Rostam Aziz anunua asilimia 31.5 ya Williason Diamonds (Mwadui)

Fikiria upya baada ya hizi details halafu njoo tena;
1. Almasi zipo toka Tanzania iumbwe na Mungu ila watanzania wakati huo hawakujua kama zina thamani mpaka alipokuja Williamson miaka ya 1940s huko

2. Anayenunua ndiyo anazipa thamani, asiponunua hata leo zitabaki hazina thamani

3. Tanzania haiweki hata Tsh 100/- kwenye utafiti na uchimbaji lakini inapewa 25% ya hisa

4. Tanzania haina teknolojia ya kuchimba hata kama tukiamua kuwafukuza Petra

5. Debeers au Anglo -American Mining ndiyo wamiliki wa makampuni haya ya akina Barrick, ACACIA, Petra etc. Wanaandika jina Ku suit mazingira ya mahali.

6. Hao hao Anglo American ndiyo solo la la haya madini. Kwa hiyo unaweza ukapata teknolojia ya kuchimba ila ukaosa pa kuyauza
 
Haya makubaliano yanaweza kuwa na faida kubwa sana kwa Williamson diamonds kwa sababu Petra ilikuwa inapumulia mashine.
Lakini uko mbeleni sitashangaa Rostam Aziz akinunua asilimia zote za Petra na kuwa majority shareholder!

Na baadae atachonga dili aiuzie serikali kwa $100 million. Subiri uone
 
Nimeona nikianza kuchambua point moja ya nyingine tutachukua muda mrefu sana nikuulize tu swali moja; Hivi Botswana wanavyofaidika na Almasi zao ni sawa na sisi ?

Kumbuka uchimbaji una athari za kimazingira na inaweza kuleta kero kwa wakazi wanaozunguka mahali husika, kwahio issue ni kupata the best deal you can na sio any deal ili mradi tu uchimbe; tusiongelee sana Diamonds ambazo Debeers wana-manipulate soko ila tuongelee madini mengine kama gold (yenye matumizi lukuki hata industrial na ni easier to sell); narudia tena kuliko kuyagawa kama zawadi ni bora kungojea tupate akili sababu hayaozi...
 
Pale Igunga kaacha nyumba za tembe tupu
 
Kabila gani na uko wa nani? huyu ni mhindi 100%
 
Rostam ni mzawa? kabila gani na ukoo wa nani?
 
Dola milioni 15 ni hela ya kununua almasi, si hela ya kununua hisa za asilimia zaidi ya 30 katika mgodi wa almasi.
Haya mambo naona ni kama yaliyotokea Russia ilivyosarambatika na watu kujichotea Keki ya Taifa kwa bei za kishikaji...., The Rise of the likes of Roman Abramovich

Sisemi kwamba hapa ndio kinatokea kitu kama hicho...., Am just saying its possible watu kujimilikisha Commanding Heights of the Country Economy
 
Ndugu yangu hata kote kule uwanja wa ndege, uwanja wa golf, boths , Uhindini , ujamaa quarters,nk. Almasi zilikuwepo ila nafikiri kufikia leo watakuwa zile kubwakubwa walishazimaliza......bongo kweli huwa ni shamba la bibi......hahahaaa
Though hawawi majority shareholder lkn wanaweza kubadilisha sana biashara na uzalishaji wa huu Mgodi! Sijui kule Makamba Jeki bado kuna almasi?
 
Kumbe Rostam Aziz ni Mzawa mwenzetu! Nilijua ni Mtanzania mwenye asili ya India.
Rostam Aziz babu zake wameanza biashara tabora 1850,makao makuu kijijini mwisi,igunga...ana mizizi na nchi kuliko wanaojiita waha ilhali ni warundi,au pengine kuliko hayati mkapa kwa mujibu wa mzee lyatonga mrema
 
Botswana kule wana hisa 49% government na 51% Debeers( kampuni inaitwa Debswana), na Namibian 49%government, na 51% Debeers,(kampuni inaitwa Namdeb)...huko walijitahidi toka mwanzoni kwa win-win situation, na sio sie tulileta siasa mapema sijui hao mabeberu ni., hivyo tukaanza kuwafukuza taratibu....
 
Huyu Jamaa alijiuzulu UBUNGE wa IGUNGA na KUSEMA Hataki SIASA UCHARWA[emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…