Roho Mbaya na Wivu wa Majirani: Kisa cha mtoto aliyetambaa hadi ndani ya gari Arusha kitufundishe umuhimu wa CCTV

Roho Mbaya na Wivu wa Majirani: Kisa cha mtoto aliyetambaa hadi ndani ya gari Arusha kitufundishe umuhimu wa CCTV

Umuhimu wa CCTV Nyumbani Uswahilini (Kutokana na Tukio Hili)
Mazingira ya uswahilini yana sifa ya nyumba zilizoshonana, watoto wengi kucheza nje kwa pamoja, na mipaka ya viwanja inayochanganyika.

Tukio la Arusha linatufundisha umuhimu wa CCTV uswahilini katika maeneo yafuatayo:

1. Kuepusha Migogoro ya Kudhaniana na "Chuki za Majirani"Kuzuia Kusingiziwa:
Uswahilini ni rahisi jambo baya likitokea (kama mtoto kuumia au kupotea) majirani kuanza kunyooshea vidole familia fulani kwa hisia au chuki.
CCTV inaleta ukweli wa kisayansi na kuondoa hisia uzushi na kutambulisha uhalisia wa watu wanaokuzunguka.
Exactly.. kuna clip nimeona majuzi Mwizi kaingia ktk nyumba ya mtu alafu Kanya na kaiba vile vile.. 😂
 
Ukweli Uliofichuliwa na CCTV: Bila uwepo wa kamera za usalama, jirani huyo angemiliki shutuma nzito za utekaji, mauaji, au hata ushirikina, jambo ambalo lingeweza kusababisha uvunjifu wa amani au yeye kushitakiwa kimakosa.
Na wangejazana wote mahakamani kushutumubkwa kitu hawana uhakika nacho.
Awali nlishangaa kwanini watu wanalaumu umaskini.lakini kumbe mienendo Yao na historia dhidi ya huyo mtuhumiwa ndio shida ya yote
 
Mhh kazi sana..
Mungu anisaidie nkipata chance nizitafute pesa Kwa Naman zote
Pamoja na kukulia kwenye shida sijawahi kuwa hivi.
Kuna mtu namjua wa karibu sana alijenga mahali,Maisha yalikuwa ya amani mpaka alipohamia jirani,Tena kwenye nyumba hajaimaliza akaamza mashindano.ameikimbia nyumba
Subiri ntafungua Uzi wa hili ntakutag uone visa Kwa kirefu🤣
Waliniuzia barabara ikiwa inafahamika kabisa haipaswi..nikanunua na kutengeneza wakapitisha magari yao bila shida.
 
Uswahili ni uswahili tu. Wapo waswahili wenye hela na wasio na hela pia wapo wenye elimu na wasio na elimu. Nilihamia sehemu moja nje ya mji nikiwa mtu wa kwanza kwanza. Wakaja majirani zangu kujenga wakanikuta na ni watu wameenda shule tu vizuri. Nikawapokea nikafurahi kuwa wakimaliza ujenzi walau usalama utaongezeka kwa kuwa tutakuwa wengi. Nikawa nawasaidia vitu vidogo vidogo wakikwama wakati wanafanya ujenzi maji, umeme, mchanga, nawahifadhia mafundi wao vifaa vya ujenzi, n.k. lengo wahamie haraka.

Aisee walipohamia nilijuta kuwajua maana kila ubaya nilipewa na mbaya zaidi wakaona haitoshi wakaamua kabisa kunipakazia uwongo/ubaya mpaka mtaa wa saba huko. Sasa kwa kuwa mimi sio fundi wa upuuzi kama wao nikasema tu kitu kimoja siwezi kupita na spika mitaani kukanusha uwongo wao na Mungu sio Juma Nature. Nilichoamua kuanzia wakati huo niliposikia stori zao kwa majirani wengine wa mbali ambao ni wema niliamua mimi na wao basi nikawa bandidu tukikutana barabarani "mambo jirani - poa" imetoka mpaka leo. Matokeo yake wakaanza kulalamika eti nimewachunia nikabaki na chekea tumboni. Na tabia ni kama ngozi wao kwa wao wakaleteana uswahili wakapaziana uwongo sasa hivi hawasemeshani tena. Mimi nimebaki nawaangalia nimevaa uso wa mbuzi sitaki hata mmoja anisogelee kabisa.

Kwa kifupi uswahili ni kitu kibaya sana na ukimshtukia mtu ni mswahili mteme mazima utapata amani ya moyo hasa ukizingatia tunaishi muda mfupi sana hapa duniani.

Ni mtizamo tu.
 
Mhh omba yasikukute
Hakimu mmoja alimfunga mtu kifungo kirefu kwa ushahidi wa kuokoteza.. Ndugu wakajiapiza kulipa kisasi
Basi wakatafuta watu wakafanya maarifa mpaka wakapata funguo ya gari yake kisha wakaenda kuchonga bandia
Baada ya hapo wakafanya mpango mochwari wakapata maiti ya mtoto asiye na ndugu.. Wakataimu usiku nyumbani kwake akiwa kalala wakaruka ukuta wakafungua buti na kuiweka ile maiti
Halafu wakaichoma tairi sindano ili iwe na slow pancha

Kulipokucha Hakimu akajiandaa kwenda kazini akaondoka... Akiwa njiani kwenye foleni dereva mmoja akamwambia tairi moja ya nyuma imepungua sana upepo na hafiki mbali
Hivyo akatafuta sehemu ya pancha na kuongeza upepo.. Fundi kukagua akakuta tairi Ina slow pancha
Ile fundi anafungua buti achukue jeki na spana anakutana na maiti
Kumbe wale walioiweka ile maiti walikuwa wanamfuatilia

Yaani hakimu hata kabla taharuki haijamuisha kwamba ile maiti imrfikaje pale.. Akajikuta keshajaziwa watu huku akishutumiwa kaua atoe kafara ili apandishwe cheo😭

Safari ya kazini mahakamani ikaishia pale na kwenda kuanza maisha mapya gerezani kesi ya mauaji
Ilimchukua miaka mitano kuweza kuthibitishwa hana hatia huku aliyemfunga akitoka baada ya miezi 6.. Maana alikata rufaa na kushinda

Hii simulizi inaitwa MAITI NDANI YA BUTI
 
Kwa kifupi uswahili ni kitu kibaya sana na ukimshtukia mtu ni mswahili mteme mazima utapata amani ya moyo hasa ukizingatia tunaishi muda mfupi sana hapa duniani.💪🏿👌🏿
 
Hakimu mmoja alimfunga mtu kifungo kirefu kwa ushahidi wa kuokoteza.. Ndugu wakajiapiza kulipa kisasi
Basi wakatafuta watu wakafanya maarifa mpaka wakapata funguo ya gari yake kisha wakaenda kuchonga bandia
Baada ya hapo wakafanya mpango mochwari wakapata maiti ya mtoto asiye na ndugu.. Wakataimu usiku nyumbani kwake akiwa kalala wakaruka ukuta wakafungua buti na kuiweka ile maiti
Halafu wakaichoma tairi sindano ili iwe na slow pancha

Kulipokucha Hakimu akajiandaa kwenda kazini akaondoka... Akiwa njiani kwenye foleni dereva mmoja akamwambia tairi moja ya nyuma imepungua sana upepo na hafiki mbali
Hivyo akatafuta sehemu ya pancha na kuongeza upepo.. Fundi kukagua akakuta tairi Ina slow pancha
Ile fundi anafungua buti achukue jeki na spana anakutana na maiti
Kumbe wale walioiweka ile maiti walikuwa wanamfuatilia

Yaani hakimu hata kabla taharuki haijamuisha kwamba ile maiti imrfikaje pale.. Akajikuta keshajaziwa watu huku akishutumiwa kaua atoe kafara ili apandishwe cheo😭

Safari ya kazini mahakamani ikaishia pale na kwenda kuanza maisha mapya gerezani kesi ya mauaji
Ilimchukua miaka mitano kuweza kuthibitishwa hana hatia huku aliyemfunga akitoka baada ya miezi 6.. Maana alikata rufaa na kushinda

Hii simulizi inaitwa MAITI NDANI YA BUTI
Alijifunza
 
,Kuna usemi usemao "Ndugu wa karibu ni jirani." Lakini kwa nyakati hizi tunazoishi, msemo huu unaanza kupoteza maana kwa kasi sana.

Leo hii majirani wamekuwa chanzo kikubwa cha maumivu, fitina, na roho mbaya za waziwazi, mara nyingi zikisababishwa na wivu wa maendeleo au chuki binafsi zisizo na miguu wala mikono.

Tukio la hivi karibuni lililotokea mkoani Arusha limestusha nchi nzima na limenifanya nitafakari sana kuhusu usalama wetu na familia zetu mitaani.

Ni kisa cha mtoto mlemavu aliyekuwa akitafutwa kwa udi na uvumba, na hatimaye akakutwa ndani ya gari la jirani.
Cha kushangaza na kusikitisha zaidi, huyo mtoto alitambaa na kuingia mwenyewe kwenye gari. Yaani bila uwepo wa kamera za usalama (CCTV), ukweli wa hili jambo lisingejulikana kabisa!. Mama wa watu angesingiziwa bure na kushitakiwa kwa kitu ambacho hajakifanya.

Kamera zimeokoa maisha ya watu wawili hapa: mtoto mkemavu na mama aliyekuwa anaenda kusingiziwa.

Binafsi nimejikuta nikitafakari maisha tunayoishi mitaani kwetu. Ukiishi kwa upole na unyenyekevu, majirani wakorofi wanakuona mnyonge na kuanza kukanyaga haki zako. Ukiamua kuwa mkali na kuweka mipaka, unaonekana una mdomo, una maringo, na unaharibu sifa yako kwenye jamii.

Naomba tujadili wakuu:Je, umeshawahi kukutana na jirani mwenye kiwango hiki cha roho mbaya au utata? Ulimnyoosha vipi akashika adabu yake?

Kuhusu teknolojia: Je, unadhani imefika wakati sasa hivi kufunga kamera za CCTV nyumbani isiwe tena anasa, bali iwe ni hitaji la lazima la usalama kwa kila familia (hata kama ni za bei nafuu)?

Mbinu gani ni bora zaidi mtaani? Ni kumkaushia kabisa jirani mkorofi na kumpotezea (silent treatment), au ni kupambana naye kisheria ili kuondoa uoga?

View: https://www.facebook.com/share/v/1CtdTiFuLM/

Inasikitisha sana mkuu Mshana Jr . Baadhi ya majirani wana roho mbaya sana aisee! Kuishi na majirani wa aina hii ni tatizo sana.
 
Pole mimi nyumba niliyopanga nimepanga na wa Nigeria tena wanaume wacheza mpila sijui wanatafuta Team kwa mjibu wao hawa nilijua kwa vile ni wageni hawana tabu

So tukawa tumezoeana kiasi fulani maana tulikua una enda gym moja ni masela

Hawana jiko wapo kwenye room moja master

Mimi jiko ninalo baasi wakaomba wawe wanatumia vitu vyangu vyombo jiko nk..
Sasa kuna mmoja demu wake kaja hapa na ajabu wanalala wote chumba kimoja🙌

Sasa najuta hilo jiko wameligeuza lao sipiki mpka wa malize wakimaliza kupika hawasafishi🙌🙌

Nimwambia huyo demu wao walau awe ana safisha akachukia
Saiv nawaangalia but nimejifunza sirudii tena nimekoma
Kitu siwezagi ni kuvumilia kitu kinachoninyima amani!
 
Back
Top Bottom