RC Makonda aandaa sherehe Arusha. Anatarajiwa kuchinja ng'ombe 200

RC Makonda aandaa sherehe Arusha. Anatarajiwa kuchinja ng'ombe 200

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ng’ombe takribani 200 watatolewa kwa ajili ya kuchoma nyama, tukio linalolenga kuimarisha uhusiano kati ya wafanyabiashara wa mkoa huo na viongozi wanaoshiriki kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma.

“Ng’ombe kama 200 hivi watachinjwa, ni kuchoma nyama tu hakuna ugali wala wali, lakini tumewaita wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Arusha” amesema Makonda

Ametangaza kufanyika kwa sherehe ndogo Agosti 29, 2024 kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wa Arusha na Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma.
Hivi kipaumbele cha mkoa wa Arusha ni nini? Wafanya biashara malalamiko yao yameshasikilizwa na kufanyiwa kazi? taasisi zinazo lalamikiwa tayari zimesha wajibishwa na viongozi ku ngatuliwa?
 
Nimepiga hesabu ya haraka haraka ng'ombe 200@850,000 =170,000,000

Yaani 170M

Labda kama hizo gharama wamechangia hao wafanya biashara, ila yeye na Ofisi yake ya Mkoa hawana hicho kiasi.
Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.....

Arusha ina matajiri wengi....

Sadaka na zaka si tu huko misikitini na makanisani....

Kulitunza dola letu kunahitaji SADAKA NA ZAKA za MALI na UHAI WETU...

Mh.Makonda analifahamu hilo fika[emoji7][emoji7]

#Nchi Kwanza[emoji7]
 
Bado huko ni kuwaza kwa kutawaliwa na fikra za kimasikini tu,

I think as we are under the capable leadership of Dr.Samia Suluhu Hassan as commander in chief of defense forces of Tanzania,

hiyo mindset ya kinyonge itakwisha kabisa na tusonge mbele tukifurahia uchumi Imara pamoja, right gentleman?[emoji205]
[emoji7][emoji1787]
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amesema ng’ombe takribani 200 watatolewa kwa ajili ya kuchoma nyama, tukio linalolenga kuimarisha uhusiano kati ya wafanyabiashara wa mkoa huo na viongozi wanaoshiriki kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma.

“Ng’ombe kama 200 hivi watachinjwa, ni kuchoma nyama tu hakuna ugali wala wali, lakini tumewaita wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Arusha” amesema Makonda

Ametangaza kufanyika kwa sherehe ndogo Agosti 29, 2024 kwa lengo la kuwakutanisha wafanyabiashara wa Arusha na Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma.
aangalie wadudu wasije wangamuunganisha kwenye ng`ombe 200 akawa wa201
 
wacha nikupe siri kidogo mzee mwenzangu ARUSHA sio ile ulikua unaijua chukua hiyo

jiji limefunguka haswaa chini ya uongozi wa RC
Nafahamu Mzee mwenzangu, ila ninachopinga ni kusema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ndiyo imegharamia hizo gharama zote.

RC mwenyewe ameteuliwa kwenye hiyo nafasi hana hata mwaka mmoja.

Nina uhakika pasi na shaka, kutokana na ushawishi wa RC, hizo gharama zimefadhiriwa na Hao Wafanyabiashara katika kudumisha mahusiano mema.

Hao watu Serikali inawaita Wadau wa maendeleo.

Lakini kusema Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwa na Bajeti ya kuhost hiyo shughuli naona ni uwongo.
 
kuna kipi cha kusherehekea?
au sababu anazo mwenyewe sirini?
kukutanisha hao watu ni mpaka kuchinja ng'ombe?
Ndio....

Sadaka na zaka si tu huko nyumba za ibada....

Dola letu la JMT linahitaji sadaka na zaka ya mali na uhai....

Mbele ya Chifu wetu ni lazima tuteketeze sadaka kwa ajili ya baraka ya ardhi....

Yaani awepo chifu mkuu chifu Hangaya halafu tuteketeze sadaka ya "ubwabwa ndondo"?!! [emoji44][emoji44]

Aaaah wapiii
 
Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.....

Arusha ina matajiri wengi....

Sadaka na zaka si tu huko misikitini na makanisani....

Kulitunza dola letu kunahitaji SADAKA NA ZAKA za MALI na UHAI WETU...

Mh.Makonda analifahamu hilo fika[emoji7][emoji7]

#Nchi Kwanza[emoji7]
Hapa nakubaliana na wewe asilimia 100.

Kwamba hizo gharama zimefadhiriwa na Hao hao Wafanyabiashara.

Jambo la kuzingatia ni suala la Ushawishi pamoja na mahusiano

Maana mikoa ipo mingi lakini sio Wakuu wote wa Mikoa wanafanya alichofanya Paul Makonda.
 
Back
Top Bottom