RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bwana Paul Makonda amesema kuanzia Aprili 20 siku ya Jumatatu kila mtu atakayepanda Daladala na anayekwenda kwenye eneo la manunuzi yeyote lazima awe amevaa Barako (Mask)

Poa siku hiyo ya Jumatatu ameelekeza biashara zote zifanyike katika mfumo wa 'Take Away', hivyo mtu akienda sehemu anunue na aondoke.

Hivi Serikali kutangaza ' Curfew ' kwa Mkoa wa Dar es Salaam ili kukabiliana na Janga hili baya la CORONA inaogopa nini hasa?
 
Maelekezo yote yanayolenga kupunguza maambukizi yaungwe mkono.

Makonda kwenye hili anastahili kuungwa mkono lakini anatakiwa kwenda mbele zaidi.

Ushauri wangu ni kuwa mikusanyiko ya ibada idhibitiwe. Kila msikiti au kanisa, siku za ibada, idadi ya washiriki isizidi watu 20 - 30 kwa kutegemea ukubwa wa jengo. Kuwe na umbali usiopungua mita 10 kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Watu wengine wafuatilie ibada kwa kupitia televison majumbani mwao, wakiona inafaa. Na wale wanaoona wanaweza kuandaa utaratibu wao wa ibada majumbani wafanye hivyo.

TBC watoa ratiba za ibada kwa kila dhehebu na dini.
 
tumeambiwa tuheshimu maagizo ya viongozi wetu yawe yanatekelezeka ama laa

adui ni korona
 
Kila mtu mdomo ukimuwasha anaongea chake. Bora rais aje atoe muongozo kama ni lockdown au curfew.
Kuliko huu utoto unao fanywa, mara take away mara kuvaa masendeu!

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo Raisi Magufuli aliteuwa watu wa kuzungumzia Corona.

Lakini baada ya muda wakaja Makonda na vibonzo vyao, mara wakakalipiwa na Waziri Mkuu wakikumbushwa kuwa wasemaji wataendelea kuwa wale wale na si vinginevyo.

Sasa wameanza tena mara funga baa,mara fungua baa, mara vaa mask ukipanda daladala.
Shida ipo wapi? Kila mmoja amegeuka kambale,tunaenda wapl?

Magu ni wakati wa kudhibiti utovu wa nidhamu wa wasaidizi wako. Likizo inatosha.
 
Hili li bashite si walifungie ndani tu kipindi hiki ambacho nchi inapitia vitu serious.. then watamfungulia baadae nchi ikitulia.
 
Jamaa ni zero kweli kwamba nikienda kununua vocha iwe take away, pipi ziwe take away, gest nibebe kitanda nikalale, mafuta sheli niende na dumu! labda kama umenukuu vibaya ila kama kasema haya basi ni zero bashite.
Mimi nadhani tuzingatie ujumbe uliokusudiwa. Anachomaanisha ni kuwa chochote utakachoenda kununua, ununue na kuondoka. Usinunue kuku choma na kukaa baa. Ukiweza nunua kuku wako, nenda ukale ukiwa nyumbani.

Lakini nadhani ofisi zote za umma na makampuni, wafanyakazi wakae majumbani. Kama haiwezekani kufunga kabisa, wabakizwe wafanyakzi 25%. Wengine wakae majumbani.

Masoko yazuie biashara nyingine zote isipokuwa vyakula.

Maduka yafungwe, tabakie na maduka ya dawa, groceries na supermarkets. Na kwenye maduka hayo uandaliwe utaratibu wa namna ya kufanya manunuzi bila msongamano. Kukifanyika haya, hata msongamano kwenye vyombo vya usafiri utaondoka.
 
Kila mtu mdomo ukimuwasha anaongea chake. Bora rais aje atoe muongozo kama ni lockdown au curfew.
Kuliko huu utoto unao fanywa, mara take away mara kuvaa masendeu!

Sent using Jamii Forums mobile app

Sikuwahi kuwaza kuna siku nitashuhudia Tanzania ambayo kijijini ni salama kuliko Magogoni au makao makuu Dodoma.

Hivi nani inafaa tumlinde zaidi kwa manufaa mapana kama ikitokea hali ikawa mbaya sana kiuchumi? Bakhresa, Mo Dewji au mkulu?
 
Mhe. Waziri alitoa ufafanuzi kuhusu uvaaji wa barakoa. Leo bAsHite anatoa AMri?

Back
Top Bottom