Rev. Moses Maghembe ajitoa T.A.G

Rev. Moses Maghembe ajitoa T.A.G

Kadri siku zinavyoendelea, jinsi inavyozidi kunyesha ndio tunaona panapovuja.

Ukristu huu wa kujianzishia makanisa tunavyotaka, umegeuza makanisa kuwa sehemu ya upigaji na wizi, na sehemu ya kula hela za wengi wenye mahangaiko na wasiojitambua.

Kuna wakati inaonekana ni biashara especially barani Africa.

Kwa mfano, hivi kanisa la TB Joshua bado lipo? Linaendeleaje? Mbona baada ya yeye kufa na kanisa nalo limekufa?
Unauliza kanisa la TB JOSHUA kuwa lipo au la ,then unahitimisha kuwa limekufa! 😒
 
Kadri siku zinavyoendelea, jinsi inavyozidi kunyesha ndio tunaona panapovuja.

Ukristu huu wa kujianzishia makanisa tunavyotaka, umegeuza makanisa kuwa sehemu ya upigaji na wizi, na sehemu ya kula hela za wengi wenye mahangaiko na wasiojitambua.

Kuna wakati inaonekana ni biashara especially barani Africa.

Kwa mfano, hivi kanisa la TB Joshua bado lipo? Linaendeleaje? Mbona baada ya yeye kufa na kanisa nalo limekufa?
A Cha uongo aliekwmbia SCOAN limekuf ni nani.... Mbona una chuki na Kanisa la TB Joshua ndugu
 
Mchungaji mwenye msimamo mkali inapokuja suala la kumtumikia Mungu aliye hai Rev. Moses Maghembe ameamua kujiondoa kuwa chini ya usimamizi wa kanisa la mahali pamoja laTanzania Assemblies of God T.A.G

Kama ilivyokuwa kwa wajina wa Maghembe, alikuwepo Moses Kulola ambaye alijitenga na T.A.G na kuanzisha E.A.G.T kwa kutokukubaliana na baadhi ya misingi ya kanisa haswa inapokuja suala la kumtumikia Mungu ipasavyo. Wengi tunafahamu uhodari wa Moses Kulola na huduma yake katika kuishi maisha ya kumpendeza Mungu.

Rev. Maghembe ndiye mchungaji pekee alikuwa na uthubutu wa kukosoa uongozi wa askofu Mkuu wa kanisa la T.A.G Dr. Barnabas Mtokambali. Alikosoa kitendo cha kanisa la kiroho kutoa tuzo ya amani kwa mwendazake wakati matukio ya mauaji yalikuwa juu.

Pia alikosoa waziwazi maadhimisho ya chama cha vijana ndani ya kanisa C.A.S yaliyofanyika Iringa kwa kufanya bonanza la mpira wa miguu. Maghembe alidai ile siyo njia ya kuhubiri injili ila ni kuishiwa kwa maono na kanisa kuanza kuiga mambo ya kidunia, kanisa linatakiwa kuleta athari duniani na siyo dunia ilete athari kanisani

Kuwa na ministry binafsi au kuwa chini ya uongozi. Wewe uko upande gani?

View attachment 3180718
Mathayo 13
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
²⁶ Baadaye majani ya ngano yalipomea na kuzaa, yakaonekana na magugu.
²⁷ Watumwa wa mwenye nyumba wakaenda wakamwambia, Bwana, hukupanda mbegu njema katika konde lako? Limepata wapi basi magugu?
²⁸ Akawaambia, Adui ndiye aliyetenda hivi. Watumwa wakamwambia, Basi, wataka twende tukayakusanye?
²⁹ Akasema, La; msije mkakusanya magugu, na kuzing'oa ngano pamoja nayo.
³⁰ Viacheni vyote vikue hata wakati wa mavuno; na wakati wa mavuno nitawaambia wavunao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita mkayachome; bali ngano ikusanyeni ghalani mwangu.
 
Kama mzee ametoka TAG manake ameona TAG imepotoka inaenda na usasa na kuacha njia ya injili. Mafundisho kuwa ya kimwili zaidi basi hakuna kanisa au dhehebu lililobakia
TAG imekuwa kama serikali, wanahamisha wachungaji hapa na pale, unakuta mchungaji ame hustle kuanzisha tawi yeye na mke wake, tawi likishajaa waumini na kupendeza anahamishwa kwingine akapambane na mazingira mengine mapya. Ukiwa na elimu ndogo ya shule huwi mchungaji. Elimu ya chini ni sekondari na ukasome chuo cha biblia upate diploma hadi degree hapo ndio utafaa vema kuwa mchungaji. Kama ni hivyo wakaongoze wasomi wenye elimu kubwa. Ndugu zao kina EAGT na FPCT nao wamewaiga, wana katiba, sera na mielekeo ya kidunia kama serikali tu
 
Hapo anawaza kuanzisha la kwake apige hela
Apogee hela kutoka wapi. Wengi hawajui kuwa kazi ta kanisa ni ngumu sana hususan ukianza kanisa jipya. Likishapata jina ndipo linapata watu na likiwa na watu wengi ndivyo na mapato huongezeka. Wachungaji wa makanisa madogo wanapitia maisha magumu sana. Wanahitaji kuombewa na kupara sapoti!
 
Back
Top Bottom