Ripoti ya CAG 2021-2022: CAG apendekeza iundwe Tume Huru kuchunguza ukiukwaji kwenye Plea Bargain

Ripoti ya CAG 2021-2022: CAG apendekeza iundwe Tume Huru kuchunguza ukiukwaji kwenye Plea Bargain

Hakika hii NCHI Umdhaniea Ndio kumbe sio na Umdhaniae SIO kumbe NDIO
REPORT ya MKUGUZI MKUU wa HESABU za SERIKALI CAG kaikabidhi REPORT yake ya MAHESABU ya SERIKALI kwa MH.RAIS kwa MUJIBU ws KATIBA.MADUDU tumeyasikia hakika Hii NCHI INAIBIWA sana na WATU waliopewa MAJUKUMU ya KUKUSANYA na KUTUNZA FEDHA za SERIKALI.
Inasikitisha sana kuona WATU WACHACHE wanaiba FEDHA nyingi ambazo zingewanufaisha WANANCHI WENGI lakini SERIKALI imekaa KIMYA kama vile HAKUNA KILICHOIBIWA.MDHIBITI na MKAGUZI MKUU wa FEDHA za SERIKALI CAG kafanya UCHUNGUZI wake na KUBAINI WIZI MKUBWA wa FEDHA za PLEA BARGAING ulivyofanyika .Zinakusanywa BIL.6 lakini BIL.1 ndio inapelekwa HAZINA
Kuna kipindi MH.RAIS alisema kuna AKAUNTI ya Fedha hizo imefunguliwa Nchini CHINA ukweli UCHUNGUZI ufanyike ili UKWELI wa FEDHA hizo UJULIKANE.
Pia CAG kazungumzia BIL.11 zilivyoyeyuka ktk HALMASHAURI ZETU huko nako UCHUNGUZI Ufanyike WAHUSIKA Wafikisgwe kwenye MAHAKAMA za UFISADI.
Kuna Mashirika kama ATCL TANESCO na TTCL kila siku NI HASARA TU binafsi naamini ni WIZI ndio MKUBWA kwenye MASHIRIKA HAYO
OMBI kwa VYAMA vya UPINZANI kwa Kuwa BUNGE letu limeshindwa KUIBANA SERIKALI juu ya UFISADI MKUBWA kama huu Tunawaomba WAPINZANI MPAZE SAUTI ZENU ili UCHUNGUZI UFANYIKE na WAHUSIKA Wafikishwe Kwenye MAHAKAMA ya MAFISADI ili Mafisadi wengine WAOGOPE kuiba FEDHA za UMMA.View attachment 2570005View attachment 2570006View attachment 2570008
Wakusanyaji wa jiwe hao.
 
Time huru ya kazi Gani? Kwani walio kuwa kwenye hicho kitengo hawajulikani?
Alie kuwa ana pokea mkwanja hajulikani?
Yaani Hela zimesha potea na bado man taka kula nyingine?
 
Ukweli ni kwamba chini ya chama Cha mapinduzi serikalini kote wanaiba na hawaoneani aibu. Na utawala wa mama watakula hadi wavimbiwe kwa miaka elfu tatu ijayo
 
tuliza mzigo huo mtoto wa juzi, unadandia behewa kwa mbele una pumzi? Mnachunguza nini wakati mlituambia pesa ziko china na account mnaijua? Hamjazichukua mnangoja nini? Chunguzeni tuone mtamfunga nani
Usikariri wapi kwa kudandia..!! Utakufa bure..!! Kama behewa linakwenda mbele unadandia nyuma, na kama linarudi nyuma unadandia mbele..!! So, inategemea uelekeo..!!
 
Naunga mkono hoja. Kamato huru iundwe haraka sana ikojumuisha watu ambao maadili yao siyo ya kutilia mashaka. Miongoni wawemo Musa Assad na Ludovick Utouh.
 
Hawa Jamaa walikusnaya 6.1 b wakapeleka 1.3 B tuu zingine 3.7 zote wamepiga
Nafikiri 3.7B sio kubwa kama hawa waliobadili deal mwishoni kabisa kwenye manunuzi ya ndege ya mizigo wametupiga 49B mkuu alafu wameambiwa eti wajitathimini waachie nafasi zao nafikiri wanapaswa kufukuzwa haraka sana then wapewe kesi ya uhujumu uchumi.
 
Iweje hela zinazoonekana ni Bilioni 6 wakati
Mr Kuku mwenyewe Pesa alizotoa ni Zaidi ya Bilioni 5.7?

Yusuph Ali alipeleka Bilioni 1 Cash

Hadi hapo hela zishazidi 6.7bil
 
Katika Ripoti yake iliyotolewa leo, CAG amesema hivi, Nanukuu "Napendekeza Iundwe Tume Huru ya kuchunguza uwezekano wa ukiukwaji wa Maadili na Matumizi Mabaya ya Ofisi ya Umma katika mchakato wa kukiri kosa na kutaifisha mali za watuhumiwa" Mwisho wa kunukuu.

Mimi binafsi naunga mkono hoja hii na ninaamini wapenda haki wote Tanzania wataunga mkono jambo hili.

Halafu Tume hii ikiundwa haitakuwa na kazi ngumu sana, wahusika wote wa jambo hili bado wako hai na wanapatikana kirahisi tu, wengine ni hawa mnawaona pichani, hawa wote wako hai na wangali maofisini.

--
Pia soma > Rais Samia: Nyuma kidogo pesa za plea bargaining nyingine uki-trace uliambiwa kuna akaunti China

View attachment 2570026
CAG Charles Kichere​
CC TikTok2021, Oxpower, KimpaGhasha, MISULI, johnthebaptist, Mayor Quimby, PakiJinja et el
 
Angetaja hiyo account sijui ya china na walisema Kuna pesa ndefu mbona CAG anataja pesa tofauti Kuna walakini hapa ...Wako sahihi kuunda tume
CAG amekagua karatasi za DPP

Serikali imefatilia barua za Plea

Ukweli utajulikana Mwezi wa 5
 
Naunga mkono hoja.

Tume ya uchunguzi iundwe mara moja na kwa haraka ili kuupata ukweli. Tume iundwe na watu ambao maadili yao hayatii shaka. Miongoni mwa wajumbe awemo Musa Assad, Ludovick Utouh, na wanasheria nguli wanaozijua sheria za kimataifa. Kama itadhihirika bank ya China ilifungua account kinyume cha miongpzo ya sheria za kimataifa, basi na yenyewe ijumuishwe kqenye mashtaka.
 
Majizi aijalishi yalikuwa awamu ipi huyo TAKUKURU achunguze tu kama kuna watu walijitajirishia huko.

Lakini ukweli unabaki palepale hakuna mtu alielazimishwa kuingia kwenye plea bargain (mfano Rugemalila, hakutaka).

Wengi walioingia kwenye hayo makubaliano ni majizi in the first place ambayo hayakutaka kukaa jela, yanashutuma ya ubadhirifu wa mali za umma, wenye ushahidi na yenyewe yakadhulumiwa na majizi mengine ili yasiende jela.

Hizo mali na hela walitoa kwa ridhaa zao wenyewe ili waachiwe baada ya kukutwa na kesi ya kujibu. Sasa kama na DPP nae alikuwa na syndicate yake achunguzwe tu. Lakini tuache kuongelea kama vile hawa watu walioingia plea bargain walikuwa innocent victims, hapana hii na yenyewe wengi wao ni majizi pia.
 
Back
Top Bottom