RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

..naunga mkono agizo la RC Makonda.

..hili la barakoa liko ndani ya uwezo wetu.

..tena tulitakiwa tuchukue hatua hizi mapema.
 
Makonda anataka tukae vikao vya familia kujadili Corona. Naona kachanganyikiwa sasa! Superstitious wanakwamaga sana
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Paul Makonda amesema kuanzia Aprili 20 siku ya Jumatatu kila mtu atakayepanda Daladala na anayekwenda kwenye eneo la manunuzi yeyote lazima awe amevaa Barako (Mask)

Poa siku hiyo ya Jumatatu ameelekeza biashara zote zifanyike katika mfumo wa 'Take Away', hivyo mtu akienda sehemu anunue na aondoke.
 
Nimepata habari hii toka ukurasa wa instagram wa Millard Ayo. Picha ina maelezo kamili.
E3D41E79-FE1A-43D1-B9C5-2E786DC23F7F.png

=================================
Tulishatoa ushauri juu ya hili pia Naomba ifanywe kwa dharura: Napendekeza kuanzia Jumamosi iwe ni marufuku mtu kutoka nje ya nyumba yake bila kufunika uso kwa kitambaa/ barakoa/ scarf - JamiiForums

===================================
Mkuu wa mkoa wa Dar, Paul Makonda ameagiza kuwa mtu yeyote anayeenda katika eneo lolote la manunuzi lazima awe amevaa barakoa (mask).

Amesema haijalishi ila lazima watu wavae barakoa “Ununue, ukate kanga, ukate leso na utafute rubber bands. Lazima uwe umevaa barakoa”

Aidha, ameagiza kuwa kuanzia Jumatatu biashara zote zifanyike kwa mfumo wa ‘take away’ yaani ufike sehemu ya kununua bidhaa, nunua na ondoka.

Lakini pia amewataka watu kuhakikisha wanakaa umbali wa mita mbili kila wakiwa eneo la wa watu huku akiwataka wenye masoko kutafuta mfumo mbadala na mzuri wa kusimama masoko.
 
Back
Top Bottom