Rufaa ya kina Mdee mbele ya Baraza Kuu dhidi ya Kamati Kuu CHADEMA: Kicheko kwa G19, Kilio kwa kina Mbowe

Rufaa ya kina Mdee mbele ya Baraza Kuu dhidi ya Kamati Kuu CHADEMA: Kicheko kwa G19, Kilio kwa kina Mbowe

Licha ya kudumu kwenye tasnia ya habari kwa muda mrefu mpka leo hii hujajua sehemu sahihi za kupata habari za uhakika na wewe unaokota screenshot???

Shame on you Pascal njaaa
Huyo ndiyo maana aliingizwa cha kike na Kigogo juu ya msamaha feki kwa yule chinga aliyeshindwa kusoma kiapo.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ukienda mahakamani kabla ya ku-exhaust internal remedial options inapoteza kesi mwanzoni kabisa via PO's.
Sasa kwa madai ya huyo muhusika kuna mashiko yapi yatakayoshawishi wasikiliza rufaa kupindua maamuzi ya kamti kuu?Mfano ushahidi wa wao kuapishwa Dodoma wataupindua vipi?

Aliyetakiwa kuwapa taarifa kwamba wameteuliwa kuwa wabunge ni nani? Kama ni katibu mkuu,je Ni yeye aliyewataarifu na wana ushahidi?
 
Aliyetakiwa kuwapa taarifa kwamba wameteuliwa kuwa wabunge ni nani? Kama ni katibu mkuu,je Ni yeye aliyewataarifu na wana ushahidi?
Katibu Mkuui hahusiki.
Naye anasikia kwenye media kama walioteuliwa.
Kazi yake ni kupeleka orodha NEC na kurudi ofisini akisubiri tangazo.
 
Bandiko linaongelea mawili: Umuhimu wa Baraza kuu kusimamia

1. Substantive justice
2. Procedural justice

Kuweka precedence nzuri kwa chama ni jukumu la Baraza Kuu.
Summary yako sijui ina maana gani maana haya mambo ni obvious Halima kwa kushirikiana na Tume and Ndugai anaelewa fika agenda yake hivyo bullet 1 and 2 are vaporous.
Mama Amon sometimes human being common sense must prevail.
 
Summary yako sijui ina maana gani maana haya mambo ni obvious Halima kwa kushirikiana na Tume and Ndugai anaelewa fika agenda yake hivyo bullet 1 and 2 are vaporous.
Mama Amon sometimes human being common sense must prevail.
Ndugu yangu, mie nimeripoti yale niliyoambiwa.
Karibu tuyajadili kulingana na Katiba, Kanuni na Taratibu za Chadema zilizo kwenye karatasi.
Lakini pia, kwa kutumia common sense kama unavyopendekeza.
 
Unawadharau waandishi wa aina hii hapa chini sio?

View attachment 1662699

Nina shaka kuhusu uhalisia wa hii inayodaiwa kuwa ni rufaa ya waliofukuzwa kwenye chama cha CHADEMA. Kinachozidi kunifanya niitile shaka ni lugha ya kebehi kwa Mbowe ambayo imetumika kwenye kichwa cha habari ambayo sidhani kama wakina Halima Mdee wanaweza kuibariki. Katika sakata lote hili wamekuwa wakimzungumzia Mbowe kwa heshima kubwa na haiwezekeni mara hii waanze kumsimanga. Aidha, rufaa imeandikwa kama inaenda Mahakamani ambako hayo mambo ya procedural justice yanaweza kupewa uzito tofauti na kwenye Baraza ambalo wengi sio wana sheria na wanachotaka kujua ni kwa nini walikiuka wito wa Chama na nani alishirikiana nao hadi kutimiza lengo lao. Kwa kifupi, waliendaje bila baraka za chama chao na kama walipata baraka ni nani katika chama alitoa hizo baraka. Hayo mengine ya mbona hatukuambiwa makosa yetu hayana tija mbele ya Baraza la waliokuwa wanachama wenzao. Hasa kwa vile wengi wao bado wanauguza majeraha waliyoyapata kwenye uchaguzi uliopita. Wanachotaka kujua ni inakuaje viongozi walioamini kuwa ni wafia chama wenzao wageuke kuwa ni "wasiliti" wa chama ambacho wamekipigania kwa kiasi cha kukubali kufungwa, kupigwa na manyanyaso mengine kwa ajili yake? Wasipojibu hili kwa kisingizio kuwa hawakuulizwa itawathibiishia wajumbe kuwa hawajutii kilichotokea na nia yao ni kuwa wabunge kwa gharama yoyote ile, hata kama italeta mpasuko mkubwa kwenye chama ambacho wanadai wana mapenzi nacho. Kwa vile sidhani kama lengo lao ni kukivuruga chama walichokipigania kiasi kile ndio maana natilishia shaka uhalisia wa kilicholetwa humu maana nia yake ni kuhakikisha kuwa rufaa yao itatupwa mbali na kuondoa kabisa uwezekano wa wao kurudi kwenye chama chao cha awali. Wote tunajua ni upande upi utakaofaidika na hali hiyo.

Amandla...
 
Mhe. Halima Mdee na wenzake wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai, baada ya kula kiapo hivi karibuni.

"Sasa ni wazi kwamba, mimi na wabunge wenzangu 18, tulionyanganywa uanachama wa CHADEMA juzi, tutarudishiwa uanachama wetu asubuhi na mapema siku Baraza Kuu la CHADEMA litakapokutana kusikiliza rufaa yetu tuliyoiwasilisha kwenye Ofisi ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, juzi tarahe 27 Desemba 2020."

Haya ni maneno ya Mbunge mmoja wa viti maalum aliyeongea na mtandao wa Mama Amon, lakini ambaye hakutaka jina lake litajwe hadharani.

Alisema kwamba, kwa mujibu wa barua ya tuhuma dhidi yao, Mdee na wenzake 18 wanakabiliwa na "tuhuma sita na ambazo ni hafifu na zisizo na mashiko kisheria."


Tuhuma sita dhidi ya kina Mdee

Mbunge huyo, aliyekuwa na ukakamavu hata kuliko baadhi ya Wabunge wa kiume kwenye Bunge lililopita, alizitaja hatua kwa hatua tuhuma hizo kama ifuatavyo:

“Mosi, tunatuhumiwa kupora madaraka ya Kamati Kuu ya Chama kwa kushiriki katika mchakato wa kula njama ya kujiteua kuwa Wabunge wa Viti Maalum, kitendo ambacho kinadaiwa kuwa kinyume cha ibara ya 7.7.16(q) inayotamka kwamba kazi za Kamati Kuu zitakuwa ni pamoja na kuthibitisha uteuzi wa wagombea Uspika, Ubunge, na Baraza la Wawakilishi. ”

“Pili, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupanga njama za kuhujumu chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka kanuni ya 3(a)(i) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”

“Tatu, tunatuhumiwa kufanya kosa la usaliti kwa kupinga misimamo ya chama hadharani na nje ya vikao vya chama, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(a)(iii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama.”

“Nne, tunatuhumiwa kufanya kosa la kujihusisha na matumizi mabaya ya madaraka/upendeleo kwa kujipatia huduma au manufaa binafsi kinyume na taratibu kwa kutumia vyeo vyetu, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 3(e)(ii) katika Mwongozo wa Kamati za Maadili za Chama."

“Tano, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila kiongozi anatarajiwa awe na msimamo wa kuaminika, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.2(iv) ya Kanuni za Chama."

“Na sita, tunatuhumiwa kufanya kosa la kukiuka sharti linalotamka kuwa kila mwanachama anatakiwa kujiepusha na upinzani dhidi ya chama na wagombea wake na makundi ya majungu ya kugonganisha viongozi na wanachama hasa wakati wa chaguzi, kitendo ambacho kinadaiwa kukiuka Kanuni ya 10.3(iv) ya Kanuni za Chama.”

"Kilichotushangaza zaidi ni kwamba, kwa tuhuma zote sita dhidi yetu walizozitaja kwenye barua ya tuhuma yenye ukurasa mmoja pekee, hakuna maelezo yoyote yenye kuonyesha nani alifanya nini, lini, kivipi, akiwa wapi, akiwa na nani, na kwa nini, jambo ambalo kisheria linamaanisha kwamba hakuna mashtaka yanayojibika tuliyopewa" anaongezea huyo Mheshimiwa Mbunge .


View attachment 1662269
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akiwa anapanga mikakati ya kisiasa na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema

Baada ya kuzitaja tuhuma zao zote, Mbunge huyo anaongeza kusema kuwa, “kwa hiyo, tayari tumejibu tuhuma hizo na majibu yetu hayana chenga hata kidogo.”

Majibu katika rufaa ya kina Mdee

Mbunge huyo alifafanua kuwa majibu yao yako katika makundi mawili. Katika kundi la kwanza, watuhumiwa wanakanusha tuhuma zote kama zilivyoorisheshwa hapo juu.

Na katika sababu zilizo kwenye kundi la pili watuhumiwa wanahoji uhalali wa mchakato ulioutumika kuwatia hatiani.

“Mosi, ni kuhusu tuhuma zenyewe. Tunasema kwamba, kwa kuwa uteuzi wa wabunge hufanywa kutokana na ushirikiano kati ya Ofisi ya Katibu Mkuu na Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi, na sisi sio sehemu ya ofisi yoyote kati ya ofisi hizo mbili, ni wazi kwamba sisi hatukujiteua, na hivyo, anayepaswa kuulizwa nani alifanya uteuzi wa Wabunge wa Viti Maalum wa Chadema ni ama Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, au Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Mahera, au wote wawili, lakini sio vinginevyo,” anasema Mbunge huyo.

“Pili, ni kuhusu tuhuma zenyewe pia. Kusudi mtu atende kosa, lazima awe eneo la tukio. Lakini, ukweli ni kwamba, wengi wetu tulikuwa mikoani siku zile za uteuzi, kwa maana kwamba hatukuwa Dar es Salaam wala Dodoma ziliko ofisi za NEC na Chadema. Sisi kama viumbe wenye mwili hatuwezi kuwa sehemu zaidi ya moja kwa mpigo. Tunaongozwa na kanuni mbili, spatial locality and temporal locality (anwani ya mahali na anwani na muda). Mtu asiyekuwepo mahali fulani hawezi kutenda kosa mahali hapo,” anasisitiza Mbunge huyo.

“Tatu, ni kuhusu utaratibu. Kwa kuwa, kabla ya kikao baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu, kama vile Matibu Mkuu, John Mnyika, walikuwa mstari wa mbele kutumia mainstream and social media (vyombo vya habari vya kimapokeo na mtandao ya kijamii) kutushambulia wakijitapa kwamba wanasubiri kula vichwa vyetu, ilikuwa ni wazi kwamba, hata ndani ya kikao hakukuwa na utulivu wala usalama unaoweza kuruhusu hoja zikatolewa, kusikilizwa na kuamuliwa kwa haki bila jazba na mapigano. Ni kama tulikuwa tayari tumehukumiwa,” anasisitiza Mbunge huyo.

“Nne, ni kuhusu utaratibu pia. Kwa mujibu wa kanuni za natural justice (kanuni za haki asilia) tulifukuzwa bila kusikilizwa. Lakini, sio haki kumhukumu mtu ambaye hujamsikiliza. Tuliomba tuhakikishiwe usalama lakini hawakutuhakikishia usalama wowote. Kulikuwa na waandamanaji Makao Makuu ya Chama na kule kwenye barabara inayokwenda hotelini ambako kikao kilipaswa kufanyika. Hata kama kulikuwa na dharula, Kanuni ya 6.5(d) ya chama inasema kuwa mtuhumiwa lazima apewe haki ya kusikilizwa, ama kupitia mkutano wa uso kwa uso au mkutano wa kidijitali inaoruhusiwa na Kanuni za chama,” alifafanua Mbunge huyo.

View attachment 1662676

Devotha Minja (katikati) akiwa na begi lililo na kitu chenye ncha kali akiwaongoza wafuasi wa Chadema kwenye maandamano yaliyoziba njia ya kuelekea hotelini ambako kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kilikuwa kinafanyika

"Na tano, ni kuhusu utaratibu vile vile. Tunapinga mtindi wa uandishi wa tuhuma dhidi yetu. Kawaida ya kuandika tuhuma ni kwamba lazima kuwepo na mambo mawili. Moja ni statement of offence (kanuni iliyovunjwa) na jingine ni particulars of offence (kitendo na mazingira yake). Katika barua za tuhuma dhidi yetu hakuna maelezo yenye kuonyesha kosa lilifanyika lini, wapi, kivipi, na pamoja na nani. Kamati Kuu iliandaa mashtaka ya kubahatisha tu. Kwa hiyo, tutaliomba baraza kuu ama kuielekeza kamati kuu kuandika upya mashtaka haya au kuyatupilia mbali kwa kuwa hayajakidhi vigezo vya tuhuma zinazojibika," anahitimisha maelezo yake Mheshimiwa Mbunge

Kwa kuzingatia haya yote, sasa unasubiriwa utaratibu wa kichama kwa ajili ya kuitisha Baraza Kuu ili likae, lipokee makabrasha ya mashtaka na utetezi, liyasome makabrasha hayo, liwasikilize watuhumiwa wakijieleza kwa mdomo, na hatimaye kuamua haki iko upande gani kati ya Kamati Kuu na kina Mdee.


Chimbuko la rufaa ya kina Mdee

Takribani, mwezi mmoja uliopita, Kamati Kuu ya Chadema ilifikia uamuzi wa kuwavua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) baada ya kujiridhisha kwamba kina Mdee walikiuka Katiba, Kanuni na Maadili ya Chadema.

Aidha, Kamati Kuu iliamua kuwavua nyadhifa zote walizokuwa nazo ndani ya Chama na hivyo kuwataka kukabidhi mali za Chama walizokuwa nazo, sambamba na kuwazuia kujihusisha na masuala yoyote yanayokihusu Chama.

Kwa mujibu wa nakala za barua za tuhuma zilizo mikononi mwa mtandao wa Mama Amon, watuhumiwa wote walipewa njia mbili za kupitia. Njia ya kwanza ni kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Kamati Kuu kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.3 na 6.5.8 ya Kanuni za Chama.

Na njia ya pili waliyopewa watuhumiwa, kama mbadala, ni kuandika barua ya kuomba kurejea kwenye chama kwa mujibu wa Kanuni ya 6.5.4 ya Kanuni za Chama. Watuhumiwa wote waliamua kupitia njia ya kwanza, yaani njia ya kukata rufaa.


Magazeti ya Saed Kubenea yawaandama kimakosa kina Mdee

Kwa sababu ya uamuzi wao huu, jana mtandao wa mwanahalisioniline.com, unaomilikiwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers Limited, inayoongozwa na Saed Kubenea, uliwashutumu wabunge hawa ukidai kwamba, kwa sababu ya uamuzi wao wa kukata rufaa badala ya kuandika barua ya kuomba uanachama, "kina mdee wameanzisha vita mpya Chadema."

View attachment 1662268

Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukwatuhumu kina Mdee kuanzisha vita ndani ya Chadema

Hata hivyo, Mbunge aliyeongea na mtandao wa Mama Amon amepinga mtazamo huo. “Kwa kuwa haki ya kukata rufaa ipo kikatiba, sioni kwa nini vyombo vya habari vya kina Kubenea vinakuwa na mtazamo hasi dhidi ya uamuzi wetu,” alionyesha mshangao.

Taarifa zaidi zilizoufikia mtandao wa Mama Amon zinaonyesha kwamba, tangu siku za hivi karibuni, Saed Kubenea amenunua gazeti la Raia Mwema kutoka kwa wamiliki wake wa awali. Amekuwa analitumia kuwashambulia kina Mdee tangu walipofanya mkutano na waandishi wa habari tarehe 01 Desemba 2020.

Kwa mfano, katika toleo la tarehe 02 Desemba 2020, Gazeti la Raia Mwema lilikuwa na habari kuu yenye kicha cha maneno “Sakata la Viti Maalum: Limekwisha Hilo,” iliyoendelezwa kwenye ukurasa wa 3.

Habari hii iliufahamisha umma habari isiyo na uthibitisho kwamba "mkakati wa kutengeneza uasi uliratibiwa na Mdee kwa kushirikiana na wenzake watatu, Bulaya, Tendega na Agnesta."

Ndani yake kulikuwa na makala iliyoandikwa na mtu aliyejitambulisha kama Issac Kimweri yenye kichwa cha maneno, “Halima James Mdee: Kutoka Ukamanda hadi Yuda Ikarioti (uk. 9).”

Makala hii pia ilichapwa kwenye gazeti la la mtandaoni, linalomilikiwa na Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisioniline.com, chini ya kichwa cha maneno: Halima James Mdee: Kutoka U-kamanda hadi yuda Iskarioti.


View attachment 1662810
Sehemu ya ukurasa kwenye gazeti la Saed Kubenea, liitwalo Mwanahalisionline.com, ukimtuhumu Mdee kuwa na tabia za Yuda Iskarioti

Aidha, katika gazeti la Raia Mwema kulikuwepo na makala ya Mwandishi Maalum yenye kichwa cha maneno “Mdee ameshindwa kujibu maswali? (uk. 11).”

Makala hii ilidai kimakosa kwamba "kitu pekee alichoweza kueleza Mdee na wenzake 18 katika mkutano huo ni uamuzi wao wa kuwasilisha rufaa ya kupinga kufukuzwa kwao na Kamayi Kuu (CC), kwenye Baraza Kuu la Taifa (BKT), basi." Makala hii ilikiuka kanuni za uandishi kwa zaidi ya 75%.

Maandiko haya matatu hayakuzingatia kanuni za uandishi kwani yalijaa habari za kupotosha ukweli na ukweli nusu nusu. Badala yake yalilenga kuharibu taswira chanya waliyo nayo kina Mdee na wenzake.

Mhariri wa gazeti hili jipya ambaye hatajwi popote gazetini, kama ilivyokuwa inafanyika hapo zamani, alibariki makosa haya. Mmiliki mpya wa gazeti hili, Saed Kubenea, ndiye anajua mhariri ni nani na ndiye anamtuma kufanya yote haya.
TISs chini ya Diwani ovyo tu

Upuuzi gani huu
 
CHADEMA wasimamie msimamo wao sisi wafuasi tuendelee kuwaamini, ama wakubali hao wa mama waende bungeni tuwatose mazima. Kwa sasa chadema inabidi iangalie faida za muda mrefu kuwatosa hao wanawake, ama wawakubali wapoteze ushawishi kwetu wafuasi wao
Siku chadema wakifanya upuuzi tutawatosa
 
Nina shaka kuhusu uhalisia wa hii inayodaiwa kuwa ni rufaa ya waliofukuzwa kwenye chama cha CHADEMA. Kinachozidi kunifanya niitile shaka ni lugha ya kebehi kwa Mbowe ambayo imetumika kwenye kichwa cha habari ambayo sidhani kama wakina Halima Mdee wanaweza kuibariki. Katika sakata lote hili wamekuwa wakimzungumzia Mbowe kwa heshima kubwa na haiwezekeni mara hii waanze kumsimanga. Aidha, rufaa imeandikwa kama inaenda Mahakamani ambako hayo mambo ya procedural justice yanaweza kupewa uzito tofauti na kwenye Baraza ambalo wengi sio wana sheria na wanachotaka kujua ni kwa nini walikiuka wito wa Chama na nani alishirikiana nao hadi kutimiza lengo lao. Kwa kifupi, waliendaje bila baraka za chama chao na kama walipata baraka ni nani katika chama alitoa hizo baraka. Hayo mengine ya mbona hatukuambiwa makosa yetu hayana tija mbele ya Baraza la waliokuwa wanachama wenzao. Hasa kwa vile wengi wao bado wanauguza majeraha waliyoyapata kwenye uchaguzi uliopita. Wanachotaka kujua ni inakuaje viongozi walioamini kuwa ni wafia chama wenzao wageuke kuwa ni "wasiliti" wa chama ambacho wamekipigania kwa kiasi cha kukubali kufungwa, kupigwa na manyanyaso mengine kwa ajili yake? Wasipojibu hili kwa kisingizio kuwa hawakuulizwa itawathibiishia wajumbe kuwa hawajutii kilichotokea na nia yao ni kuwa wabunge kwa gharama yoyote ile, hata kama italeta mpasuko mkubwa kwenye chama ambacho wanadai wana mapenzi nacho. Kwa vile sidhani kama lengo lao ni kukivuruga chama walichokipigania kiasi kile ndio maana natilishia shaka uhalisia wa kilicholetwa humu maana nia yake ni kuhakikisha kuwa rufaa yao itatupwa mbali na kuondoa kabisa uwezekano wa wao kurudi kwenye chama chao cha awali. Wote tunajua ni upande upi utakaofaidika na hali hiyo.

Amandla...
1609287946362.png

Bado una mashaka?
 
Mkuu Matilda, msimtukane mtu matusi yahusuyo chastity of a woman, ni sawa na mtu mwingine kumtukana mama yako!. Wanawake wote ni mama zetu, waheshimu, unless una uhakika she's a bitch na ulimuona akijiuza ukalipia na ukahudumiwa!. Heshima kitu cha bure!.
Jf tuheshimianeni jameni!.
P
Nakubaliana na ulilolisema kuwa kuna haja ya kuheshimiana lakini iwe kwa wote sio wanawake peke yao. Aidha, kuna tofauti kati ya "bitch" na "whore". Sio lazima "bitch" ajiuze. Lakini ukweli unabaki kuwa sio vizuri kumuita mwenzako "bitch" au "whore".

Amandla...
 
Ndugu,

Kazi ya kuendesha nchi inatumia secret service kama nervous system inavyofanya kazi kwenye mwili wako. Hakuna kitu kinatokea mwilini bila central nervous system kushiriki. Kwa hiyo, kinachotokea Bungeni, Mahakamani, Gerezani na kwingineko kinaripotiwa sehemu moja kuu--ccordination point. Usiulize tena swali kama hili:nani aliemtoa Nusrat Hanje gerezani usiku kuwahi kiapo Dodoma asubuhi yake ?! It is a non-starter.
Naam [emoji111]
 

Bado nina shaka. Kuwa na screenshot ya barua ya Mnyika sio uthibitisho kuwa ulichoandika ni kweli. Inawezekana ikawa ni kweli lakini mimi bado ninatia shaka. Inawezekana ikawa wewe ndie uliyeiandika, lakini bado nitatia shaka mpaka siku ikithibitishwa na waliopelekewa hiyo rufaa. Lakini hautapita muda mrefu ukweli utajulikana na Baraza litaamua litakaloamua. Mimi binafsi sijuiukweli uko wapi.

Amandla...
 
Back
Top Bottom