Ripoti ya CAG 2021-2022: Rais Samia ataka baadhi ya mashirika yasiyo na tija kufutwa

Namuunga mkono mama
 
Namuunga mkono kwa hili, hakuna haja ya kung'ang'ana na mavitu yanayotafuna pesa za walipa kodi tu bila umuhimu wowote.
Kama mashirika tumeshindwa kuendesha si hata serikali yenyewe tumeshindwa pia? Shirika lililopo chini ya wizara tunasema tumeshindwa, alafu wizara tumeweza? Haiingii akilini
Kama kufuta basi na wizara nazo zifutwe
 
TTCL ni kampuni ya umma, naiona hatari simu nyeti kama za ikulu na Usalama zikipitia kampuni binafsi, ambazo wanahisa ni wale mabeberu.

TTCL wabaki na land line na miundombinu wezeshi ya mawasiliano
Hapa ndiko CCM yenu ya wezi na wavivu ilipotufikisha. Shirika kama hili linashindwaje kuendeshwa kwa faida kama siyo hujuma? Mkurugenzi, bodi na mazagazaga kibao si yanateuliwa na rais?
 
Tanesco walichofanya wameuza madeni yao yote kwa serikali. Hata hayo mashirika yakifanya hivyo hutaona hasara.

Najiuliza ilikuwaje mama samia alikubaliana na hawa kina maharage kuuza madeni ya Tanesco kwa serikali
Wewe umetoa wapi hizo hasara maana leo tanesco hajatajwa kabisa
 
TTCL ni kampuni ya umma, naiona hatari simu nyeti kama za ikulu na Usalama zikipitia kampuni binafsi, ambazo wanahisa ni wale mabeberu.

TTCL wabaki na land line na miundombinu wezeshi ya mawasiliano
Kwani hujui Rais hutumia namba ya Voda?

Serikali ina 49% Airtel
 
Tanesco walichofanya wameuza madeni yao yote kwa serikali. Hata hayo mashirika yakifanya hivyo hutaona hasara.

Najiuliza ilikuwaje mama samia alikubaliana na hawa kina maharage kuuza madeni ya Tanesco kwa serikali
Hana ''kichwa'' cha kuweza kujisimamia chenyewe. Japokuwa sikatai akubali ushauri lakini kuna mambio mengine hata kwa common sense ya mwenyekiti wa kijiji ni upumbavu kukubaliana nayo.
 
Serikali haifanyi biashara, mashirika kama TRC au TTCL waachiwe wawekezaji alafu serikali iwe mbia tu awe anakula tozo na gawio lake
Walishadanya hivyo ikashindikana. Tumesahau ATCL tuliingia ubia na South Africa? Mwisho shirika ndio likawa mfu
Ttcl tulifanya hivyo tena chini ya waziri mwandosya, mwisho wa siku shirika likawa mfu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…