Ripoti ya CAG 2021-2022: Rais Samia ataka baadhi ya mashirika yasiyo na tija kufutwa

Ripoti ya CAG 2021-2022: Rais Samia ataka baadhi ya mashirika yasiyo na tija kufutwa

Unaweza kuwa sahihi, lakini kuna baadhi ya mashirika yameuwawa na hawahawa tuliowaamini. TANESCO bila mikataba feki kama IPTL na kina DOWANS ingekuwa inajiendesha kwa faida.

Serikali makini ingeshughulika na hawa waliotuingiza kwenye mikataba tata ili kuwafundisha wengine wanaokusudia kutuhujumu kuwa kuna kuwajibika.

Tumewahi kuwapa wahindi TRC, hali ilikuwa mbaya zaidi kuliko ilivyokuwa chini ya serikali.
TANESCO hata kabla ya IPTL na DOWANS, haijawahi kutengeneza faida. Tatizo ni aina ya watu walioko huko.
 
TTCL itasimamaje mbele ya Rostam
ATCL itasimamaje mbele ya Rostam
Hapo ndo tuseme hatuna letu tena

Ttcl kwa namna moja au nyingine hawabebeki tena. Walibebwa na jpm na walikuwa na nafasi kubwa sana kufanikiwa ila wakajisahau mazoea yakarudi. 0 creativity as usual
 
Hapana havihusiani maana unaweza kuta katika hio wizara kuna mashirika mengine yanafanya vizuri.... inawezekna wewe ni mtumishi humo usijali utahamishwa taasisi hutofukuzwa kazi
Umeshaondoka kwenye point, Mimi sio mtumishi mimi napambana na box. Shirika kufanya vibaya solution yake sio kulifuta.

Shirika kufanya vibaya tafsiri yake ni uongozi mbaya. Ndio maana nikasema kama shirika ambalo lipo ndani ya wizara linafanya vibaya vipi kuhusu wizara?

Kuna wizara mara nyingi amekua akilalamika kufanya vibaya, mbona hatuzifuti?
 
TTCL ni kampuni ya umma, naiona hatari simu nyeti kama za ikulu na Usalama zikipitia kampuni binafsi, ambazo wanahisa ni wale mabeberu.

TTCL wabaki na land line na miundombinu wezeshi ya mawasiliano

Hizo watabaki nazo. Sio kwamba watafuta operation zote
 
Ttcl haiwezi kufanikiwa sababu mafisadi papa kutoka CCM ndio wamiliki wa makampuni binafsi yanayoshindania soko. Juzi wamezuia kampuni ya kimarekani liyotaja kuwekeza mtandao wa intaneti wa bei nafuu kwa sababu za kitoto zilizotolewa na mtumishi wamafisadi Nape Mnauye
Yule mpumbavu m'moja ninamchukia takataka yule.
 
Ni rahisi waweke sheria kali tu wanaweza
Sheria mbona zipo toka kitambo,sema huyo wa kuzisimamia hizo Sheria kwa uwadilifu ndiyo hatuna, watu wakija na Asali tu Sheria inawekwa pembeni ili watu walambe Asali kwanza!!
 
Hii nchi ishalogwa
Kufuta shirika sio solution, Leo amesema kuwa wakati wa matengenzo ya ndege invoice ilikua ni bilion 60. Ghafla akaletewa tena invoice nyingine gharama zimeongezeka badi bil 200, alipouliza akaambiwa vifaa vimepanda bei.

Kwa mfano huo hapo tatizo ni kufuta shirika? Kwa nn hapo hapo asianze kutoa mfano kwa mtu kama huyo?

SGR gharama za ujenzi kwa kilomita 1 zimeongezeka sana kipande kipya cha Tabora-Kigoma, tofauti kabisa na vipande vingine vyote. Hapa bado tutaona tatizo ni kufuta shirika? Hawa wakishindwa kufanya shirika si wanaamia kwenye wizara na miradi mingine?
 
TTCL ni kampuni ya umma, naiona hatari simu nyeti kama za ikulu na Usalama zikipitia kampuni binafsi, ambazo wanahisa ni wale mabeberu.

TTCL wabaki na land line na miundombinu wezeshi ya mawasiliano
Haaaà sasa unahic TTCL ipo salama unajua wanatumia satellite zipi
 
Hivi inakuwaje Shirika kama TRC kuendeshwa kwa Hasara?
Kama mteja anahitaji mabehewa 80 ya kusafirisha mizigo hadi kigoma inayokwenda DRC,wao wanakwambia tunayo 15 tu!!hapo kuna nini?njia ya treni haifanyi kazi kwa kiwango chake inavyotakiwa,lazima tu gharama za uendeshaji zitakuwa juu!!
 
TRC isifutwe bali atafutwe mwendeshaji, ikiwezekana kampuni ya nje ya nchi. Watumishi wa Serikali jawana kabisa weledi wa biashara au uchumi.
Sasa Nchi yote tuwakabidhi Wabia waiendeshe Kama sisi wenyewe tumeshindwa! Kama hatuwezi hata kuwajibishana kwenye hizi hasara zinazo thibitiswa na CAG unatagemea Kama Watu wataogopa kulamba Asali Kama Mchwa!!?
 
Back
Top Bottom