Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Humu 80% ni blabla tu hakuna facts ya maana, ATCL ni loss ya bil 60 kwa miaka mitano, ni loss sio wizi, uendeshaji wa shirika lenyewe, takribani mashirika yote yamekula loss, suali lingekuwa je pamoja na loss ya mashirika yote haya mbona bado wanaendelea na biashara hiyo?.
 
Siku ya leo sijui tuuiteje huko; Mbaya? Au nzuri sana?

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali inayoendelea kusomwa muda huu si kwamba tu inawaweka CCM na watetezi wa mwendazake kwenye wakati mgumu sana, lakini tayari imechefua wananchi wengi kwa kiwango kisichomithilika.

Madudu ya SHUJAA WA AFRIKA yanatisha na kutia kinyaa.

Madudu ya MTETEZI WA WANYONGE Yanatia hasira sana.

Chukulia hili moja BILIONI 3.9 kwenye matengenezo ya ndege moja ambayo HAIKUFAA![emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]

Upinzani uliwahi kusema upigaji wa awamu hii utavunja rekodi, watu wakabeza sana. Lakini wakati ni hakimu mzuri. Uongo hupanda lift lakini ukweli hukwea ngazi. Mahakama ya mafisadi inaweza kuanzia pale kwenye nyumba ya milele ya mwendaAzakwe marehemu hayati.

Huu uozo uliendelea kuwekwa wazi peupe hivi tusishangae kuona siku moja marehemu akalikimbia kaburi lake. N itokee kuna kitu kinaitwa maandamano kifanyike[emoji848][emoji848][emoji848] Bila udhibiti imara si ajabu kuwakuta waandamanaji wakilicharaza bakora kaburi la shujaa wa Afrika na kuipopoa mawe picha yake.

Baada ya kusomwa hii ripoti, masikio yote yako kwa Bimkubwa. Je, atasemaje? Watu wamefura kwa hasira. I hope hatawazingua
Mahabusu ziandaliwe za kutosha sasa. Ni zamu ya kubadilisha wapangaji. Karibia kila wizara ina vimeo vya kutisha.
Sikubaliani na kinacholengwa na mada hii; kwamba "JPM alikuwa fisadi mkubwa na anaumbuliwa na ripoti ya CAG". Ukweli ni kwamba ni kweli kulikuwa na maovu yaliyokuwa yanaendelea tangu awamu zilizotangulia na JPM alikuwa akipigana na hayo na kuwaasa Watanzania wamsaidie kuyafichua na kumuombea. Hivi ni sahihi kweli kumlaumu JPM kwamba alijenga ukuta Mererani lakini wizi unaendelea na kwa hiyo hatua alizochukua zilikuwa ni za kidhalimu? Kitu sahihi ni kusema hatua zilichukuliwa kwa nia njema kutatua tatizo lililokuwepo lakini hazikuzaa matunda yaliyotarajiwa. Siyo kwa sababu mtekelezaji alikuwa na nia mbaya ya ufisadi. Mada inaashiria kwamba JPM alikuwa fisadi mkubwa akijificha kwenye kivuli cha kutetea wanyoge. Huo ndio ukweli wenyewe japo hakufanikiwa katika matakwa yakwe sawasawa na Nyerere alivyoshindwa katika siasa yake ya ujamaa na kujitegemea. JPM alifichua ufisadi uliokuwa ukifanyika Muhimbili na mahospitali mengine. Akaweka kingingi. Mashine za kupimia zikafufuliwa ndani ya wiki mbili; wagonjwa wakawa wakipata dawa kwenye famasia za hospitali ambapo awali ya hapo walikuwa wanaambiwa wakanunue kwenye famasia za binafsi; vitanda vikapatikana kwa wagonjwa ambapo zamani walikuwa wakilala wagonjwa kadhaa kwenye kitanda kimoja na wengine sakafuni. Siyo sahihi kusema kwamba Awamu ya Tano ilikuwa imejaa uozo na kiongozi wake alikuwa fisadi. Hii nakataa kabisa. Sahihi ni kusema kwamba Awamu hiyo ilijitahidi kurekebisha uozo lakini haikufanikisha iliyotarajia kwa asilimia 100; na tuongeze kwamba kutofanikiwa huko kulitokana na ushirikiano mdogo kutoka kwenye jamii kuwafichua wapinga maazimio ya juhudi za serikali.
 
Mikutano na maandamano ya vyama vingi hutaki....wabunge wa upinzani hutaki....bunge live hutaki..... vyombo vya habari hutaki....wanaharakati hutaki....wakosoaji hutaki....haya ndio matokeo yake.
Kichwa chako kina akili nyingi kupitiliza,Kama wanasayansi wangegundua kumuongezea mtu mwingine akili Kama vile mtu anavyoongezewa damu,tungekuomba ukawaongezee watu wa Lumumba,hasa hawa wa buku 7 maana wanapiga hela bure tu.
 
Siku ya leo sijui tuuiteje huko; Mbaya? Au nzuri sana?

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali inayoendelea kusomwa muda huu si kwamba tu inawaweka CCM na watetezi wa mwendazake kwenye wakati mgumu sana, lakini tayari imechefua wananchi wengi kwa kiwango kisichomithilika.

Madudu ya SHUJAA WA AFRIKA yanatisha na kutia kinyaa.

Madudu ya MTETEZI WA WANYONGE Yanatia hasira sana.

Chukulia hili moja BILIONI 3.9 kwenye matengenezo ya ndege moja ambayo HAIKUFAA![emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064]

Upinzani uliwahi kusema upigaji wa awamu hii utavunja rekodi, watu wakabeza sana. Lakini wakati ni hakimu mzuri. Uongo hupanda lift lakini ukweli hukwea ngazi. Mahakama ya mafisadi inaweza kuanzia pale kwenye nyumba ya milele ya mwendaAzakwe marehemu hayati.

Huu uozo uliendelea kuwekwa wazi peupe hivi tusishangae kuona siku moja marehemu akalikimbia kaburi lake. N itokee kuna kitu kinaitwa maandamano kifanyike[emoji848][emoji848][emoji848] Bila udhibiti imara si ajabu kuwakuta waandamanaji wakilicharaza bakora kaburi la shujaa wa Afrika na kuipopoa mawe picha yake.

Baada ya kusomwa hii ripoti, masikio yote yako kwa Bimkubwa. Je, atasemaje? Watu wamefura kwa hasira. I hope hatawazingua
Mahabusu ziandaliwe za kutosha sasa. Ni zamu ya kubadilisha wapangaji. Karibia kila wizara ina vimeo vya kutisha.
Nafikiri kosa kubwa la mwendabure ni
1- ushamba
2- kibri
3- misifa
4- zarau
Vitu hivi si rahisi kuvistukia kama unavyo labda MOLA apende uvijue ili uchukue hatua ya kuachana navyo kinyume na hapo salio la oxygen linakata ghafla yaani.
 
Ni kweli kabisa kuwa ufisadi uliofanyika kipindi hiki cha mwendazake kinavunja rekodi ya tawala za awamu zote tokea nchi ipate Uhuru wake toka kwa mkoloni.
Na watawala wanahusika moja kwa
Sio vyema kumsema vibaya marehemu hubiri yale yake mazuri!
Kwa yale mazuri aliyoyafanya (kama yapo) alishalipea mshahara. Sasa ni wakati wa kushughulikia yale mabaya.
 
Kaka Mshana wewe ni mzoefu, nadhani unakumbuka ripoti ya 2014 ambapo hoja karibu zote zilipanguliwa! Nadhani hata hizi ngoja ziende Bungeni. Nina mdogo wangu mahali ananiambia watu wanakimbizana kujibu hizi hoja.

Najiuliza walikuwa wapi kabla? Huu ni uzembe wa hali ya juu. Tunaimani na Bi Mkubwa kuwachukulia hatua wahusika kabla hawajaichafua serikali ya awamu ya sita.
  • Ikithibitika wizi na ufisadi fukuzaa
  • waliichelewa kujibu hoja fukuzaaa
  • waliohonga hela pale OR TAMISEMI wakapata hati safi na kwenye ma taasisi ya umma fukuzaaaa! Wakiwemo hao watumishi wa CAG

Wanadamu ni wabaya sana jamani wasimzingue mama!
Ha ha haa,hoja za ukaguzi wa maodita wakaguliwa huwa wanapewa muda maalumu wa kuzijibu.
Kinachokosa majibu ndio huwa kinapelekwa Bungeni.
Ingekua hivyo unavyosema wewe ingekua vurugu tupu.
 
9BF1136A-6605-468B-B8C2-4B7387324A67.jpeg

Yanapigwa chini tunaanza bandari..

Mponde Magu mfaidishe JK..

Mtaimba mapambio milele
Hadi polepole alijifanya CAG na kutoa mchanganuo wa 1.5T.....ndo maana naamini hata haya mamiradi ya SGR, stiglaz, Busisi, na manunuzi ya ndege yatakuwa na upigaji wa kufa mtu....
 
Nchi bila kuweka sheria kali za kuwadhibiti wezi wizi hautokwisha hata aje nani kungoza, pia mfumo wetu ubadilike
Hakuna Sheria kali bila katiba mpya
Na CCM hawataki katiba mpya wanajua ndio mwisho wao

Bila ccm imara nchi itayumba-Nyerere
Mtanikumbuka kwa mema-magufuli
Kazi ieendelee-mama samia
 
Shida yetu kubwa ni kwamba tunapojadili haya mambo hatuji na masuluhisho. Na kila mwaka ni yale yale. Upigaji wa kutisha!

Kama jamii tufanye nini ili kuikomesha hali hii? Tunawezaje kuukomesha ufisadi? Kwa nini viongozi wetu wanakuwa hivi? Tufanye nini?

Mwendazake keshalala. Hata tukipopoa mawe na kucharaza bakora kaburi lake hatatusikia. Kimbembe ni kwetu tuliobakia. Ni kweli hatuwezi kuikomesha hali hii?
Katiba na kuiondoa CCM madararakani.
 
Yanapigwa chini tunaanza bandari..

Mponde Magu mfaidishe JK..

Mtaimba mapambio milele
Na hapa bado ripoti ya July 2020 mpaka March 2021 itakuwa mbaya sana... Mtulie wananchi wafurahie matunda ya Demokrasia ambayo waliyakosa muda mrefu..
 
Ni kweli kabisa kuwa ufisadi uliofanyika kipindi hiki cha mwendazake kinavunja rekodi ya tawala za awamu zote tokea nchi ipate Uhuru wake toka kwa mkoloni.
NIMEANZA KUELEWA KWANINI UTEUZI WA KICHERE ULITILIWA MASHAKA KIPINDI ANAINGIA KUHUDUMU OFISI YA CAG.
 
Maliasili pekeyake BILION 34 matumizi yasiyo na stakabadhi! Bado akabebwa na mbeleko bwana HK kumbe kule kuhangaika na waganga kulikusudia kuficha mengi.
Utawala wa bwana yule hivyo ni VIJISENTI. Bado ninaendelea kujumlisha hizo tuhuma zikifika pigo moja la ESCROW mnistue.
 
Magu aamshwe aeleze kwaa nini alitudanganya
Tutajie mifano ya vitu tulivyokuwa tukidanganywa. Mwingine hapo chini anazungummzia ATCL na kuashiria kwamba shirika limelipa Taifa hasara, na yote haya ni kwa sababu ya 'ufisadi' wa JPM. Sasa nikuombe uchunguze mashirika makubwa zaidi ya ndege kama KLM, British Airways, Lufthansa na SwissAir, na utupe mchanganuo wa biashara zao kwa mwaka jana. Ukweli ni kwamba mwaka haukuwa mzuri kwa biashara ya ndege kutokana na corona na si kwa sababu ya ufisadi wa JPM.
 
Back
Top Bottom