Road trip update: Dar - Mtwara - Dar | Hali ya Barabara inatisha | Ila nimetumia mafuta ya Tsh 150,000/= tu!

Mimi ndio maana weekend ndefu yoyote lazima nitoke nje ya Dar kuoumzisha akili. Hapa nipo Moro nauli kwemda na kurudi familia 78,000/- tu
 
Huko ni pazuri ila nimegundua wewe sio msimulizi mzuri.

Mtu baada ya kusoma havutiwi kufanya Road trip kama wewe.
Duh kijana anajitahidi mkuu. Wengi wamefanya road trips kwa simulizi zake.
 
Wabunge wao wapige kelele aisee. Kuna siku tulikua humu tunaongelea safari ya kwenda Songea kupitia Mtwara aisee mara 100 upite Morogoro. Utasimbuliwa na jam ya maroli ila ukivuka Moro ushatoboa.
Hii njia Dar Mtwara nilipita mara ya mwisho 2013 ilikuwa nzuri sana na haina magari mengi wala askari. Inasikitisha ilivyo sasa hivi.
 
Hongera Mkuu.

Ila naomba ufafanuzi hapo kwenye kuzima Gari. Yaani Safari yote hukuzima Gari.

Au kitaalam unaposafiri Safari ndefu kama Dar Mbeya, halafu ukafika Iringa ukataka kula chakula, Je unaweza zima Gari? Au unatakiwa uiache inaunguruma? Then unazima Mwisho wa Safari?
 
Shukrani mkuu.

Hamna, gari unazima vizuri kabisa bila shida. Magari ya siku hizi ya kisasa (miaka ya 2000 kuja juu), ata ukisafiri km 300 non stop ukifika mahali we zima, sema hauna haja ya kusikilizia dk 10 sijui, unless ulikua unaendesha kwa fujo saaaana.

Mimi hapo inavoonesha ayo masaa inamaanisha gari ilikua ON. Ni mjumlisho tu. Kwamba labda day 1 ilikua ON masaa kadhaa. Day 2 ikaendeleza. Ivo ivo ni kama odometer inavojumlisha kilometa za jana na za leo na kesho.

Wengi tunachofanya ambacho sio kibaya ni: unavowasha unaliwasha kama sekunde 15 ndio unaanza kuondoka, na unavoondoka unaanza kuondoka slowslow later ndio unakanyaga speed kali, ni kizuri kwa kuacha gari lipate joto, ni precautions nzuri ingawa madhara yake kwa magari ya kisasa ni negligible.

Pia wakati wa kuzima ukifka (kama umesafiri muda mrefu unaanza kwa kupark, labda unashuka, unashusha mizigo, au unafunga geti, then ndio unazima, zinakua km dk 2 ivi, pia sio mbaya, tunasema oil inakua imeshuka imetulia, sio mbaya pia ila ata ukizima chap madhara n madogo.

Kwa mfano, hybrid ukiwa njiani kuna muda engine inajizima yenyewe au magari kama Mazda CX5 au BMW yana iStop /stopstart gari kwenye foleni inajizima yenyewe kusave mafuta kwahiyo ata kama umesafiri km 1000
Yenyewe inazima.
 
Nimekupata Mkuu.

Unajua kuna Siku nipo safarini sasa nikawa nakula mahali halafu gari nimeiacha inaunguruma sasa nikawa nawaza hivi hapa mtu akiingia halafu akasepa na Gari tampata wapi?

Sasa nimeelewa kumbe next time takuwa nazima ili ni relax napokuwa nimesimama mahali.
 
Muhimu ni kucheza na mshale wa RPM, ukisimama hutakiwi kuzima gari wakati RPM ipo juu ya 1000. Hivyo wastani wa dk 1 ni muhimu sana.
 
Yaani ukifika, ukaweka P, dakika 2 tu unazima. Haina wasiwasi.
 
Muhimu ni kucheza na mshale wa RPM, ukisimama hutakiwi kuzima gari wakati RPM ipo juu ya 1000. Hivyo wastani wa dk 1 ni muhimu sana.
Sure, unavojivuta vuta pale baada ya kuweka Parking hadi umalize unazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…