chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Mtaka ni kama ana serikali yake ambayo haiendani na ya CCM na Samia, hivi mtoto unamfukuza shule ili iweje? Kwanza ni mtoto, anahitaji malezi na maangalizi.
Kwa aina ya waalimu tulio nao, hivi unawapa mamlaka yote hayo?
Mtaka ni moja ya members wazuri wa magrupu ya Chadema, na huwa mchangiaji mzuri wa fedha
==========
Njombe. Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Anthony Mtaka amewaagiza wakuu wa shule za Serikali kuwafukuza wanafunzi watukutu badala ya kuwachapa viboko au kuwarudisha nyumbani.
Mtaka alisema hayo alipozungumza na wanafunzi wa Sekondari ya Wasichana ya Manyunyu, iliyopo Matembwe wilayani Njombe.
Alisema shule si sehemu za watu kufanya mizaha na wazazi wengi wanaheshimu sana shule binafsi lakini za Serikali mambo huwa tofauti.
“Kuna shule za binafsi zikiagiza mwanafunzi aje na nguo mbili wanaenda nazo hizohizo, ukienda na ya tatu unarudishwa, wanakuambia shule hii ni marufuku mtoto kuja na simu ukienda nayo unarudishwa nyumbani, huku kwenye shule zetu za umma tuna mizaha mingi,” alisema.
Mizaha hiyo alisema inasababisha mwanafunzi akifanya vituko na mwalimu akamwadhibu basi mwalimu atajadiliwa hadi kwenye mitandao ya kijamii na polisi watamkamata kuandika maelezo, lakini ujinga huo haufanyiki shule binafsi.
Alisema jamii inapozungumzia maadili ni lazima yasimamiwe na namna ya kuyasimamia ni kuyajenga tangu vijana wakiwa shuleni.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe, Valentino Hongoli alisema “mwaka jana mheshimiwa Rais alitupatia Sh60 milioni ambazo tulijenga madarasa matatu na ofisi shuleni hapa, kama tusingepewa watoto wangeshindwa kusoma.”
Mkuu wa Sekondari ya Wasichana Manyunyu, Advera Bagoka alisema wanafunzi waliotakiwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu walikuwa 202, ila walioripoti ni 120 na 51 wamebadilisha shule, huku 31 hawajulikani walipo.
“Shule yetu ina uhaba wa walimu wa sayansi na hisabati,” alisema.

Mtaka: Mwanafunzi mtukutu afukuzwe shule, asichapwe