Ripoti ya CAG 2021-2022: CAG apendekeza iundwe Tume Huru kuchunguza ukiukwaji kwenye Plea Bargain

Wakusanyaji wa jiwe hao.
 
Time huru ya kazi Gani? Kwani walio kuwa kwenye hicho kitengo hawajulikani?
Alie kuwa ana pokea mkwanja hajulikani?
Yaani Hela zimesha potea na bado man taka kula nyingine?
 
Ukweli ni kwamba chini ya chama Cha mapinduzi serikalini kote wanaiba na hawaoneani aibu. Na utawala wa mama watakula hadi wavimbiwe kwa miaka elfu tatu ijayo
 
tuliza mzigo huo mtoto wa juzi, unadandia behewa kwa mbele una pumzi? Mnachunguza nini wakati mlituambia pesa ziko china na account mnaijua? Hamjazichukua mnangoja nini? Chunguzeni tuone mtamfunga nani
Usikariri wapi kwa kudandia..!! Utakufa bure..!! Kama behewa linakwenda mbele unadandia nyuma, na kama linarudi nyuma unadandia mbele..!! So, inategemea uelekeo..!!
 
Naunga mkono hoja. Kamato huru iundwe haraka sana ikojumuisha watu ambao maadili yao siyo ya kutilia mashaka. Miongoni wawemo Musa Assad na Ludovick Utouh.
 
Hawa Jamaa walikusnaya 6.1 b wakapeleka 1.3 B tuu zingine 3.7 zote wamepiga
Nafikiri 3.7B sio kubwa kama hawa waliobadili deal mwishoni kabisa kwenye manunuzi ya ndege ya mizigo wametupiga 49B mkuu alafu wameambiwa eti wajitathimini waachie nafasi zao nafikiri wanapaswa kufukuzwa haraka sana then wapewe kesi ya uhujumu uchumi.
 
Iweje hela zinazoonekana ni Bilioni 6 wakati
Mr Kuku mwenyewe Pesa alizotoa ni Zaidi ya Bilioni 5.7?

Yusuph Ali alipeleka Bilioni 1 Cash

Hadi hapo hela zishazidi 6.7bil
 
CC TikTok2021, Oxpower, KimpaGhasha, MISULI, johnthebaptist, Mayor Quimby, PakiJinja et el
 
Angetaja hiyo account sijui ya china na walisema Kuna pesa ndefu mbona CAG anataja pesa tofauti Kuna walakini hapa ...Wako sahihi kuunda tume
CAG amekagua karatasi za DPP

Serikali imefatilia barua za Plea

Ukweli utajulikana Mwezi wa 5
 
Naunga mkono hoja.

Tume ya uchunguzi iundwe mara moja na kwa haraka ili kuupata ukweli. Tume iundwe na watu ambao maadili yao hayatii shaka. Miongoni mwa wajumbe awemo Musa Assad, Ludovick Utouh, na wanasheria nguli wanaozijua sheria za kimataifa. Kama itadhihirika bank ya China ilifungua account kinyume cha miongpzo ya sheria za kimataifa, basi na yenyewe ijumuishwe kqenye mashtaka.
 
Majizi aijalishi yalikuwa awamu ipi huyo TAKUKURU achunguze tu kama kuna watu walijitajirishia huko.

Lakini ukweli unabaki palepale hakuna mtu alielazimishwa kuingia kwenye plea bargain (mfano Rugemalila, hakutaka).

Wengi walioingia kwenye hayo makubaliano ni majizi in the first place ambayo hayakutaka kukaa jela, yanashutuma ya ubadhirifu wa mali za umma, wenye ushahidi na yenyewe yakadhulumiwa na majizi mengine ili yasiende jela.

Hizo mali na hela walitoa kwa ridhaa zao wenyewe ili waachiwe baada ya kukutwa na kesi ya kujibu. Sasa kama na DPP nae alikuwa na syndicate yake achunguzwe tu. Lakini tuache kuongelea kama vile hawa watu walioingia plea bargain walikuwa innocent victims, hapana hii na yenyewe wengi wao ni majizi pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…