RPC Muroto atoa onyo kwa BAWACHA, asema wanaotaka kuandamana watakipata wanachokitafuta wakasimulie wenzao huko Geita

RPC Muroto atoa onyo kwa BAWACHA, asema wanaotaka kuandamana watakipata wanachokitafuta wakasimulie wenzao huko Geita

Haki bila wajibu sio, wafuate tu sheria wasiandamane tu kwa jaziba wasije vunjwa viuno bure, kama ni mandamano halali hata mie nitakuja.
 
Wamejipanga kuwamiminia risasi sio,vitisho kamazama za ukoloni!!
 
Wanawake BAWACHA nendeni tuone polisi atakae wapiga. Nendeni.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma amesema ofisi yake haina taarifa rasmi za maandamano ya bawacha hivyo atakayeandamana atakutana na mkino wa dola.

Kamanda Muroto amewataka akina mama hao waliopanga kuandamana waje na computer na madaftari ya kuchukulia notisi ili waandike kile watakachokutana nacho kisha wakawafundishe na wenzao wa huko Geita ili liwe somo la keheshimu sheria na taratibu zake.

Source ITV habari

My take; Kwa kuwa Bawacha hawajaanza Safari ni busara wakahairisha kama Simba na Yanga!
" Nimepishana na mabasi 7 njiani shelui yakitokea kanda ya ziwa kuelekea dodoma. Kesho ni kesho"
 
Hebu muoneni huyu kamanda!

Anawaonya Bawacha kuhusu maandamano yao huku akiwa flanked na mapolisi wanawake waliovalia mavazi maalumu [ambayo nahisi ni ya kupambana na ghasia] huku wameshikilia mabunduki na wakiwa wamenuna!

What the hell is this?


Ni ushamba tu, huyu ni wale 60% ambao wapo kazini lakini siyo competent! Labda alienda shule kamanda wetu, lakini hakuelimika!
 
Hawa Bawacha mda wa kufanya maendeleo wanataka wakaandamane.. Waandamane zijengwe ofisi za chama chao sio ile stoo ya mkaa ufipa pale.
 
Aliaminishwa kwa kijisheria kipumbavu kuwa hatashitakiwa hata akisigina katiba akapewa maekekezo mkwara juu lazima waweke watu wao toka upinzani kukidhi takwa la kuwa upinzani na kuweka wenyeviti kamati za bunge toka upinzani hela za demokrasia zije.....kiburi hicho ndio kinamfanya akomae......historia haitamuacha salama ......zike dola mil 12 matibabu ndio bait kwake toka mwendazake.....
 
Amewaambia wachukue daftari na kompyuta ...!!! Basi sawa
 
Gilles Muroto amesema "Asiyefunzwa na mama yake atafunzwa na kamanda wa polisi dodoma"

Huyu mzee eti kuna watu wanampigia chapuo awe IGP!!

Kuna sehemu tumekosea sana sisi kama nchi.
hahahaha mkuu hiyo methali ameitunga lini..
 
Anataka kumkwamisha Mama Yetu.

Kwani Katiba inasemaje kuhusu huo uhalali wa hao wabunge?
 
Na ni haki yao kikatiba,ruksa kufanya maandamano ya amani,ba ulinzi mnapewa,ila uonevu huu.
Gilles Muroto atatoa Ulinzi na uuokoaji.. Kwani hamza uwezo wa kuwakilisha malalamiko bila kukimbizana?.

Mwana kulitafuta, mwana kulipata.
 
Huu sasa ni muendelezo
Toka pambano la Yanga/Simba
To pambano Bawacha/Covid19

MAMA shituka
 
Back
Top Bottom