Huyu naye anapotoka sasa; majukumu yake kiktaiba ni haya matatu, hilo la kuhakikishwa watumishi wanapandishwa madaraja sio mojawapo. CAG hana jukumu la kukagua kama watu wanapandishwa madaraja labda tu kama mahesabu yataonyesha kuwa walilipwa kwa kupandishwa madaraja hayo hewa. Angalia Katiba
View attachment 1747174
Nchi hii kila mtu anataka kuonyesha power baada ya Magufuli kuondoka. Hata sheria ya CAG tena the most recent ya mwaka 2020 nayo inaweka wazi majukumu yake yanahusiana na mahesabu ya hela na mali za umma tu:
View attachment 1747178
View attachment 1747180
View attachment 1747181
Hili la watu kupanda madaraja nadhani ni namna ya kutaka kupendwa na wahanga wa kutokupanda madaraja. Point ya nyongzea za mishahara na kupanda madaraja ninaijua kuwa kila mara mishahara ilipokuwa inapanda, ama thamani ya shillingi ilikuwa inaporomoka au bei za vitu zilikuwa zinapanda. Lakini swala la kupanda madaraja au kufukuzwa kazi siyo mojawapo ya majukumu ya CAG iwapo vitendo hivyo havihusihiwa mataumizi mabaya ya pesa na mali za umma.