RC Makalla: Machinga wakirudi maeneo waliyohamishwa, nitakuwa sitoshi kwenye nafasi yangu

RC Makalla: Machinga wakirudi maeneo waliyohamishwa, nitakuwa sitoshi kwenye nafasi yangu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewataka watendaji wa mitaa kulinda maeneo yao, kuhakikisha wamachinga waliohamishwa hawarudi tena maeneo hayo, wakikuta kibanda watajua watendaji wanahusika.

Amesema wamachinga wakirudi katika maeneo waliyohamisha itamaanisha yeye hatoshi kwenye nafasi yake. Na amewataka Taasisi, shule na mashirika yalinde maeneo yao wamachinga wasivamie.

Kisheria, mtu akifanya biashara kwenye hifadhi ya barabara ni faini Tsh. 300,000 au kifungo kisichozidi mwaka mmoja. Mkuu wa Mkoa amebainisha.

 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewataka watendaji wa mitaa kulinda maeneo yao, kuhakikisha wamachinga waliohamishwa hawarudi tena maeneo hayo, wakikuta kibanda watajua watendaji wanahusika
Amerahisisha maisha huyu, Kama huna hela unanunua maembe unaweka barabarani unakamatwa unaenda kula Dona la bure mwaka mzima.
 
Machinga ni watoto wetu pia,
Waangaliwe kwa jicho la huruma.
Wawezeshwe,wapewe Maeneo permanent ya kufanya biashara zao.
Pale wanapokosea waelimishwe
 
Alowaruhusu ni ccm anaowachinjiia baharini ni CCM Ila naipenda ccm inavyojua kuuma na kupuliza.

Kura za wamachinga zitatafutiwa mbinu jinsi ya kuzipata ni jambo la kusubiri tu tuone uchaguzi utapowadia kama kweli hili zuio litakuwa ni la muda au la kudumu itafahamika tu mo na daimond Nani simba.
 
Aweke akiba ya maneno, uchaguzi ukikaribia atayakana maneno yake.
Sema machinga huwa awaijui ccm inang'ata na kupuliza
 
Hivi, mliopo huko jijini,sasa kuna mabadiliko ama? Maana sisi wa vijijini tunasoma tu. Ni kweli jiji limekaa sawa kama jamaa hawa wanavyodai?
 
Kwa hiyo machinga washakuwa majangili sasa,ni vijana tu wenye nguvu zao ambao wameamua kujitafutia riziki iliyo halali sema sio maeneo rasmi...wakigeuza mindset zao na kuwa majambazi sijui kama utakuja kutoa kauli kama hiyo ya kuvimbilwa.
 
Watarudi tu..hata kama ni baada ya mwaka, au karibia na uchaguzi. Halaf tuone atafanyaje
 
Back
Top Bottom