Road trip update: Dar - Mtwara - Dar | Hali ya Barabara inatisha | Ila nimetumia mafuta ya Tsh 150,000/= tu!

Kaka, ya 2014 Hybrid. Ni cc 1,500 7 gear DCT.

Tatizo waliviuza Japan tu kwahiyo Lugha nimeangaika nimeshindwa. Nimeshazoea sahivi.

Kusema kweli Mtwara nimejaribu kuzunguka ila moyo haujapaelewa. Nilipita kule kuna soko kubwaaaaaaa la ghorofa hafu watu wanauzia vitu chini. Nikapita sehemu ni kama ghost town sioni mtu wala gari. Nikaja ushuani huku jirani na bahari. Nikasogea njia ya port. Nikashuka na barabara ya Bodi ya Korosho.
Nikarudi roundabout ya samaki, Nikarudi tena juu kuzurura zurura nikaenda beach pale dah.

Moyo haujakupenda sijui. nikaamsha.
 
Uzi mzuri sana. Asante!
 
Dah sema mikoa ya Kusini imepoa sana
Kule Mtwara kote mpaka Lindi mpaka Rufini kulitakiwa kujengeke sana pale kuna miradi mingi ya gas ilitakiwa kupaendeleza.

Zasa hivi huko Iran kuna vita mfereji umefungwa ilitakiwa tuwe tunauza gas nje kwa mabilioni ya dola tunajenga nchi.

Ila tatizo kinachowezekana pengine duniani, Tanzania hakiwezekani.
 
Nafikiria kudrive kushuka huko maana kuna jamaa kaniambia diversion zote za madaraja na makaravati zimekamilika na road ni nzuri sasa nashangaa we unasema kuna mahandaki, sielewi
 
Hapo umezunguka Mtwara mjini sasa. Barabara uliyopita na kukuta soko la ghorofa ndiyo Chuno road hiyo na hilo soko linaitwa Chuno pia. Mji upo kimya sana, vurugu utazikuta eneo la Bima ulipojaza mafuta labda na upande wa nyuma kule wa pale Puma. Hilo ghorofa pichani ndiyo moja ya landmarks za Mkoa, jirani hapo kuna kanisa jeupe. Ungekuwa unatokea Puma kuja uelekeo wake usingesita kulipiga picha, mkoloni alituliza akili sana eneo hilo.
 
Nafikiria kudrive kushuka huko maana kuna jamaa kaniambia diversion zote za madaraja na makaravati zimekamilika na road ni nzuri sasa nashangaa we unasema kuna mahandaki, sielewi
Barabara ya kusini si weather proof. Kwa kipindi hiki cha mvua haiwezi kukosa hitilafu.
 
Juzii juzii nilienda dar to mwanza kama taifa hatuna barabara kabisaa..

Iviiii wanasiasa na ndugu zao nao wanatumia barabara hizi hizii tunazo pita sisiii

Aisome mwigulu mchemba
 
Niliwahi pita Njombe-Songea-Masasi-Lindi then Dar, kipande chenye barabara nzuri ni Songea mpaka Tunduru tu, baada ya hapo ni Majanga matupu!

Kama Masasi kwenda Lindi ndo kuna Barabara mbovu sijapata ona, vipi madaraja ya Lindi Dar yashakamilika yote?
 
Nafikiria kudrive kushuka huko maana kuna jamaa kaniambia diversion zote za madaraja na makaravati zimekamilika na road ni nzuri sasa nashangaa we unasema kuna mahandaki, sielewi
Atakua anatumia Land Cruiser za Serikali. Niamini mimi, kama umepita Morogoro Rd, Dodoma Rd, au huku Bagamoyo Rd ukasema izo ni mbaya, basi huko Ni mara 3 yake. Mkuu barabara sio nzuri kabisa.
 
Mkuu nipo interested na consumption ya gari 31km/L ni gari aina gani? Ni hybrid?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…