Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Ripoti ya CAG imefichua madudu mengi ya awamu ya tano, kulikuwa na ufisadi wa kutisha

Na hapa bado ripoti ya July 2020 mpaka March 2021 itakuwa mbaya sana... Mtulie wananchi wafurahie matunda ya Demokrasia ambayo waliyakosa muda mrefu..
Wananchi hatusubiri ripoti tunasubiri miradi ya maendeleo na ya jamii iliyopo ikamilike kws spidi ya Magufuli na zaidi na.mipya tuione hatisibiri ripoti za makaratasi sisi

Ripoti za Magufuli hazikuwa kwenye makaratasi tulikuwa tukiziona Live kwa macho barabsta4,miradi ya umeme kila kijiji,zahanati nk hatuna muda mchafu wa kud
kusubiri ripoti za vikaratasi vya CAG

Ripoti za Magufuli hazikuwa makaratasi zilikuwa moja tu mwenye macho hasmbiwi tazama oneni wenyewe kilichofanyika.Hatutaki ripoti za press conference tunataka vinavyoobekana na wanyonge vya kusaidia wanyonge

Ripoti someaneni huko huko kwenu mkimaliza leteni maendeleo
 
Umeguswa ukweli..
CAG anasema ndege zitakamatwa..[emoji16]
Hili jambo niliwhikulisema hapa. Watanzani wengi ni wale anaotaka papo kwa papo; huwezi kuwekeza mamilioni kwenye mradi, halafu ,waka huo huo ukategemea faida. bezos alichukua takriba miaka kumi na tano kuanza kupata faida hadi kuwa tajiri namba moja duniani....
 
Siku ya leo sijui tuuiteje huko; Mbaya? Au nzuri sana?

Ripoti ya mkaguzi mkuu wa serikali inayoendelea kusomwa muda huu si kwamba tu inawaweka CCM na watetezi wa mwendazake kwenye wakati mgumu sana, lakini tayari imechefua wananchi wengi kwa kiwango kisichomithilika...
Kama ni kweli,basi wote waliokuwemo ndani ya hiyo serikali kuanzia mama ,PM,VP na mawaziri wajiuzuru ili uchaguzi mpya ufanyike.Wasitufanye wajinga
 
Kuna mambo mengi sana yanafikirisha kwenye hili sakata jipya la ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu kuibua madudu mengi ambayo serikali iliyokuwa chini ya hayati JPM yamejitokeza.

Upigaji umetokea kwa kiasi kikubwa sana na ni dhahiri kuwa tulikuwa tunaibiwa kimya kimya. Siku zote wizi wa kimya kimya ni mbaya sana kuliko ule wa hadharani. Tulikuwa tunakaririshwa mara nyingi kuwa mianya ya wizi wa mali za umma imezibwa kwa hiyo hali ni shwari.

Kwangu mimi namchukulia Hayati Magufuli kuwa alikuwa kiongozi mzalendo na na mwenye dhamira kubwa sana na maendeleo ya taifa letu la Tanzania [emoji1241] Ukiachana na upigaji ulioainishwa na Mkaguzi kwenye ripoti yake, swali la kujiuliza ni kwamba mbona mambo yalikuwa yanaenda? SGR ilikuwa inaendelea, Stand ya Mbezi Luis imekamilika, Kijazi Flyover imekamilika, Vituo vya afya tele, Mradi wa umeme ulikuwa unaenda vizuri. Je, tunataka kuaminishwa kuwa Hayati Magufuli hakuwa mzalendo na mali za umma?

My take, itachukua muda mrefu sana kupata kiongozi mwenye spirit kubwa kama JPM, huu ni mwanzo tu... Yaani hata mwezi haujaisha ila ashaanza kusakamwa. Hapo ndo naamini kuwa Magufuli alipigana vita nyingi sana wakati wa uongozi wake.

Raha ya milele umpe Ee Bwana; Na mwanga wa milele umwangazie, apumzike kwa amani; AMEN.
 
Kama ni kweli,basi wote waliokuwemo ndani ya hiyo serikali kuanzia mama ,PM,VP na mawaziri wajiuzuru ili uchaguzi mpya ufanyike.Wasitufanye wajinga
Yajayo yanafurahisha
 
CAG amesema stendi ya mabasi ya Magufuli iliyopo Kibamba manispaa ya Ubungo haikuwemo katika usanifu wa ujenzi wa barabara ya njia 8 kutoka Ubungo hadi Kibaha.

Kwa maana hiyo stendi ya Magufuli itaongeza msongamano wa magari tofauti na lengo la mradi huo wa barabara la kuondoa kabisa foleni kati ya Ubungo na Kibaha.

JamiiForums-707237655.jpg
 
Hii ripoti ya CAG imetuonyesha,kutufundisha na kutuonya kuwa tunahitaji taasisi imara na siyo mtu mmoja mwizi na fisadi anaejidai na kujinadi imara.

Kwa ushahidi wa ripoti hii ya CAG Magufuli alikuwa ni kiongozi populist ambae alikuwa ni mwizi,fisadi na mzembe wa mali za uma aliekuwa anajificha kwenye chaka la siasa za propaganda.
617950972148.jpg
20210092523.jpg
 
Hela nyingi za utekelezaji wa miradi ya mwendazake ilikua haipati baraka za bunge.

Hivyo hatujui ni sh ngapi zilikua zinaenda.

Ni kweli nchi hii ni tajiri kama alivyokua anaimba.

Lakini ndio hivyo katupiga sana.

Maana hata ndege amenunua kwa keshi, je ni nani anajua bei zake?

Na kuna kipindi cag alikua hakagui hilo shirika.

Na tulikua tunaambiwa linatoa gawio.

Mkuu hebu ngoja kwanza.

Hivi si unakumbuka tuliokotaga vichwa vya treni?
 
Kuna mambo mengi sana yanafikirisha kwenye hili sakata jipya la ripoti ya Mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kuhusu kuibua madudu mengi ambayo serikali iliyokuwa chini ya hayati JPM yamejitokeza....
Mkuu ni vipaumbele tuu , kipind cha JK mtu alikuwa anachota 200billion , mtu mmoja , lakn vitu vilienda , JPM alibug kwenye vipaumbele thus why watu wengi wanaona ni Bora Tu amekufa ...jamaa pesa Kwa wananchi ilikuwa ni hamna , walionufaika walikuwa wakuu wake wa vitengo.

Mimi jamaa yangu yupo Tanroad ana kampuni yake ya ujenzi anapiga pesa mbaya , miradi ni mingi Sana , shida inakuja Kwa wananchi jamaa alikuwa hovyo kubalance na hii ilitengeneza chuki kubwa mno, kundi la wafanyakazi hakuna anayempenda , wastaaf ndo usiseme kachota pesa zao wengine mpak wamekufa hawajalamba kitu.

vijana wasomi Wana chuki kubwa mno na jamaa, wafanya biashara ndo usiseme , CCM wenzake hawakumpenda , alikomaa na na miradi Tu hayo ambayo wote tuliopo sa hv duniani tutayaacha ... Lakni njaa ni ya Kila sku , mi mwenyewe nilikuwa fan wake by 2015 Ila jamaa nilimchukia mno Kwa misimamo yake ya kutojali maslah ya watu.

imagine tetemeko limetokea Kagera kiongozi unaropoka et sijaleta tetemeko kisa hela unataka zikajenge mabarabara .... Alaf unawaziba watu midomo , atakayelalamika unatishia kumfuta kazi , watu wanakuwa wanatembea wamejikunyata , unafanya upendavyo.

Kimsingi ukiwaza Sana kumfikiria mwishowe unajisemea Tu Bora amekufa , maana usingepata lolote la unafuu Kwa misimamo yake ya hovyooo
 
Huku kwetu kiwalani ,yombo barabara za lami hadi mlangoni..hapa tumeumia
 
Magufuli ameongeza deni la zaidi ya Trillion 18 katika kipindi cha miaka mitano ya utawala wake. Amekopoa nje kwa mabeberu, mifuko ya pensheni, benki za kibiashara n.k
 
Niliwahi kusema humu kuwa hadi awamu hii imalize muda wake inaweza kuvunja record ya ufisadi wote uliowahi kutokea Tanzania na imekuwa hivyo; Ogopa sana serikali isiyopenda uhuru wa habari, isiyopenda upinzani na uongozi wa mtu mmoja (one man show) tena anaependa kujitukuza na kutukuzwa kuliko hata Mola aliyemuumba.
 
Kwa ushahidi wa ripoti hii ya CAG Magufuli alikuwa ni kiongozi populist ambae alikuwa ni mwizi,fisadi na mzembe wa mali za uma aliekuwa anajificha kwenye chaka la siasa za propaganda.
 
Kama alivyowahi pendekeza awali,pr Assad alikuwa sahihi sana maana ni mmbobezi na amezunguka nchi nyingi kaona na ni msomi.Tatizo binadamu tunatanguliza chuki binafsi.Wa kale walisema hata adui yako akikushauri jambo msikilize na ulifanyie utafiti huenda likawa ukweli,Kuweka taasisi yenye sheria na taratibu ni muhimu kuliko matamko.
 
mods muwe mnafuta nyuzi zisizo na kichwa wala miguu au ziwekwe kwene jukwaa la jokes..
 
Back
Top Bottom