RC Makalla: Kuanzia usiku wa leo hakuna Panya Road atasalimika, operesheni inayoanza si salama kwao

RC Makalla: Kuanzia usiku wa leo hakuna Panya Road atasalimika, operesheni inayoanza si salama kwao

alafu yule bibi alikuwa anawabembemleza
Anayekuambia uchukue mkopo si atakayekuja kukudai ukishindwa marejesho.

Hii nchi ina raisi mwenye sauti ya kubembeleza ila inalindwa na watu katili sana.
 
Panya road nini? Siamini kabisa kwamba kuna watu wanaitwa Panya road ila kuna wezi wanaotumia mapanga kuvamia watu kuwaibia na kuwajeruhi wanotaka kuwazuia wasichukue wanachotaka.
Kwa vyovyote iwavyo polis baadhi wanahusika katika matukio aya haiwezekani wezi wateke mtaa mzima afu polis washindwe kuwanasa. Kibaya zaidi wanaiba mchana mimi sikubaliani na ayo majina yenu mnayobatiza wezi kwakuwaita Panya road.
Mkuu hao panya ni tatizo!
Polisi wakiwa kwenye defender lao wakakutana na hao panya wanageza au wanapita kwa kasi wanaondoka!

Polisi kuwakamata panya labda wakiwa mmoja moja huko mtaani na sio kwenye tukio.

Shida inakuja baada ya kuwakamata mtaani utathibitishaje kama kweli ni muhalifu?

Ndo hapo ktk op kama hii iliotangazwa wataumia wengi tu ambao hawahusiki, kuna namna nyingi tu za kuzibiti uhalifu sio lazima iwe nguvu kwa nguvu.

Unaweza kuzuia uhalifu kwa kutumia nguvu lakini mentality ya uhalifu unaiondoaje kwa nguvu?
Nategemea operation itafanikiwa kwa muda tu na baadae maisha yataendelea vile vile!
Kwasababu hakuna kilichobadilishwa.

Ni kwa nn kundi la watu zaidi ya 100 wanakubaliana kuvamia kujeruhi na kuiba? Lazima kuna tatizo linarukwa na kujikita kwenye matokeo. Ni kama inshu ya singo maza tu!
 
Hebu jaribu ku-google uandike 'self defence body spray' au Pepper spray self protection'. Utaona zinakouzwa kwa hapo Dar. Mie nime-google naona kuna hadi watu wanaziuza zoom Tanzania (Kinondoni. Tsh 40K). Sema siwezi weka link JF wazije wakanipiga ban. Hawaruhusu kuweka link humu.

Hizi spray pia zinatumika haswa kwa wadada wanaoenda kutoa huduma nyumbani kwa mtu kwa kazi kama usafi ama kazi za ndani kwa siku. Akifika kwa boss ake kisha boss akataka kumfanyia unyanyasaji wa kijinsia, mdada anatoa kwenye kimkoba chake na kum-spray huyo janaume. Hatarudia tena kunyanyasa wanawake.

Nimekupa mbinu zaidi mkuu. Elimisha na wengine huko uliko. Ulinzi binafsi ni jukumu lako kwanza kabla Polisi hawajafika.
Hizo link za zoom ni za mda kidogo,nlifikiri ungenitajia duka maalum wanalouza recently
 
Hapo panya road wajiandae tu,
Ni mwendo wa kunyang'anywa mapanga kisha wanapelekwa kwenda kuonyesha sehemu wanapoficha mapanga yao.
Wakifika huko panya wengine wanakuja kuwaokoa panya wenzao kisha yanatokea majibishano ya mapanga kati ya panya road na askari wetu, ila kutokana na weledi wa askari wetu wanafanikiwa kupambana kimedani mpaka panya wanachanyikiwa na kwa bahati mbaya wanaanza kukatana mapanga wenyewe kwa wenyewe na kujeruhiana vibaya sana.
Askari wetu wakiwa wanawawahisha hospital bahati mbaya panya wanapoteza maisha wakiwa njiani kutokana na kupoteza damu nyingi kwenye majeraha waliyopata.

Mimi binafsi naunga mkono panya wote wanyang'anywe mapanga yao haraka iwezekanavyo kabla hawajaleta athari kubwa zaidi katika jamii.
 
Hapo panya road wajiandae tu,
Ni mwendo wa kunyang'anywa mapanga kisha wanapelekwa kwenda kuonyesha sehemu wanapoficha mapanga yao.
Wakifika huko panya wengine wanakuja kuwaokoa panya wenzao kisha yanatokea majibishano ya mapanga kati ya panya road na askari wetu, ila kutokana na weledi wa askari wetu wanafanikiwa kupambana kimedani mpaka panya wanachanyikiwa na kwa bahati mbaya wanaanza kukatana mapanga wenyewe kwa wenyewe na kujeruhiana vibaya sana.
Askari wetu wakiwa wanawawahisha hospital bahati mbaya panya wanapoteza maisha wakiwa njiani kutokana na kupoteza damu nyingi kwenye majeraha waliyopata.

Mimi binafsi naunga mkono panya wote wanyang'anywe mapanga yao haraka iwezekanavyo kabla hawajaleta athari kubwa zaidi katika jamii.
Hao panya ni watoto tu wasio na adabu na malezi mabovu.
Hawana ubavu wa kwenda kujibishanan na polisi wenye AK 47 na mabati yaliyochongwa.
 
Kwenye kuokoa kuna wanaopona na kufa, so issue ya watakaorudi ni nafuu warudi na vilema vya kudumu, mfano mtu anarudi akiwa hana pua, masikio na vidole vya miguuni, nyonga imelegezwa kama mlenda!.
Kuna wale wanarudi huoni majeraha ua milele na maumivu yasionekana, hiyo inakuwa mpaka kiakili wanakuwa hawako sawa. Inapaswa kuwa special case.
 
Afadhali wamefanya yao kabla ya sikukuu...

wadhibitiwe mapema...

Mazalia ya omba omba hayo..watoto hawana kwao!
Wana kwao na wengne wanahudumia familia kwa kaz hii haramu. Wazazi wengne wanajua kaz wanazofanya watoto wao na wamebarik
 
Haha, kuna watu wapuuzi sana. Watadai haki za kibinadamu zinavunjwa. Za wengine wanaofata sheria, wanaoibiwa,kupigwa, kuuawawa, kutoweza kutembea kwa uhuru hazivunji.

Tunajali haki za wahalifu tu.
Anandugu yake mwalifu au nae ni mwizi huyoooo. Wachache wafe kwa maslah ya weng
 
Mawazo ya kipuuzi kbs na mawazo km haya ndy wanakuwa Nayo polisi baadhi wakishapewa kazi ya kuingia mtaani kutafuta wahalifu..

Enzi hizo za wahuni wa Temeke Mimi nimewahi kusombwa polisi kisa tupo kitaani tunacheza draft na polisi wanatafuta vikundi vya kihalifu

Wangekuwa na mawazo km yako wengi tungekufa bila hatia

Km umezaliwa uswahilini wanakotokea hawa panya road,mburahati,kigogo,manzese,tandika nk haiwezi kuepuka kukutwa na majanga ya kihalifu ktk safari ya maisha yako..

Hao watoto wamejikuta Tu wamezaliwa uswahilini,hawakujichagulia wao wenyewe ingawa uhalifu ni Jambo walilolichagua..Polisi wakiingia mtaani wanachojua wanaenda kukamata panya road uswahilini,sasa mara kadhaa inatokea wanakamatwa na wasiohusika..Je,kuua ni solution?? Fikiria tena mkuu!!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Acha wauwawe hata dini ,inasema anaye uwa na yeye auwawe ,kumbuka operation iliofanyika Boston miaka kadhaa iliopita ,kuna wakat maamuzi yakikatili ndio uleta tija kwa umma!!
Aiwezekan panya road wanasumbua kisha jamii inayo ishi nao eti haiwafaham sikweli kabsa.
Mtaan watu wanajuana kibaka nan mvuta Bhangi yup na mpenda madem nani!?
Kwa wanaojielewa Kwenye operation hizi aziwakut sehem atarish maana taarifa unayo!!
Na ukikutwa lazima uwajibike
 
Kitendo Cha kuongezeka kwa matukio ya uhalifu ni dhahiri kwamba maisha ni magumu Sana na tutashudia mengi Sana haya ya Panya Barabara ni mwanzo tu
Maisha kuwa magum awakupatii kibali cha kudhuru watu na kuwaibia ,tumetokea huko huko ,kushindia andaz Moja had jion ,tena unavuta mda chai unakunywa saa Sita au saba kasoro ili izibe gap ya lunch, na atujawai dhuru mtu , hawa ni majambazi ,na wameyachagua Maisha hayo na lazima waangamizwe kwa gharama yoyote
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema "Kuanzia leo, baada ya tamko langu leo, usiku wa leo na kuendelea hakuna 'Panya Road' atasalimika katika mkoa wa Dar, oparesheni inayoanza usiku wa leo si salama kwa 'Panya Road', oparesheni inayoanza leo inaenda kuua uti wa mgongo wa mtandao mzima wa 'Panya Road"

Ameongeza "Niwasihi wazazi kwamba operesheni hii haitowaacha watoto wao wahalifu, kama mzazi ulizoea kupata zawadi kwa mtoto, TV bila kujua kipato chake, akudanganye 'amebeti', kawatafuteni watoto wenu kwenye vituo vya Polisi kuanzia kesho"

Amesisitiza "Kila Wilaya kwa mikoa ya Kipolisi, kutoa taarifa za kila siku za Operesheni ondoa 'Panya Road' na kudhibiti uhalifu katika mkoa wa Dar es Salaam kila siku, toeni taarifa tusipotoa taarifa watazitoa taarifa mbaya"

Ameyasema hayo siku moja baada ya kundi hilo la uvamizi kuvamia na kujeruhi watu 19 katika Maenel ya Mtongani, Kunduchi mkoani humo
Wasiojulikana waingilie Kati basi mchezo uishe
 
Hao panya ni watoto tu wasio na adabu na malezi mabovu.
Hawana ubavu wa kwenda kujibishanan na polisi wenye AK 47 na mabati yaliyochongwa.
AK 47 unaifahamu? Yani waende kukamata watoto na AK 47! Wacha masihara hiyo ndude inatumika Ukraine na si kwa panya.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Suluhisho siyo kuwamaliza ila kuwawekea mazingira rafiki ya kujipatia riziki halali. Nguvu ya Dola kamwe haiwewiki watu huru
Unaambiwa ni vijana wa 14- 18 years. Wanavuta bangi, kunywa pombe na kutumia madawa mengine ya kulevya. Umri huu ni kuwa wamekosa ajira ama wameasi masomo na kuingia mtaani kufanya uhalifu?
 
Back
Top Bottom