RPC Dodoma atumbuliwa baada ya kutoa taarifa tata ya binti kulawitiwa anaweza kuwa anajiuza

Tumeona taarifa kwenye vyombo vya habari yenye kichwa cha habari kinachosema, "RPC; ANAYEDAIWA KUBAKWA NA KULAWITIWA ALIKUWA KAMA ANAJIUZA", kauli inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hayo yametokana na mazungumzo kwa njia ya simu na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi ambaye miongoni mwa maswali aliyomuuliza kamanda (mwandishi huyo), Je upelelezi wa kesi umekamilika? na swali lingine alilomuuliza inadaiwa alikuwa anajiuza? Majibu ya kamanda aliyomjibu mwandishi huyo ni kwamba hata kama ni hivyo hangestahili kutendewa hivyo.

Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa kauli hiyo kama inavyoonekana kwenye hicho kichwa cha habari siyo msimamo wa Jeshi la Polisi kauli sahihi ni kama zilivyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kwa umma Agosti 4,6 na 9,2024. Vilele tungependa kujulisha kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani leo Agosti 19,2024.

Jeshi la Polisi lingependa kuomba radhi kwa kila mmoja aliyeguswa na kuchukizwa na kauli hiyo inayosambaa kwenye vyombo vya habari wakati ufuatiliaji ukifanyika kupata usahihi wake. Aidha wakati uchunguzi huo wa kupata usahihi wa kauli hizo, Mkuu wa Jeshi la Polisi amefanya mabadiliko madogo kwa kumhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Theopista Mallya kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP George Katabazi.

View attachment 3073887

Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
Kumhamisha toka Dodoma kwenda Dar es Salaam ni promosheni kwa kazi nzuri aliyoifanya, hongera Mallya.
 
Weka link ya hiyo akaunti ya Polisi iliyopo Instagram
Ukiacha maneno kama "Tumeona, Tungependa" ambayo hayawezi kuwa lugha ya Kitaasisi, na mwandishi kutokujua wapi inakaa herufi kubwa na wapi panahitaji space, taarifa haipo katika akaunti ya polisi huko insta
 
Hivi kama ushahidi inaonyesha dogo alikua anajiuza haikutakiwa kusema?? Wale jamaa ndio wanamakosa kumrekod lakin Yule BINTI nae mpaka kafika pale itakua kuna kitu
Afande kaongea ukweli wa kesi .ila kawaida ya ukweli hua mchungu ..kumbe hata hao c maafande ni wahuni tuh wameamua kumfanyia uyo Dada
Na mtungo wadada wengi wamepigwa ila hawajarekodiwa ila izo case ni nyingi mno mtaani hasa arusha
 
Ameondolewa madaraka tu, lakini rank yake inabaki palepale, zile bahasha za URPC ndio basi tena.

Makao makuu ni kusoma magazeti tu hakuna wa kukuletea rushwa.
Ndio hicho nilichokizungumzia nafasi ya kimadaraka
 
Tumeona taarifa kwenye vyombo vya habari yenye kichwa cha habari kinachosema, "RPC; ANAYEDAIWA KUBAKWA NA KULAWITIWA ALIKUWA KAMA ANAJIUZA", kauli inayodaiwa kutolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hayo yametokana na mazungumzo kwa njia ya simu na Mwandishi wa gazeti la Mwananchi ambaye miongoni mwa maswali aliyomuuliza kamanda (mwandishi huyo), Je upelelezi wa kesi umekamilika? na swali lingine alilomuuliza inadaiwa alikuwa anajiuza? Majibu ya kamanda aliyomjibu mwandishi huyo ni kwamba hata kama ni hivyo hangestahili kutendewa hivyo.

Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa kuwa kauli hiyo kama inavyoonekana kwenye hicho kichwa cha habari siyo msimamo wa Jeshi la Polisi kauli sahihi ni kama zilivyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kwa umma Agosti 4,6 na 9,2024. Vilele tungependa kujulisha kuwa watuhumiwa watafikishwa mahakamani leo Agosti 19,2024.

Jeshi la Polisi lingependa kuomba radhi kwa kila mmoja aliyeguswa na kuchukizwa na kauli hiyo inayosambaa kwenye vyombo vya habari wakati ufuatiliaji ukifanyika kupata usahihi wake. Aidha wakati uchunguzi huo wa kupata usahihi wa kauli hizo, Mkuu wa Jeshi la Polisi amefanya mabadiliko madogo kwa kumhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP Theopista Mallya kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi SACP George Katabazi.

View attachment 3073887

Pia soma>> Polisi: Wanaotuhumiwa kubaka na kulawiti ni kama wavuta bangi, hawakutumwa na Afande, yule dada alikuwa kama anajiuza
Serikalini kuna watu wengi sana wenye akili ndogo yani hawana uwezo wa kiakili
 
Teuzi za akina Dr Mwigullu, Dr Kigwangalla, MwanaDiwani nk zote zilianzia hapa Jf

Bado Lucas na ChoiceVariable 😂
Mwanadiwani bila shaka alikuwa.... Lizaboni wengi walimhisi ni Madelu lameck nchemba huku hamy d akidaiwa ni Mwana wa Moses wakati huo huo buku 7 from lumumba wakitumia mheko kujibu hoja... Alipoingia mwendazake magogongoni na kwenda lumumba aliwafurrumusha wote
 
Uyo shangazi aliongea kumlinda mshangazi mwenzio ..

Polisi ni kazi ya laana .
Can you imagine unamkosesha mtoto wa mwanamke mwenzio haki. na tena una mchafua unatengeneza uongo eti "kama alikuwa anajiuza" sure? Wakati kwenye clip wabakaji wanamtuhumu kwa sauti kabisa wametumwa na afande.
kweli hii ni kazi ya laana
 
Back
Top Bottom