Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Ripoti ya Richmond Bungeni (FULL TEXT) na yatokanayo

Bwana Maane hicho kiboko ulichotaka kukielezea kinaitwa hamsa ishirini. Tuendeleee na mada.
 
Date::11/16/2009Rostam: Nataka uchunguzi mpya, si lazima wawe majaji

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

MBUNGE wa Igunga, Rostam Aziz amemwambia Spika Samuel Sitta kuwa bado kuna umuhimu wa kuchunguza upya kashfa ya Richmond na kwamba namna au njia ya uchunguzi huo ni jambo jingine.


Rostam, ambaye alitakiwa na kamati teule ya Bunge kujitokeza ili aeleze sababu za Richmond kutumia anuani ya kampuni yake ya Caspian na sababu za kuitafutia kampuni ya ushauri wa mambo ya habari, pia amemwambia Sitta kuwa kama mtu anaweza kuhukumiwa kwa tuhuma, basi hata mbunge huyo wa Urambo Mashariki asingeweza kuwa hapo alipo.


Rostam aliipigia simu Mwananchi mwishoni mwa wiki kutaka kutoa ufafanuzi wa maelezo ya Sitta ya kupinga ushauri wake kuwa liundwe jopo la majaji watatu kuchunguza suala hilo kwa kuwa ana uhakika kuwa kamati teule ya Bunge, ambayo iliongozwa na mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe ilitoa ripoti ya uongo na haikumtendea haki.


Sitta alipinga pendekezo hilo la Rostam akisema kuwa maamuzi ya Bunge hayawezi kuchunguzwa upya na mhimili mwingine wa nchi na akamshangaa Rostam kwa kutaka kujitetea sasa wakati alipewa nafasi hiyo lakini hakuitumia.


Lakini Rostam alisema kama njia ya kutumia majaji ni ngumu, basi hata kuwe na usikilizwaji wa umma pamoja lakini akasisitiza: "Ninachotaka ni haki itendeke... suala la njia ipi itatumika ni jingine kama ya majaji ni ngumu."


Mbunge huyo wa Igunga ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (Nec) ya CCM alizidi kujitetea kuwa hajawahi kupewa haki ya kujitetea bungeni kwani alipotaka kufanya hivyo, Spika alimzuia.


Rostam alisema uamuzi wa kutaka uchunguzi mpya unatokana na ukweli kwamba, kuna nyaraka nyingi za msingi ambazo hazikutumiwa na kamati hiyo teule ya Bunge iliyoundwa kuchunguza utoaji wa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura kwa Kampuni ya Richmond Development LLC mwaka 2006.


Alifafanua kwamba mbali ya kutotumika nyaraka nyingi za msingi, kamati hiyo pia haikutoa haki na muda wa kutosha kwa baadhi ya watu kujieleza (akiwemo yeye) na kuhoji kama watu wanaweza kuhukumiwa bila kujitetea nani atasalimika.

Rostam alitakiwa kwenda kujitetea mbele ya kamati hiyo Desemba 24 mwaka 2007, lakini hakutokea na alijieleza baadaye kuwa kamati ilimwita wakati ikijua kwamba siku hiyo ilikuwa ni siku kuu na hivyo asingeweza kutokea. Hata hivyo, Mwakyembe alisema watu wengine walioitwa siku hiyo, akiwemo mkurugenzi wa Takukuru, Dk Edward Hoseah walitokea na kuhojiwa.


Akijenga hoja zake kuhusu hukumu ya mtuhumiwa, Rostam alisema hata Spika Sitta aliwahi kukumbana na kashfa mwaka 2001 katika wilaya yake ya Urambo, lakini kamati ya CCM ya mkoa ilikataa kumwajibisha.

"Kama watu wangekuwa wanahukumiwa kwa tuhuma basi Sitta leo hii angekuwa siyo Spika wala mwanachama wa CCM," alidai Rostam.


"Zilikuja tuhuma tena za..., lakini mimi nikauliza kama alipewa haki ya kujitetea, tukaambiwa bado, basi nikasema uamuzi huo ungekuwa batili hivyo isingefaa kumhukumu."

Kuhusu tuhuma za kuhusika kwa kampuni yake ya Caspian, Rostam alisema suala la mawasiliano na Dowans alikwishaweka bayana kwamba linatokana na shughuli za kibiashara na akasema tuhuma kwamba aliwahi kuratibu mawasiliano na Richmond ni uongo na upotoshaji umma.


"Mbona Caspian ilijenga Mwananchi (jengo la Mwananchi Communications linalochapisha gazeti hili), hapa tatizo la mawasiliano linatoka wapi? Lakini pia sijawahi kuwa na mawasiliano na Richmond hata siku moja wala kampuni yangu," alijitetea.


"Kama barua pepe ni ushahidi wa kuhusika na kampuni, je tusemeje kuhusu yeye (Sitta) aliyekuwa na mawasiliano na hata kupendekeza kudhamini utambulisho wa Richmond?"

Spika Sitta alikiri kuileta Richmond kama mwekezaji wakati akiwa mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), lakini baada ya kubainika kuwa kampuni hiyo haina uwezo, ilinyimwa mradi wa bomba la mafuta kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza mwaka 2004.


Rostam alihoji kwanini Spika hakuwahi kulieleza bunge hata siku moja kuitambua Richmond iwe kwa uzuri au ubaya kwani ndiye aliyewahi kuileta.


"Kwa kuongoza bunge lililoambiwa Richmond ilikuwa kampuni hewa na ya kitapeli ya akina Rostam wakati yeye akijua kuwa hayo hayakuwa ya kweli kwa maana, ni mtu aliye karibu nao (wamiliki wa Richmond) na kutosema kuwa hayo si kweli, hakuwatendea haki wananchi," alisema mfanyabiashara huyo. "Hakutendea haki wananchi, Bunge na wamiliki wa Richmond ambayo aliwahi kuileta akiwa TIC na kudiriki kuwaombea udhamini."
 
Mbona RA ameanza kuhaha namna hii kwa siku za hivi karibuni kuna nini kinachoendelea ambacho labda wengi wetu hatukijui? Namwona kama mfa maji ambaye haishi kutapatapa!!!

Tiba
 
Hivi watanzania millioni 40 tunababaishwa na huyu muntu? kama anaona hakutendewa haki si aende mahakamani akilishtaki bunge au serikali kwa aidha kumuhukumu au kumtuhumu kwa kitu kisicho cha kweli?
yaani anafanya watanzania wote na wawakilishi wao wote ni tumbafu?
kweli ndio maana Nyerere alikuwa anaonyesha kweli yeye ni kiongozi wa nchi hata kama ni Udikteta, lakini inafika mahali nchi lazima ijionyeshe yenyewe ni kubwa kuliko kidubwana kimoja, ambacho kinajifanya chenyewe ni nchi na wengine ni mandondocha wake.
huyu ni bakoro kumi na mbili na kama afya yake si nzuri angala sita na siku amnatoka keko/ukonga nk bakora zingine sita akamuhadithie mkewe, kama atakuwa na uwezo huo.
Na hili ndio liwe funzo kwa viongozi waafrika wengi wao wanaishi katika maisha ya kuwa black mail na majambawazi kama huyu? waache kupokea mulungula ambao badae ina wa-kost, iwe milioni, billioni , inaishia kuto zaidi.
 
RA ni tumbaf tu anatuona watanzania wote mabwege. Asubiri siku zake zikifika atajua mchicha si mlenda.
Wakina Mramba waliotuchezea akili wakituambia tule majani si walinyea ndoo kule keko?
 
CCM kupitia NEC ikifanya hivyo itakuwa imetenda kosa la UHAINI na inastahili adhabu kali toka kwa wananchi.
Kwa nini isiwe adhabu toka kwa msajili wa vyama? yule mwanasheria Tendwa?
Mi nadhani ni wakati muafaka wa wananchi kuipeleka sisi m mahakamani ikijaribu kuvunja sheria!
Hili wanasheria mwasemaje ati?
 
CCM ndo chama tawala hakiguswi na sheria zinazowagusa wengine...sheria zao,tokea mfumo wa chama kimoja,serikali yao,mahakama zao,hao mnaotaka wawachukulie hatua wanawachagua wao,ni kama kesi ya nyani vile kumpa ngedere halafu ukitegemea haki...wapi na wapi bana!!!!
 
"Mbona Caspian ilijenga Mwananchi (jengo la Mwananchi Communications linalochapisha gazeti hili), hapa tatizo la mawasiliano linatoka wapi? (Du the so called kingmaker anaweza kuwa na argument za kipumbavu namna hii?? Mbona hajiulizi kwa nini hakuhusishwa na mkataba wa Buzwagi ilhali Caspian ilikuwa na tenda ya kufanya civil works kubwa kubwa pale?????

"Kama barua pepe ni ushahidi wa kuhusika na kampuni, je tusemeje kuhusu yeye (Sitta) aliyekuwa na mawasiliano na hata kupendekeza kudhamini utambulisho wa Richmond?" (Du kwa hiyo kumbe source ya hii hoja ni wewe Rostam aiming at neutralizing ishu yako????? But it is so weak and so low....... try another one)


Rostam alihoji kwanini Spika hakuwahi kulieleza bunge hata siku moja kuitambua Richmond iwe kwa uzuri au ubaya kwani ndiye aliyewahi kuileta. And therefore wewe huna makosa hata baada ya ujambazi huu maana Kampuni ililetwa na Sita.......only in Tz.


"Kwa kuongoza bunge lililoambiwa Richmond ilikuwa kampuni hewa na ya kitapeli ya akina Rostam wakati yeye akijua kuwa hayo hayakuwa ya kweli kwa maana, ni mtu aliye karibu nao (wamiliki wa Richmond) - Hivi kuwajibika katika nafasi yako kikazi tayari unakuwa karibu na watu wanaohitaji huduma ofisini kwako????? na kutosema kuwa hayo si kweli, hakuwatendea haki wananchi," (Toka lini Rostam ukawa na huruma na watanzania??????)

Maswali ya kujiuliza:

1. Rostam alikuwa wapi kulalamika muda wote huu almost more than 1yr n half down the line?

2. Rostam is such a big man, kingmaker, JK's best friend etc. etc. anaogopa nini mpaka anaonekana kuweweseka kila kukicha?

3. Rostam anafahamu nini kuhusu utekelezaji wa mapendekezo ya bunge ktk sakata la Richmond? Inawezekana vibaraka wake wamempa hint kwamba he is gonna be hit.

4. Rostam anajitetea binafsi au pamoja na akina EL?

5. Je Rostam anaamini kwamba Richmond ni kampuni hewa na ya kitapeli?? Self conviction. Na je ni kwa nini waandishi hawamuulizi hili?

6. Rostam kwa nini anasaka sympathy from the court of public opinion?

7. Toaka lini Rostam amekuwa na huruma na wananchi, je katika hoja zote za ufisadi amewahi kuchangia bungei in reflexion ya kuwaonea huruma wananchi???????



All in all mi naona tunahangaika bure na huyu jambazi...... Root cause ya kutokwisha kwa hili jambo ni JK and he is the problem of not winding up on this, yes I said it!!!!
 
Dawa yao imeshatimia,......ki kutowachagua Mafisadi wote...na wala kutorudisha majina yao.....hivi jeshi na vyombo vya usalama vinafanya nini??wanaangalia tu ujinga wa wanasiasa???wanafanya wanavyotaka??inasikitisha sana.....hawajui wajibu wao kama vyombo vya dola...na usalama pia....corrupt....

Hiyo ndiyo Tanzania, vyombo vya usalama navyo vimeingiliwa na Mafisadi, sijui utaenda kwa nani. Wananchi wakichoka waatamua kuchukuwa sheria mikononi mwao kabla nao hawajaingiliwa na Mafisadi.
 
Sasa hizo nyaraka muhimu ambazo hazikutumiwa na kamati si aziweke hadharani?Au mpaka uchunguzi mwingine?Duh,hawa watu muda mwingine naishia kujiuliza kuwa hivi hivyo vichwa vyao ni kwa ajili ya kuota nywele tu!?
Anayetaka uchunguzi,scotland yard is the right option.Period.
"The lady doth protest too much,methinks".W.Shakespear used to say.
 
China watuazime kale kasheria kao au itakuwa ni kuvunja haki za binadamu?
 
Haka kawimbo ni katamu sana kanaonekana "Richmond" Kila kukicha kamo! ila mie nimekachoka kabisa

Richmond kwenye NEC?...hakuna cha kushangaza, nchi imemshinda bro JK aliowaweka na waliomuweka yeye madarakani wote ni kizazi cha nyoka.. "Nyoka-----Eva----Adam----KIFO"
 
CCM kupitia NEC ikifanya hivyo itakuwa imetenda kosa la UHAINI na inastahili adhabu kali toka kwa wananchi.
mbona imefanya makosa mengi ya uhaini na hamna adhabu yeyote kutoka kwa wananchiii...!!!!

Kwani Richmond ni nini mpaka itingishe chama dola???Bado chama wanauwezo wa kujadili na kufunga mjadala huuu kwa masilahi yaoo..
 
Back
Top Bottom