Roho inaniuma nimetimiza miaka 35 sina mtoto wala maisha

Mkuu wala usisononeke, kila mtu anakimbia mbio zake binafsi kwenye maisha! Mungu hawai wala kuchelewesha jambo kwa kiumbe wake....unaonaje ungekua tajiri ukiwa na miaka 25 halafu sasa hivi ungekua umefikisika huna hata mia? Unamfikiriaje yule mzazi aliezaa wale watoto 4 wote waliokufa uwanja wa Taifa mmoja akiwa na miaka 11, kwa maana sasa hana hata mmoja na yupo sawa na wawe, unaonaje ungepata mtoto ukiwa na miaka 20 na angekufa mwaka huu akiwa na miaka 15? MUNGU ndio mjuzi, nina miaka 40 mkuu na mtoto wangu wa kwanza ana miezi 3, ndivyo Mungu alivyonipangia na maisha yanaendelea! 35 years bado na endelea kuomba na hata ukikosa shukuru pengine Mungu ameona watoto watakua si kheri kwako!
 
 
Nadhani umemueleza jambo la msingi. He should keep fighting by working hard...the limit is the sky
 
Hilo la mtoto linawezekana, pambana
 
d Hiii dunia hii ina mafumbo mengi sana juu ya maisha yetu sisi Binadamu.

Bil ya kumtegemea Mungu kwa kumshirikisha kwa kila kitu, mafanikio ni ndoto za mchana kabisa.

Nimekumbuka 2019 July, yule Mchungaji M-Nigeria Msabato aliyekuwa akihubiri ktk makambi alipata pigo zito sana baada ya Familia yake ya watu 7(Mke+Watoto) kufariki dunia kwa moto uliowalipukia wakiwa nyumbani na kuunguza wote pa1 na nyumba yake yote kisha kusalia yeye pekee aliyekuwa ktk hayo makambi.

Mwaka huo huo 2019 December kijana mwingine tena Mtanzania alifiwa na Mkewe+watoto wawili kwa mlipuko wa gesi nyumbani kwake na kuteketeza familia yake yote akifuatiwa na Baba yake mzazi kufariki pia baada ya kupata mshtuko tokana na vifo vya familia ya mtoto wake/Me.

Mungu atusaidie kutuepusha na majaribu na kutushindia changamoto za kimaisha, Amina.
 
Wako soap soap 24/7, halafu utasikia nimesahau kadi ya benki nyumbani, nisaidie buku tu. Kumbe ndo anaenda kula.

Jinga kabisa.
 
Asiye na maisha ni aliyekufa
 
Mungu akubariki sana kwa shuhuda ulizotoa hapa Chifu.
 
Inavyoonekana wewe ni aina ya wale watu wanaopenda sana kuonewa huruma na kupewa pewa pole!

Huu ni ujinga uliopitiliza na usiposhituka utaishia hivi hivi

Aina ya watu Kama wewe wengi wao ni wale katika malezi yao kila kitu waliamuliwa na wazazi. Yaani hufanyi kitu hadi Mzazi wako akuruhusu hata katika vile vitu vidogi vidogo

Aina hii ya malezi ikikutana na mtu ambaye ubongo wake hauko sharp ataendelea kutegemea amri ya Mzazi hadi uzeeni kiasi kwamba hadi Mzazi anaanza kukushangaa

Fanya maamuzi acha kulia lia! Kila mtu anaishi maisha yake! Utapewa pole na kutiwa moyo lakini bila kuchukua hatua utaendelea kubaki hivyo hivyo na hizo pole hazitakusaidia chochote

Mwenye kufanya maamuzi ni wewe na wala hakuna wa kuamua kwa niaba yako. Kupewa pewa pole sio sifa nzuri.

Na inavyoonyesha unafanya vitu huku mbele ukiwa umetanguliza uoga na mindset ya kusubiri ushindwe ueleze watu wakuonee huruma wakupe pole

Pambana watu wakupe hongera wanapoona mafanikio, na katikati ya mapambano kuna milima na mabonde watu wakupe pole baada ya kuona juhudi zako zilipofikia

Ni hayo tu!
 

Wewe ndo tunawaza sawa...sipendi kbs mtu muoga oga mie arghhh! Ni muda wa kufanya action huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…