Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mwaka wa Fedha 2019/2020

Ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mwaka wa Fedha 2019/2020

CAG HONGERA SANAAA TENA SANAA
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana na ripoti za idara hii muhimu serikalini ya CAG.

Kwa kweli ukipata watu wanaofanya kazi zao kwa weledi na wenye hofu ya Mungu utajifunza mengi sana hususani kwenye hizi nchi za dunia ya tatu.

Nafikiri kwa uwazi huu huu, ndio uliomfanya CAG kabla ya huyu tuliyenaye sasa kupokonywa tonge mdomoni, hayo mambo ya ukweli na uwazi bwana!

Ukweli ni kwamba, ili nchi iende mbele tunahitaji mambo haya sana, lakini najaribu kuwaza kwa akili zangu ndogo tu na kubaki na maswali yafuatayo: Hawa CAG team, wanafanyaje kazi yao? Je?
  1. Wanakagua mahesabu ya serikali baada tu ya shughuli zote za serikali kukamilika au wanahusishwa pia kwenye michakato ya manunuzi ya serikali?
  2. Kama ndivyo, je mapendekezo yao huwa yana nguvu gani kabla ya hasara kama hizi kujitokeza?
  3. Na kama wana fursa ya kupendekeza jambo lolote kabla ya hatari, mapendekezo yao husikilizwa na nani haswa?
  4. Je, Mtawanyiko wao katika idara za serikali ukoje, au wapo wapo tu kama idara ya nyeti ya TISS, kwamba hawafahamiki sana miongoni mwetu wananchi wa kawaida?
  5. Kama wapo hadi ngazi za chini kwa maana ya kijiji au kitongoji, nini jitihada zao katika kupambana na kuzuia matumizi mabaya ya fedha za serikali kabla ya hatari?
  6. Kama ni wachache, kwanini serikali isiwekeze nguvu zaidi katika idara hii muhimu sana kwa ustawi wa nchi zetu changa kwa kusomesha, kuwajengea uwezo na kuwaajili kila kona ya nchi hii ili tuokoe pesa nyingi badala ya kusubiri kuja kufichua uovu wakati pesa ilishateketea?

Naamini pesa za kuwaajili hawa watu kila kona zitakuwa ndogo tu kulinganisha na upotevu wa mabilioni ya pesa yanayopotea kila mwaka.

Na hapa ndio sehemu pekee na nzuri ya ajira kwa vijana, tena ya kizalendo kabisa kuliko kila mwaka tunalia hatuna uwezo wa kuajili wakati mabilioni yanapigwa na wajanja na wanaendelea kupeta tu mtaani. Inauma sana ndugu zangu
  1. Inaonekana chombo hiki kinakagua vizuri sana serikali pamoja na idara zake. Wao kama zilivyo taasisi nyingine za serikali tunaamini pia wanatumia pesa za serikali kuendesha shughuli zao.

Je, wanakaguliwa na nani ili nasisi wananchi wa kawaida tujiridhishe na usafi wao ili tusije hisi kuwa ni kakitengo fulani tu kanakofanya kazi kwa ajili ya maslahi ya kundi fulani tu la watu wachache kwa maslahi binafsi ama kufurahisha uongozi ulioshika hatamu
  1. Kama idara hii nyeti itakuwa nyuma ya wanasiasa ndugu zangu tumekwisha kabisa, ni vyema nao tujue wazi wanatumiaje raslimali zetu kwa uwazi kabisa na wawe kwanza kutueleza bajeti yao na matumizi yao kabla hata hawajaanza kueleza madudu ya idara za serikali, lakini pia wawepo wengine nyuma yao kuhakiki hicho wanachokisema kama ni kweli au la.

Najua inaweza kuwa ngumu lakini hakuna kinachoshindikana chini ya jua.

Kwa maana hakuna malaika hapa duniani na kamwe hatotokea, hivyo tunaweza jikuta tunayumbishwa sana kama taifa na vyombo vyetu hivi ili tukose pa kusimamia kwa sababu tu ya mifumo yetu mibovu iliyojikita zaidi kuibua changamoto kuliko kuzizuia ama kuzikabili.

Kwa wakubwa wenzangu mtakumbuka kuwa hata kwa marehemu Mkapa tulisikitika sana, kwa Mzee Kikwete tulisikitika pia, Hayati Magufuli vivyo hivyo pengine zaidi, naamini pia na mama yetu Samia hatotoka salama katika hili, kwa kuwataja wachache

Wazo langu, kitengo hiki kiwe kama TAKUKURU, yaani wajikite zaidi katika Kuzuia na Kupambana na matumizi mabaya ya fedha za serikali katika idara zote ili kuokoa pesa zinazopotea kila mwaka, kuliko mtindo wanaoenda nao sasa.

Angalizo, tukiwaajili kila ngazi na wakafahamika huenda nao wakaingia kwenye mkumbo wa rushwa tukashindwa kupata clear data, sema labda waundiwe sheria ngumu zaidi ili nao wakibainika kukiuka maadili ya kazi yao ikiwemo basi wapewe adhabu kali zaidi kuliko mtu mwingine yeyote yule ikiwemo hata kunyongwa kabisa endapo itathibitika hivyo. Vinginevyo hizi hadithi hazitakuwa na mwisho kabisa, na itakuwa mtaji wa kisiasa tu kila uchwao

Naamini wanachofanya wao kwa sasa, Ufujaji ufanyike kwanza ndio wao wapite kukagua, hapa kila mwaka wataibua tu maovu mengi tena sana. Niko radhi kwa ufahamu wangu mdogo nikosolewe katika hili.

Kingine ni kuwa, hata viongozi wetu tulionao kwa nyakati zote pengine wametokana na veting mbovu ama kubebana au kujuana, sasa tusitegemee wakawa na weledi katika matumizi sahihi ya pesa hata siku moja.

Kubwa kuliko yote, wana siasa wetu hawana rangi maalum wanabadilika kulingina na mazingira na matakwa ya viongozi walio juu, hili nalo ni hatari sana na sumu kwa taifa letu lina linalohitaji utashi wa ndani ili tutoke hapa tulipo.

Suluhu ya muda mrefu ninayoiona, ni kukamilisha mchakato wa katiba yetu mpya ili tupate viongozi stahiki tena kwa kuzingatia taaluma zao kwa ngazi zote kuanzia mawaziri na mpaka huku chini na si vinginevyo.

Bila hivyo, sitapiga tena kura kama nilivyofanya mwaka jana, endeleeni tu kunichagulia muwapendao nyie, mie bado naona mazingira hayako sawa kwa sasa ila naamini ipo tutavuka tu upepo huu, kama tulivyowatoa wakoloni, hivyo hata ukoloni wa kifikra utatoweka tu.

Poleni sana kwa kuwachosha na uandishi wangu mbovu, mimi ni msomaji tu, ni mvivu sana wa kuandika. Ahsanteni!
 
Swali ni jee ANGEKUWEPO ANGEONGEA ? Au ripoti ingekuwa nyingine kabisa ya kusifu na kubudu?

Mimi naulaumu katiba yetu ambayo inaruhusu MTU mmoja kuwa kama MUNGU wa TZ, kama ataamua kuitumia kwa matakwa yake binafsi. Tutasiseme bora ameondoka ila akitokea mwingine bado ananafasi ya kurudisha pale pale kama katiba ndo hii hii.
 
Sijasoma yote. Ila hii huwa ni road map ya matumizi yajayo.
 
Sahihi kabisa.
Swali ni jee ANGEKUWEPO ANGEONGEA ? Au ripoti ingekuwa nyingine kabisa ya kusifu na kubudu?

Mimi naulaumu katiba yetu ambayo inaruhusu MTU mmoja kuwa kama MUNGU wa TZ, kama ataamua kuitumia kwa matakwa yake binafsi. Tutasiseme bora ameondoka ila akitokea mwingine bado ananafasi ya kurudisha pale pale kama katiba ndo hii hii.
 
Ntajaribu kujibu kdogo
1.wanakagua baada ya matumizi ya mwaka fulani

2.mapendekezo yana nguvu mana ukicheza huna kazi

3.
4.
5.
6.

CAG pia anakaguliwa na kampuni binafsi inayochaguliwa na PAC

mengine sijui wahusika watasema
 
Swali ni jee ANGEKUWEPO ANGEONGEA ? Au ripoti ingekuwa nyingine kabisa ya kusifu na kubudu?

Mimi naulaumu katiba yetu ambayo inaruhusu MTU mmoja kuwa kama MUNGU wa TZ, kama ataamua kuitumia kwa matakwa yake binafsi. Tutasiseme bora ameondoka ila akitokea mwingine bado ananafasi ya kurudisha pale pale kama katiba ndo hii hii.
MKUMBUKE KITU KIMOJA. HUYU CAG ALITEULIWA NA MAGUFULI , ALIKUWA TRA AKAMTOA AKAMPELEKA KUWA RAS NJOMBE [ Yote hiyo kumlainisha na kumuonyesha power yake] HALAFU AKAMRUDISHA KUWA CAG!!! NINA UHAKIKA KABISA KUWA HAYA YOTE MADUDU ANAYOONESHA KACHELE ASINGEYAONESHA IWAPO MWENDAZAKE ANGEKUWA HAI!!! ALIKUWA SIO MVUMILIVU WA KUAMBIWA UKWELI Hivyo Kachele kulinda ugali wake [ hasa kuhusu ATCL] angeyefukia!!

Kuna watu wanatakiwa kujibu maswali kutokana na ripoti hii ya CAG. Mmoja wapo anayetakiwa kujibu ni huyo Waziri wa USAFIRISHAJI; walitumia utaratibu upi kujinunulia hizo ndege, hiyo bodi ya ATCL aliunda vipi na kujaza watu wasio na weledi kama ripoti inavyosema?

Kutokana na uozo alioibua CAG, sasa naanza kuona sababu iliyowafanya watu wa kundi fulani kumpigia debe huyo Chamliho kuwa angependekezwa kuwa makamu wa Rais!!
 
CAG HONGERA SANAAA TENA SANAA
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana na ripoti za idara hii muhimu serikalini ya CAG.

Kwa kweli ukipata watu wanaofanya kazi zao kwa weledi na wenye hofu ya Mungu utajifunza mengi sana hususani kwenye hizi nchi za dunia ya tatu...
This time CAG report imekaa mkao naona, shida ni kwamba yeye anaweza kutoa mapendekezo tu hana mamlaka mengine, kwenye kutekelezwa sasa inategemea anayepewa mapendekezo ni nani
 
Tuliaminishwa kuwa awamu ya JK ilikuwa ya wapiga dili, mafisadi, wezi, wala rushwa na wabadhilifu kuliko awamu ya tano, kumbe haikuwa hivyo. Upigaji upo kwa kiwango kile kile au pengine kupita kwa awamu zote tu.

Tuliaminishwa na kufoka na tumbua tumbua za hadharani kumbe looh!! ni zalongwa mbali zatendwa mbali. Tulibadilisha kupata wezi wapya tu.

Nini kifanyike kuzuia wizi na ubadhilifu serikalini?
 
CLOUDS wanajaribu kuuhadaa umma kwa kutumia vyombo vyao, wanajaribu kuchallenge na kuibeza ripoti ya CAG.

eti wadai wao walitoa invoice kwa mamlaka husika!!

huu ni ujanja na utapeli mkubwa.

Tunaomba TAKUKURU watimize wajibu wao maana hapa kuna fedha za wananchi zimechotwa bila kufuata utaratibu,

sheria ifuate mkondo wake.
 
Nasikiliza Clouds Fm, hawazungumzii chochote kuhusu report ya CAG, inawezekana sindano imewaingia na Sasa wanatafakari, majibu kwa Takukuru, wapi zilipo receipt za sh 600 million.
 
... majizi tu yale kwa mwamvuli wa uzalendo feki ili kujimegea keki ya taifa na wameimega kweli.
 
Habari wanaJF,Ni kwanini mthibiti mkuu wa hesabu za serikali hatoi ripoti ya punguzo la mishahara kuanzia 2015-2021? Nimeona Anazungumzia mpaka foleni za morogoro road.
 
Wewe Sasa utaulizia Hadi mishahara waliyokatwa watia nia

Labda wanaVichwa vya WENDAWAZIMU wenzangu tumsikilize mtaalamu.

Kwako mwalimu kashasha
 
Tabora peke yake HATI Chafu 4. Nadhani viongozi Wakuu wa mkoa wachukuliwe mkoa.
 
Back
Top Bottom