioni hii mtembea kwa miguu amekanyaga Nyanya daah nimeacha timbwili hapo.....wamepanga service road yote.
Sehemu za kupita kwa miguu unakutana na foleni sababu ni machinga
 
Tatizo hapa sio kupangwa tungeni sheria upya waambieni baada ya miaka mitatu mtahamia kule tulikowatengea maeneo,nyie tambueni neno machinga limeficha Familia.sio kutamka machinga tu
 
Leo RC Makalla amekaa na madiwani kuwaelezea nia yake ya kuwapanga upya wamachinga ktk jiji hili la kibiashara

Chanzo: ITV habari

Wamachinga walipewa Uhuru usiyokuwa na mipaka kiasi kwamba waligeuka kuwa kero kwa kila mtu.

Uamuzi wa RC Makalla uungwe mkono ili hawa wanyonge wafuate utaratibu. Na wawe na maeneo maalumu ya kufanyia kazi zao. Wasizagae hovyo.
Hili naliunga mkono, na TANROADS nao wawekeze katika kusafisha barabara kwa kutumia sweepers yale magari sio manual na pia mifereji kwa kushirikiana na wenyeji au wafanyabiashara
 
Wakati mwigine nawaza kuwahoji id za nida HAWANA uwoga kabisa kama mtanzania
 
Chadema wanashangilia machinga wakikosa pa kufanyia baishara zao ili wapate wateja kwenye mikutano Yao ya siasa.
Stroke man sijui unafeli wapi kila muda kuiwaza chadema tu, hali iliyokuwa kariakoo unaona sawa vile?
 
Hili la wamachinga ni time bomb
Rais Samia asiliendee kichwakichwa, litamuondolea kuaminika na kuungwa mkono na maelfu ya wamachinga akiliendea kwa pupa

Hakuna short term solution kwenye ishu ya wamachinga, linahitaji bajeti, ujenzi wa miundo mbinu ya kuwaaccomodate n. k

Isitoshe, Wamachinga walihakikishiwa na serikali kutosumbuliwa, Sasa Samia atimize ilani na ahadi waliyoitoa kwa wamachina mwaka 2020, la sivyo hii ni hadaa.

Serikali ya Magufuli ambayo Samia alikuwa makamu wake iliwahakikishia Wamachinga kutowasumbua, na hadi 20000 za vitambulisho ikawatoza, Sasa iweje awageuke? —Hii itamsumbua sana Samia, It is a political gamble akifanya hili KWA SASA BILA MIUNDO MBINU YA KUWAACCOMODATE WAMACHINGA

Tuchague moja, kile tunachokiita țţţuchafu wa Machinga, au jeshi la vijana lililokata tamaa kwa kushindwa kujiajiri.
Mkuu kwa namna yeyote ile ya kuwashugulikia wamachinga wote waliotapakaa Dar ni ngumu. Itakuwa ni vigumu kuwapatia wote sehemu ya kufanyia biashara. Nadhani kuwe na plans 2. Plan ya kwanza, kwa wale wenye uwezo wa kulipa kodi la pango - wapewe/wajengewe sehemu za biashara kama ile ya machinga complex. Wale ambao hawana uweze wa kulipa kodi watafutiwe eneo nje ya Dar wawekewe miundombinu ya kilimo au shughuli nyingine yeyote ya ujasiliamali kama wale waliopelekwa Gezaulole, wakaazishe vijiji huko. Ilikuwa vigumu kuanza lakini leo Gezaulole ni mji mdogo unaopendeza.
 
Back
Top Bottom