RC Makalla: Machinga wakirudi maeneo waliyohamishwa, nitakuwa sitoshi kwenye nafasi yangu

RC Makalla: Machinga wakirudi maeneo waliyohamishwa, nitakuwa sitoshi kwenye nafasi yangu

Kwa hiyo machinga washakuwa majangili sasa,ni vijana tu wenye nguvu zao ambao wameamua kujitafutia riziki iliyo halali sema sio maeneo rasmi...wakigeuza mindset zao na kuwa majambazi sijui kama utakuja kutoa kauli kama hiyo ya kuvimbilwa.

Ajira zilivyosimamishwa umewahi kisikia wasomi watageuka majambazi. Waliojitolea JKT na hadi leo hawana kazi umewahi kusikia watakuwa majambazi? Acheni kuwadharau wamachinga na kuwaona vibaka.
 
Hili ni pigo aisee
Wanategemea kutoka ndo wale mkuu.na pia mzunguko katika biashara za jumla utashuka.yani akuna biashara ambayo haitoguswa na hl swala.mana wanapopelekwa ndipo walipotoka na kuja barabrani.wangepewa elim dheni na kipindi kirefu wajiandae pale pole
 
Mbona kama naona maeneo ya Kariakoo mbali na kuvunjiwa vibanda bado wanaendelea kufanya biashara zao?
 
Wanategemea kutoka ndo wale mkuu.na pia mzunguko katika biashara za jumla utashuka.yani akuna biashara ambayo haitoguswa na hl swala.mana wanapopelekwa ndipo walipotoka na kuja barabrani.wangepewa elim dheni na kipindi kirefu wajiandae pale pole
Wale wa maduka kariakooo wanachekelea wakati wanunuzi wao ndio hao wamefukuzwa, sababu walikuwa wanatoa bidhaa madukani wanauza barabarani
 
Tatizo hao watendaji wenyewe ni wamachinga

Makalla ajue kuwa madiwani na wenyeviti wa mitaa wanahusika na biashara za machinga. Akitaka kuendelea na ukuu wa Mkoa wa Dar. lazima ahakikishe kuwa madiwani na wenyeviti wa mitaa ambayo kutakuwa na wafanya biashara kwenye sehemu zisizo rasmi vikiwemo viwanja vya makazi anawawajibisha kabla ya yeye mwenyewe kuwajibishwa!!!

Kulinda kitumbua chake asikae ofisini tu bali afanye inspection wilaya zote akianzia na wilaya ya Kinondoni. Akikaa ofisini tu akingojea ripoti itakula kwake kwani hao wasaidizi wake watamuingiza chaka!!!
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewataka watendaji wa mitaa kulinda maeneo yao, kuhakikisha wamachinga waliohamishwa hawarudi tena maeneo hayo, wakikuta kibanda watajua watendaji wanahusika.

Amesema wamachinga wakirudi katika maeneo waliyohamisha itamaanisha yeye hatoshi kwenye nafasi yake. Na amewataka Taasisi, shule na mashirika yalinde maeneo yao wamachinga wasivamie.

Kisheria, mtu akifanya biashara kwenye hifadhi ya barabara ni faini Tsh. 300,000 au kifungo kisichozidi mwaka mmoja. Mkuu wa Mkoa amebainisha.

Tawire mh.Mkuu wa mkoa.....💪
 
Kwa hiyo machinga washakuwa majangili sasa,ni vijana tu wenye nguvu zao ambao wameamua kujitafutia riziki iliyo halali sema sio maeneo rasmi...wakigeuza mindset zao na kuwa majambazi sijui kama utakuja kutoa kauli kama hiyo ya kuvimbilwa.
Kwa hiyo majambazi wanaweza kuizidi Serikali?!!! Kweli kabisaaa?!!
 
Back
Top Bottom