RC Rose: Mkoa wa Chato utakuwa na wilaya 5 Kakonko, Biharamulo, Ngara, Bukombe na Chato yenyewe


Mkuu tusidanganyane...set up ya utawala wa nchi yetu..Rais ndo mwenye mamlaka na sauti ya mwisho fungu liende wapi! Hukuona JPM alikuwa anawasimanga waliojaribu kuchagua wapinzani wake kisiasa?

Hakuna mbunge anayeleta maendeleo Tanzania!

Ukweli ni kwamba kuanzisha mkoa mpya..angalau itasaidia watu wagawane kidogo kilichopo. Ila kiuhalisia wilaya kama Kakonko, Ngara zilisahauliwa kabisa. Maybe wakipata mkoa..wananchi wanaweza pata fursa kidogo.
 
Lakin bado ni mbali Sana. Yaan ushafika morogoro tayari ukitoka Dar.


Population density na population zinamata imagine kagera ina 3 million people,na density ya 120 people per square km. So ni sahihi Sana kuugawa.

Mkoa kama Dar ni mdogo na unawilaya nyingi sababu ni population density na population.

Ni upumbavu kutengeneza mkoa mpya Kwa sababu ya umbali Tu bila kuangalia population utakuwa mkoa wa nyasi Tu na mbuga mfano kama Lindi yenye density ndogo
 
Hata kagera pia.

Hiv hawajiulizi Kwa nini mkoa wa Dar na Kilimanjaro ni midogo lakin ina wilaya nyingi.
Sababu kuu ni population density na population.


Mkoa kama kagera Una density ya 120 na population above 3million ukiwa wa tatu nchi nyuma ya Dar na mwanza so ni Bora ugawanywe ili watu wawe managed vzr.

Tofauti na mikoa kama Lindi wenye density ya 13 per km
 
Hakuna kinachoshindikana Kwa serikali
 
Tuambie sababu ya JPM kuwachukia wahaya
 
Wengi wanaopinga humu ni wale wanatumia nauli sh 400/=kwenda kupata huduma mkoani. Hivi imagine mtu wa ngara ana kesi Bukoba mjini na anaudhuria karibia kila wiki au mara mbili kwa mwezi, huyu mtanzania wa hali ya chini ataweza??
Kiukwwli hizi wilaya zinahitaji kusogezewa kiuduma karibu
 
[emoji3][emoji3][emoji3]mtu anasema eti na Lindi itengwe!!! Hebu tuwe serious kidogo penye ukweli tuuseme, hili wazo ni zuri
 
Mhh. Uitoe Kahama Shinyanga ibaki na nini ?
Shinyanga si itabaki na wasukuma wa Maswa, Kishapu, Lohumbo na Shinyanga yenyewe: zenye utajiri wa almasi na ng'ombe. Kahama iungane na wanyamwezi wenzao kuunda mkoa wao wa mahama, zao linalopatikana kahama pekee hapa duniani lakini halitambuliki na sasa hivi karibu litapotea kwenye uso wa dunia.
 
Moshi ingeshakuwa mkoa na Kilimanjaro Jiji. zamaaaani sana aisee.hembu angalieniangalieni

Yaani tungekuwa na wilaya ya
1. Pasua
2. Marengo
3. Himo
4. Mwaga
5. Kilema
6. Dar west KLM
7. Uru
8. Kishumundu
9. Rombo
10. Ugweno
 
Ni kweli kama watakuwa fair Bihalamuro pana deserve kumpunguzia umbali mtu wa Ngara na Kakonko nadhani na Bukombe
Makao makuu hayaangalii ukatikati wa eneo, Kuna factor nyingi ikiwemo miundombinu ya ku accommodate huduma na hadhi ya mkoa. Wilaya zingine walikua wanajipanga wakati Biharamulo inapiga porojo. Yaani hata kama B'mulo ingekua ina miundombinu ya kupokea makao makuu sawa tu, hata Kakonko au Ngara ingekua inajitosheleza ingekua vema tu lakini katika wilaya zote pendekezwa,

Wenzenu walikua wanafanya mapokeo kuanzia majengo ya mahakama, vyuo, hospital zenye level ya kanda ukiacha ya wilaya ambayo ipo siku mingi, mahotels, traffic lights, international airport (sio airstrip kama ya katoke) miradi chungu mzima yenye levels ya kikanda na wala si ya kitaifa halafu leo unasema makao makuu yapelekwe Biharamulo ambako hata hospital ya wilaya tu haipo mnang'ang'ana kuijenga pale barabarani like serious mnaomba makao makuu wilaya kongwe Afrika Mashariki tangu enzi za Mjeruman lakini bado unasema ni ya pili kwa umaskini. Kwanini watoto wenu Chato waliendelea kwa kasi hata baada ya kujikata kuliko Biharamulo ?!

Hii Chenga ya mwili ilishapigwa kitambo hakuna namna ni kuwa wapole tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…