RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

RC Makonda: Yeyote anayeenda katika eneo la manunuzi lazima avae barakoa. Kwenye misongamano watu wakae umbali wa mita 2

Angetoa walau wiki moja watu wavinunue, na hili litawezekana kwa barakoa za vitambaa maana watu wataweza kuzitumia kwa muda mrefu. Ukishaitumia siku hiyo unaifua kwa ajili ya kesho.....zile medical mask za N95 gharama yake ni kubwa, maana itatakiwa ubadilishe kila siku, ni bora ziachwe kwa ajili ya wahudumu wa afya...
 
Wavaa nikabs tunafunika sio pua na mdogo bali uso mzima isipokua macho by default.

Wavaa mitandio inabidi mu upgrade.

Tuendelee kumuomba Mungu wetu mmoja tu muweza wa yote, tuliishi neno na tudumishe ibada.

Singo maza.
 
Wagawe izo barakoa kuanzia ngazi ya kata serikali ya mtaa adi mjumbe wa nyumba kumi mbona wakati wa Jk ugawaji wa vyandarua uliwezekana kaya moja inapata adi vyandarua vitatu

Gaweni izo barakoa na sanitizer msizikalie maofisini

Mabinti kama pesa za kununua pedi zinazotumika mara1 kwa mwezi zinawashinda barakoa wataweza ambazo zinatumika kila siku?
 
Ukitaka kujua "UKAIDI WA WATANZANIA" kesho kuna viongozi wa dini watapanda madhabahuni kufanya ibada kwenye mikusanyiko mikubwa ya watu.
Kesho ni kilele,lazima tujae kumuomba Mungu azuie hili janga ktk inji yetu na dunia.

Tujitokeze kwa wingi tumshinde shetani.

Sent using iphone pro max
 
Agizo liko vizuri lakini anaelitoa najua hayuko serious na hana uwezo wa kufuatilia kama maagizo yake yote..
Halafu mask za vitambaa utazitumia kuzuia vumbi tu lakini virus inapita kama ilivyo..
Huvai mask ili kujikinga na virusi wewe unaevaa, bali unavaa ili kama unaumwa basi utakapokohoa virusi visiende mbali sana hivyo kupunguza uwezekano wa kuambukiza wengine, hivyo ni muhimu kila mtu avae ili tulindane, umeelewa?
 
Kila mtu mdomo ukimuwasha anaongea chake. Bora rais aje atoe muongozo kama ni lockdown au curfew.
Kuliko huu utoto unao fanywa, mara take away mara kuvaa masendeu!

Sent using Jamii Forums mobile app

Wakati unasubiri na ugonjwa utakuwa unakusubiri wewe? Unafukuzwa na simba unangoja kuambiwa kimbia?
 
Yaani mwanaume kamili anaogopa corona...hii ni aibu kwa RC Makonda!
Jack Ma ametoa bure hivi tu eti?
Mnaanza kufanya yaliyokua inabidi yaanze day one!
Day one ilikuwa ni ipi?
 
Sikuwahi kuwaza kuna siku nitashuhudia Tanzania ambayo kijijini ni salama kuliko Magogoni au makao makuu Dodoma.

Hivi nani inafaa tumlinde zaidi kwa manufaa mapana kama ikitokea hali ikawa mbaya sana kiuchumi? Bakhresa, Mo Dewji au mkulu?
Ujinga mtupu!
 
Inaogopa lawama. Sasa hivi kinachofanyika ni kuwatega wananchi, wanawachanganya kwa kauli zao, hali ikiwa mbaya wawalaumu kuwa hawakutekeleza maagizo waliyopewa.

Hawajiamini hawa watu.
Imekuwa MAGANGA wa kienyeji mashariti kibao ukishindwa moja inakuwa sababu duu haya
 
Back
Top Bottom