Rev. Moses Maghembe ajitoa T.A.G

Rev. Moses Maghembe ajitoa T.A.G

Hahaha huyu jamaa niliwahi kuona video moja kawa mkali sana kwamba waumini hawatoi sadaka na hawamuhudumii mchungaji naye angesusa.

Mahitaji ya wachungaji yameongezeka, wanataka V8, wanataka majumba makubwa, wanataka malipo kwenye kila ibada, halafu wanataka waumini tutoe pesa, na wanataka tushinde na tukeshe makanisani, pesa tunatoa wapi?
 
Mchungaji mwenye msimamo mkali inapokuja suala la kumtumikia Mungu aliye hai Rev. Moses Maghembe ameamua kujiondoa kuwa chini ya usimamizi wa kanisa la mahali pamoja laTanzania Assemblies of God T.A.G

Kama ilivyokuwa kwa wajina wa Maghembe, alikuwepo Moses Kulola ambaye alijitenga na T.A.G na kuanzisha E.A.G.T kwa kutokukubaliana na baadhi ya misingi ya kanisa haswa inapokuja suala la kumtumikia Mungu ipasavyo. Wengi tunafahamu uhodari wa Moses Kulola na huduma yake katika kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Rev. Maghembe ndiye mchungaji pekee alikuwa na uthubutu wa kukosoa uongozi wa askofu Mkuu wa kanisa la T.A.G Dr. Barnabas Mtokambali. Alikosoa kitendo cha kanisa la kiroho kutoa tuzo ya amani kwa mwendazake wakati matukio ya mauaji yalikuwa juu. Pia alikosoa waziwazi maadhimisho ya chama cha vijana ndani ya kanisa C.A.S yaliyofanyika Iringa kwa kufanya bonanza la mpira wa miguu. Maghembe alidai ile siyo njia ya kuhubiri injili ila ni kuishiwa kwa maono na kanisa kuanza kuiga mambo ya kidunia, kanisa linatakiwa kuleta athari duniani na siyo dunia ilete athari kanisani

Kuwa na ministry binafsi au kuwa chini ya uongozi. Wewe uko upande gani?
T. A. G limevamiwa.
 
Unajua ukitaka kugombana na wajinga wa dini uwaeleze ukweli?
Haya makanisa bandia yote yatakufa. Sio wivu, ila ni ukweli mtupu. Hayana vision wala mission. Ukweli na uongo huwa una tabia ya kujitenga
ila usilete habari za ukatoliki ukidhani ndio kanisa la kweli kuliko hayo unayoyaita ya bandia. Fahamu kuwa katoliki ilishaachwa siku nyingi tangu zama za kina Luther
 
Tena yupo aliyewahi kushika wadhifa wa juu katika idara hiyo alikuwa mlokole.
Ni yule aliyekuwa DG wa idara hiyo wakati wa Mwendazake alikuwa Pastor wa Kanisa la Dar City Harvest.
Sijui kama bado anaendelea.
kama sikosei ni balozi mmojawapo ya nchi huko nje, aliteuliwa kutoka dg wa idara hiyo. Hata hawa kina mwamposa msiwachukulie poa mkadhani ni mapastari wa kawaida
 
Nilipuuzia uzi ila baada ya kuona hiyo picha imenibidi nimakinike

Sasa kama unasema mimi siamini Mungu una matatizo
Tunataka kukunusuru hatuko kwa ajili ya kukubembeleza
Almanusura wewe upo kwenye janga
Tunakupa dawa unatema, KAFE

Hebu tupieni video zake mimi nakumbuka hiyo moja tu
 
Back
Top Bottom