Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Roma Mkatoliki amwibua Mwakyembe, adai hana elimu ya kumshauri yeye mwenye digrii 4. Kama anapenda siasa aanzishe chama cha siasa

Sasa nina mashaka na Digrii za Mwakyembe:
1) Ni kigeugeu. aliwahi kulishwa sumu na nywele zikapeperuka. sijui anavaa wigi? lakini baada ya kuvutishwa bangi ya CCM, sasa kashika adabu anaimba mapambio na kujitoa ufahamu
2) Alikiuka maandishi yake mwenyewe kwenye utafiti wake aliouchapisha, akatoa msimamo tofauti bungeni. Tundu Lissu akamshika shati. Msomi gani huyo asiyeamini alichoandika mwenyewe, tena baada ya kufanya utafiti?

Lakini pia, kuwa na digrii haina maana unatumia common sense. Kama Mwakyembe ana digrii 4, basi Roma Mkatoliki anazo 10!!

Tusichanganye vitu viwili kuwa na akili(interegent) na kuwa na elimu (educated) mtu anaweza akawa na elimu lakini hasiwe (intelligent) au hasiwe huru katika kuelezea ukweli kwa sababu za kulinda maslai yake tunawaashuhudia wengi tu katika kipindi hiki
 
Kwanza kuwa na degree zote hizo na haushauriki ni kuonyesha dhahiri Degree Zake hizo Nne (4) hazijamkomboa kutoka kwenye ujinga akokuwepo nao toka mwanzo Afu 4 Helpless Degrees na mwenye degree moja Yenye msaada yupi mwenye Faida kama akoshikilia nchi anashaurika iwe wewe yeye MHEPERE Embu atoe Hoja yenye Mashiko sio kutambia Elimu alopo nayo.
 
[emoji23]
tapatalk_1573907570153.jpeg
 
Mwakyembe kachemsha sana sasa Roma ndiyo msomi zaidi yake kwani kukurupuka kutoa matamko pasipo kutafakari ndiyo madhara yake haya
Roma akili kubwazi usilinganishe na akili za makaratasi za Mwaky
 
Albert Einstein aliwahi kuulizwa akili ni nini? What is intellect? Akasema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani.

Kwa mujibu wa Einstein kuna watu wakiondoa yale waliyofundishwa darasani, vichwa vyao vinabaki vitupu. Kitu pekee walichojaza kichwani ni walichofundishwa darasani. Hawa ndio hujisifia vyeti, au idadi ya "digrii" walizonazo. Hawana akili, japo wana elimu.

Einstein alisema hakuna uhusiano kati ya elimu na akili. Kuna watu wana elimu lakini hawana akili, na wengine wana akili lakini hawana elimu. Ni bora uwe na akili ukose elimu, kuliko uwe na elimu ukose akili.

Icons wa Sayansi kama Isaac Newton, Galileo Galilei na Archimedes of Syracuse hawakuwa na elimu yoyote ya cheti, diploma wala degree, lakini walikua na AKILI. Ugunduzi wao mpaka leo unaiongoza dunia.

Akili siku zote ni "superior" kuliko elimu kwa sababu akili ndio ilibuni elimu. Yani watu wenye akili walikaa wakaweka utaratibu wa mtu kukaa darasani na kujifunza kwa kipindi fulani, kisha apimwe kwa mitihani na atunukiwe cheti. Ubunifu huo ulifanywa na wenye akili. Kama huamini jiulize mtu wa kwanza kutunukiwa degree duniani alifundishwa na nani?

So mtu mwenye akili lakini akakosa elimu, ni msaada kwa jamii kuliko mtu mwenye elimu lakini akakosa akili. Mark Zukerberg hakumaliza shule lakini kwa kutumia akili amebuni mifumo rahisi ya mawasiliano kupitia mtandao.

Yeye ndiye mmiliki wa Facebook, Whatsapp na Instagram. Wale maprofesa waliomuona "kilaza" darasani leo wanatumia ubunifu wake kuendesha maisha yao. Kama sio FB basi wanatumia Instagram au Whatsapp. Maprofesa wenye elimu kubwa wamezidiwa ujanja na "kilaza" mwenye Akili.

Usijidharau kwa uchache wa madarasa ulionayo, unaweza kuwa na akili nyingi kuliko mwenye degree 4.

Kumbuka Einstein alisema akili ni kile kinachobakia baada ya kuondoa yote uliyofundishwa darasani. Jiulize ukiondoa yale uliyofundishwa darasani unabaki na nini? Yani ukiondoa hiyo diploma, degree au PhD unayojivunia, kichwa chako kinabaki na nini?

Kama kuna kitu kinabakia basi hicho kinachobakia kinaitwa "AKILI". Na kama hamna kinachobakia basi hilo bichwa halina tofauti na mtungi wa gesi.
#SinaAkili
#NinaDegree4

Malisa GJ
Hii nondo ineenda shule.
 
T
Mlaleo,
Halafu kwa kuongezea Roma ni mwalimu na ni graduate yule. Mwambie mzee atulie dawa iingie vizuri.anavyojitingisha hivyo sindano itavunjikia ndani
Tena kapiga PCM yule,logic imelala usipime.
Kwani waziri kwenye hizo degree 4 kasoma logic?.
Ndo maana Roma amemvuruga ubongo.
Yule Ni mwalimu wa Math na Chem,waziri sijui alisoma Nini advance level.
 
Na yule mbunge wa Mtera akiwa anaongea bungeni anamtazamaje? Maana na yeye ni LY. Huwa anamwona anafuka tu Moshi?
 
Pale anayechaguliwa kuwatumikia waliomweka kwenye kazi anapojisahau na kuanza kuwatukana.., hio inaitwa kulewa madaraka...

mwananchi yoyote anaweza na kupaswa kumshauri / kusema anachoona kinafaa kwake kwa wale wanaoishi kwa kutumia jasho lake (kodi)
 
Roma amedanganywa na wanasiasa wabaya tu
Roma amedanganywa na wanasiasa wabaya tu
Roma arudi shule jamani Mtu anaefundisha au aliwahi kufundisha chuo sio wa kumfananisha na alieishia darasa la saba jamani huo ni ukweli usiopingika Mwakyembe alipasua GPA kubwa Bachelor akabakizwa kuwa mwanataaluma UDSM huwezi fananisha na Msanii yeyote hapa nchini
Roma amedanganywa na wanasiasa wabaya tu
We mwen
Wape. Waambie ukweli. Kushabikia ujinga hakujawahi kumtoa mtu. Wasanii wote waliotajirika dunian sio wale waliochanganya siasa na sanaa. Wasanii wote dunian kote waliojaribu kuchanganya siasa na sanaa waliishia kubaya sana.

Sanaa haijawahi kuchanganywa na siasa na ikabaki kuwa sanaa.

Mnavyochangia jaribun kuwa real kwenye reality. Sio kushabikia vitu ambavyo havijawahi kuwa positive hapa dunian.
We mwenda wazim kweli ndio nyie nyie mapunguani, kwani Roma amekwambia anataka kuwa bilionea?wewe na mwa kiembe akili zenu za kukodisha,fisi maji wewe
 
Nimeishia lasaba mkuu,ila huu upupu wa Waziri siwezi kukubaliana nao,na sio mara ya kwanza kuropoka,huko wizara ya michezo alihamishiwa baada ya kuropoka kwamba huwezi kufunga ndoa bila kuwa na Cheti cha kuzaliwa huku akijua asilimia kubwa ya watanzania hasa vijijini hawana hivyo vyeti,naona anarudia makosa.
Kiprotokali huwezi kubishana na mtu mwenye less credentials au higher credential than yours.

Yeye anazo nyingi sana aisee 4, jadadeki wakati wao wanasoma sisi tulikua tunachunga mbuzi kwa Babu.

Tulishindwa kupanga kumbe automatically tulipanga kufeli.
 
Hakuna sehem aliyotajwa lakini bado makalio yanamwasha..!
Hata Mimi niidhani labda katajwa kwenye mashairi kumbe anajihami kwa Jiwe asijiulizwa huo wimbo umeusikia?nimeusikia Mzee na huyu kijana nilishamuonya anzishe chama cha siasa.teh,teh ,teh ......
 
Roma arudi shule jamani

Mtu anaefundisha au aliwahi kufundisha chuo sio wa kumfananisha na alieishia darasa la saba jamani huo ni ukweli usiopingika

Mwakyembe alipasua GPA kubwa Bachelor akabakizwa kuwa mwanataaluma UDSM huwezi fananisha na Msanii yeyote hapa nchini

Gpa kubwa ya ngapi? Itaje. Bachelor aliyosomea ni ya nn ?

HAuwezi kumfananisha na msanii yoyote kwenye mambo gani? Au kwenye uandishi wa mashairi ,kama hivyo nyimbo yake iko wapi tuzilinganishe na za roma.

Ametusaidia nn sisi na hizo elimu zake nne ,au kaisaidia tu familia yake ? Vizuri ukaweka wazi watu wajue.
 
Back
Top Bottom