Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Kwa ufupi hii ni taarifa tu, so ushauri wako hautabadili chochote wala kuongeza chochote, vipi lakin uzima upo??

Ni hivi, mi huwa siumizwi alafu anayeniumiza akabaki salama, nikiumizwa mi nakuumiza mara 10 alafu fresh, maisha yenyewe mafupi haya, mi niwe na stress alafu wew ucheke ili kiwe nini... sipendagi ubwege kabisa, na nitabaki kwenye kumbukumbu zako milele ukijifanya kuniletea habari za ajabu..

Miez 8 iliyopita nilidate na dada mmoja hivi mrembo, height moja hivi mauzo sana na mzigo wa kuvuta huko nyuma haukuwa haba, kifupi mvuto wa yule dem hauna shaka, kama ni maksi basi A ya 95+... mapema nikamwambia mambo ya kiboya sitaki, km utacheat jitahidi nisijue, nikijua umeumia....Akajifanya hadi kulia pale kwamba ananilove nyang'anyang'a na kamwe hakuna mwanaume kama mimi, nikasema poa but take my words ukinizingua hutoamini nitakachokufany, na km hunitaki niache uende, na kama pia itakuw mechi za dharula tu alafu kimya tuambiane, moyo wangu hauchezewi.. akasema nisiwe na shaka ananipenda, nikasema poa.

Tabia yangu ni kwamba kamwe siwezi kuwa na mpenzi zaid ya mmoja kwa wakati mmoja, so nikiwa na mmoja huyo huyo. Sasa mwezi mmoja nyuma nikausoma mchezo dizain kama demu wangu analiwa hivi, sikumuuliza, nikakomaa hadi nikapata password zake facebook na insta.. nikazama inbox yake, daah ni balaa tupu, ashapigwa mashine na mshikaji mmoja hivi, then jamaa dizain kama anakomaa naye amle 0715 hiv sema demu anabana.. text yake hii hapa..

"Baby naridhika sana nawew, ila unanibania side B, nyimbo za side A zote nimeskiliza why uninyime za side B mpenz?, kama side A nilsikilza kwa elfu 70 bas side B lazma dau lipande.. nielewe bas"

Demu akajibu..

"Mi nina mtu na tuna malengo je akigundua na kuniacha itakuwaje"

Jamaa..

"Hawezi gundua, kwani huwa anakagua huko, ila navyokujua huwez nibania.. nitakutoa out ukafanye shopping ya maana, na nitakutumia 100,000 kesho"

Demu...

"Mmh poa tutaangalia tukikutana tar.22 jamaa akiondoka kama tulivyopanga".

Zipo nyingi nying but hizo kiufupi,....

Mimi kwa huyu demu..., nampa nachopata, najinyima sana apate yeye, nishamtoa shopping za maana mara kibao na tayari nishaandaa pesa nzuri tu kwa ajili yake, Krismass na mwaka mpya, maana tar.hizo sitakuwepo kutokana na majukum ya kazi yangu, nammudu kiujumla, nguo, usafiri, pesa ya kula, malazi nafanya mimi.. yeye hana chochote zaid ya gamba lake la diploma. Muda wote huo sina demu zaid yake.. na on bed naperfom fresh hadi anaomba poo yeye..

Nilichokifanya baada ya kugundua hilo, nimescreenshot charting zote hadi picha walizopiga wakiwa lodge wametumiana kupitia fb messenger nimejitumia kwenye simu yangu, then nimeuchuna.. kifupi tayari nimeshampiga chini ila siwez kumwambia tuachane kiboya boya hiv bila yeye kuonja joto la jiwe kidogo, na kamwe sitafanya naye mapenz tena.. ambacho kimebaki kwake ni kumpa kidonda cha milele..

Ifahamike ananipenda japo tamaa anazo, ashanitambulisha kwa rafiki zake wote, dada yake, hadi mama yake.. kifupi anaitwa mrs mimi... na uchafu anaoufanya ni siri kubwa sana na ndo maana anatumia fb messenger maana anajua siwez hisi chochote huko.. tayari tarehe ya kupeleka barua ishapangwa, tarehe 07 jan... mashangazi zake wote wanajiandaa kwa tukio hilo.. upande wetu pia tunajiandaa..

Nataka nifanye nini?? Siku hiyo ya tukio la kwenda kwao kujitambulisha rasmi ndo siku yangu ya kumuumiza, maana kwao anaaminika sana, anaimba kwaya kanisan, ana vyeo vingi ving vya huko kanisani.. na huwezi mzania hata kidogo kama ni mshenzi.. siku hiyo mbele ya Mchungaji wake, ndugu zake, mama ake, mashangazi na marafiki zake wakiwa na smartphone zao naenda umiza mtu vibaya sana, sio kwamba nitampiga hapana, ila nataka nimafanyie tukio ambalo litaweka maumivu ya kudumu kwenye moyo wake na kamwe hatokuja nisahau..

Tarehe 7 january, save the date....

USIPOTEZE MUDA KUNISHAURI CHOCHOTE, HUWA NIKIPANGA SIPANGUI..
Sas mkuu kama yuko humu Jf sitaar ashausoma mchezo?au ata marafik zake siwatamwambia thn plan itafel
 
Ushauri wangu siku ya tukio nenda na watu kibao kwa ajili ya ulinzi,,,nenda njombe ukajizindike,tafuta bastola ya kutishia,,,,kwani ukifanya hayo utakua umejisogezea Sikh zako za kifo
 
Uliwezaje kupata password? Hapo nahisi pana ukakasi ni rahisi kupitia account kwa kutumia simu yake pamoja na hivyo ni vigumu kuzipata labda kama alizinote mahali jambo ambalo kwa watu wa leo sidhani
 
Sasa kama unajua hautaki ushauri umeweka thread hapa ili iweje? Au ndo unataka tukusaidie kukupatia namba za wapiga picha waje siku ya tukio!

Tunasubiria part 2 tujue kilitokea kitu gani but be very careful

Happy new year in advance
Kwani kila thread inaomba ushauri?
 
Kama unampenda kweli mkomoe huyo jamaa sio demu wanawake ni wadhaifu panga fumanizi then umkomeshe huyo jamaa pia msaidie dada wa watu asiharibiwe na huyo jamaa

Mapenzi mabaya kupenda kubaya sana najua unafanya hivyo ila pia hilo jambo litakuuma sio mchezo utatamani usingefanya hivyo
 
Daahh. Usingizi wote umeniisha kwa hii post. You will kill the guy,

Huo ni ushenzi hata mamako mzazi atakulaani kwa huo upuuzi, Ndugu zao pia watakulaani kwa huo ujinga. Humtaki mtobolee ushenzi wake zen sepa.
Aaahhh!! hata ivyo hutaki shauriwa ....kafie mbele
Dawa ya uahenzi ni ushenzi,demu wake naye angemwambia mumewe mtarajiwa kua yeye ni msaliti tena analiwa hadi tigo halafu asepe amuache jamaa kuliko kuacha hadi jamaa agundue mwenyewe.
 
Kwa ulichopanga kumfanyia ikatokea umemkosa Nina uhakika utamtoa roho msichana wa watu. We ni hopeful prisoner.
 
Kama sio Chai za Jf basi kazi ipo mkuu.


Pole Sana, lakini pia angalia unaweza kumdhalilisha/kumuumiza lakini ukajikuta umejifedhehesha mwenyewe na ukadharaulika mbele ya Jamii yako iliyokuheshimu.
Hakuna jamii itakayomdharau,watakaomdharau jamaa watakua ni waungaji wakubwa wa vitendo ovu kama anavyofanya huyo mdada.
 
Mwenzenu revenge yangu n kukaa kimya nashangaa ndo hua inamuumiza my dear ex ,haishi kuniomba msamaha japo niliwah mwambia nishamsamehe na awe na Amani ...,ila naona hua haamin kama nilisamehe.
Kwasababu hamcherewi kulipiza kwa gume gume
 
Back
Top Bottom