RC Rose: Mkoa wa Chato utakuwa na wilaya 5 Kakonko, Biharamulo, Ngara, Bukombe na Chato yenyewe

Sasa mbona umeandika Heading kama tayari imeshapitishwa kumbe ni mapendekezo tu?
 
Pia huko zenji waongeze mikoa
 

Mkuu nadhani uko sahihi. Lakini pia ukiangalia hizi wilaya tajwa ni sehemu ambazo zimesahaulika kiukweli. Mf. Ingawa Ngara ni wilaya yenye mipaka na nchi mbili, tena strategic kwa uchumi wa taifa letu..bado hata barabara ya kufika huko ni mbovu. Maybe mkiwapa mkoa, mtazinduka mjenge miundo mbinu ya kusadia hawa watu. Naamini wanaweza hata kujenga Universities, vyuo vya ufundi nk. Ndo ajira zenyewe.
 
Watu wanachangia kwa mihemuko bila kuangalia uhalisia. Binafsi nakubaliana na hili pendekezo kwa sababu hizi
1. Itarahisisha watu wa biharamulo na ngara kupata huduma kuliko ilivyo sasa
2. Itarahisisha hizo wilaya kutoka Kigoma nazo kupata huduma karibu.
3. Itarahisisha utoaji wa huduma katika mkoa wa Kagera ambao idadi yake ya watu inazidi kuwa kubwa zaidi (ni mkoa wa tatu kwa idadi ya watu lkn bado mkubwa)
4. Kanda ya ziwa inashuhudia ongezeko kubwa la watu kuliko maeneo mengine ya Tanzania kwa hyo kumegwa ni jambo jema.
5. Wilaya zilizopo pendekezwa zina rasilimali nyingi lakini bado zipo chini kimaendeleo, hivyo zikisimamiwa kwa karibu zinaweza kuinuka
Vilevile nipendekeze mambo yafuatayo
1. Makao makuu yawe biharamulo au nyakanazi (kuna uzi humu ulishapendekeza mkoa wa nyakanazi), hii ni kwa sababu hapa ndo katikati.
2. Lakini ili kuondoa mashaka na wasiwasi kwa wapinzani wa Magufuli vilevile jina la mkoa lisiwe chato, naona Burigi litakuwa bora ili kuitangaza na hifadhi ya Burigi
 
Unaunda mkoa mpya kwa kumega ardhi toka mikoa mingine isiyotaka kumegwa!!!!

hahahaha mkuu usiwe stressed..wote tunapita.....JPM alikuwa anasema everything is temporary......hata maisha yetu ni temporary....haya ni majina tuu..Tanzania ni ile ile.....popote ulipo ni geographical accident.
 
brilliant! I would support Nyakanazi au Burigi! Majina mazuri sana hayo. Na yapo Neutral!
 
Mbona wakiufanya mkoa watafanikiwa mno .

Mkoa kagera unaachiwa na wahaya Tu peke Yao.

Biharamulo na ngara hazikuwa wilaya za wahaya Bali wasubi, wasukuma na wahangaza
Hujanipata sawia, alitaka Chato isichanganyike na wasio wasukuma. Kwake wasubi aliwaita wahaya; wanyambo pia aliwaita kuwa ni wahaya nao. Isipokuwa alipokuwa Katoke seminari alichangamana na wahangaza ambao kwake hawakuwa wahaya. Kwake ilimradi lugha yako inasikilizana na wahaya basi ni mhaya na tuseme ukweli hakuwapenda! Hivyo kitendo cha kuingiza biharamulo kuwa part ya chato inaua dhamira yake maana lugha yao inasabihiana na kihaya.
 
[emoji23][emoji23][emoji23]Hakuna kukata kabla ya kona
 
Hakuna umbali huo kati ya Ngara na Bukoba. Ukipita Karagwe ni KM 270 na ukipita Biharamulo ni KM 300. Pili KM haziwezi kuwa sababu ya kugawa kwa sasa, dunia inaelekea kuwa ya kidijitali na umbali wa kimawasiliano unazidi kupungua siku hadi siku.

Tunatumia sababu zisizo na mashiko kuongeza gharama za uendeshaji.
 
Makabila mseto mangapi ? Waha, wasukuma, wasubi, wahangaza na wasumbwa. Na wasukuma watabaki kabila kubwa katika mkoa huo tarajiwa maana Wilaya hizo karibu zote isipokuwa Ngara na Kakonko wasukuma ndio majority
Kabila kubwa pekee lisilokua na umoja wa kuunga kuunga na lenye wivu wa maendeleo ndani kwa ndani ila ni la wachapakazi kweli kweli.
 
Watz wengi sana ukisoma comments unaona ni wajinga, wana wivu na maendeleo ya nchi yao as if sehemu fulani ikiendelea sio ndani ya Jamhuri...wengine with very poor analytical skills wana compare mikoa yenye mapori kama Tabora na Morogoro wanq sahau Geita ni kati ya mikoa yenye population density kubwa per square kilometers. Unataka waanzishe mikoa ku service miti na mapori?
 
Naona wako Sawa Tu. Sema tatizo mkoa umeitwa chato Bora ungeitwa biharamulo na makao makuu yakawa pale.

Mkoa wa kagera wamefanya poa kuugawa na watafanikiwa maana mkoa Una population kubwa na mrefu.kutoka ngara to bukoba ni km 400
Biharamulo vichwa maji tia maji tia maji sana. Wakipewa makao makuu ya mkoa haifumi pale. Hawana ali ya maendeleo pale. Majungu ndiyo yao, ndio maana kamebaki vile vile toka enzi za mjerumani mpaka leo. Ki wilaya ka wajuaji wasiojua kama hawajui. I rest my case.
 
Mbona makabila yanafanana Tu.

Ngara wahangaza
Biharamulo wasubi na wasukuma
Chato wasukuma
Bukombe wasukuma.



Kagera imebakiwa na wahaya na wanyambo Tu na walitofautiana Sana kimaendeleo na kitamaduni na biharamulo na ngara
Umewasahau kabila la waha, aka wanadiaspora
 
Kweli kabisa waitu
 
Sasa unataka umaskini usogezwe Biharamulo makao makuu badala ya kuuvutia pengine ukapunguzwe! Kumbuka pia Kakonko alikua wa kwanza kwa umaskini kwa hiyo kiujumla ni mkoa mpya wenye changamoto na inatakiwa wananchi wachangamke kuukwamua. Anzeni na kuchagua wawakilishi wenye akili za kuwakwamua wananchi na maeneo yao. Wabunge na madiwani, halafu mpewe viongozi wasimamizi wenye uthubutu. Hilo ni eneo potentials sana hasa katika kilimo na ufugaj.
 
Lakini kwa upande wangu naona ni poa kabisa. Hizi wilaya japo juu ziko mbali sana na makao makuu ya mikoa iliyo. Mfano Ngara to Bukoba ni mbali kuliko Ngara to chato. Kwa upande wangu naona imetulia tu.
Endapo hitaji lipo Basi Biharamlo ama Nyakanazi panaweza kuwa Kati . Ngara Hadi Chato ni km 257;Kakonko Hadi Chato km 193;Bukombe Hadi Chato km 137;Biharamlo Hadi Chato km 123; Endapo kigezo ni kuabudu mzimu Basi sawa Ila Kama ni jiografia na kusogeza huduma kwa wananchi kuifanya Chato makao makuu huo mkoa mpya ni uendawazimu, udikiteta,ushamba,ulimbukeni....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…