Rufaa ya kina Mdee mbele ya Baraza Kuu dhidi ya Kamati Kuu CHADEMA: Kicheko kwa G19, Kilio kwa kina Mbowe

Licha ya kudumu kwenye tasnia ya habari kwa muda mrefu mpka leo hii hujajua sehemu sahihi za kupata habari za uhakika na wewe unaokota screenshot???

Shame on you Pascal njaaa
Huyo ndiyo maana aliingizwa cha kike na Kigogo juu ya msamaha feki kwa yule chinga aliyeshindwa kusoma kiapo.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Ukienda mahakamani kabla ya ku-exhaust internal remedial options inapoteza kesi mwanzoni kabisa via PO's.
Sasa kwa madai ya huyo muhusika kuna mashiko yapi yatakayoshawishi wasikiliza rufaa kupindua maamuzi ya kamti kuu?Mfano ushahidi wa wao kuapishwa Dodoma wataupindua vipi?

Aliyetakiwa kuwapa taarifa kwamba wameteuliwa kuwa wabunge ni nani? Kama ni katibu mkuu,je Ni yeye aliyewataarifu na wana ushahidi?
 
Aliyetakiwa kuwapa taarifa kwamba wameteuliwa kuwa wabunge ni nani? Kama ni katibu mkuu,je Ni yeye aliyewataarifu na wana ushahidi?
Katibu Mkuui hahusiki.
Naye anasikia kwenye media kama walioteuliwa.
Kazi yake ni kupeleka orodha NEC na kurudi ofisini akisubiri tangazo.
 
Bandiko linaongelea mawili: Umuhimu wa Baraza kuu kusimamia

1. Substantive justice
2. Procedural justice

Kuweka precedence nzuri kwa chama ni jukumu la Baraza Kuu.
Summary yako sijui ina maana gani maana haya mambo ni obvious Halima kwa kushirikiana na Tume and Ndugai anaelewa fika agenda yake hivyo bullet 1 and 2 are vaporous.
Mama Amon sometimes human being common sense must prevail.
 
Summary yako sijui ina maana gani maana haya mambo ni obvious Halima kwa kushirikiana na Tume and Ndugai anaelewa fika agenda yake hivyo bullet 1 and 2 are vaporous.
Mama Amon sometimes human being common sense must prevail.
Ndugu yangu, mie nimeripoti yale niliyoambiwa.
Karibu tuyajadili kulingana na Katiba, Kanuni na Taratibu za Chadema zilizo kwenye karatasi.
Lakini pia, kwa kutumia common sense kama unavyopendekeza.
 
Unawadharau waandishi wa aina hii hapa chini sio?

View attachment 1662699

Nina shaka kuhusu uhalisia wa hii inayodaiwa kuwa ni rufaa ya waliofukuzwa kwenye chama cha CHADEMA. Kinachozidi kunifanya niitile shaka ni lugha ya kebehi kwa Mbowe ambayo imetumika kwenye kichwa cha habari ambayo sidhani kama wakina Halima Mdee wanaweza kuibariki. Katika sakata lote hili wamekuwa wakimzungumzia Mbowe kwa heshima kubwa na haiwezekeni mara hii waanze kumsimanga. Aidha, rufaa imeandikwa kama inaenda Mahakamani ambako hayo mambo ya procedural justice yanaweza kupewa uzito tofauti na kwenye Baraza ambalo wengi sio wana sheria na wanachotaka kujua ni kwa nini walikiuka wito wa Chama na nani alishirikiana nao hadi kutimiza lengo lao. Kwa kifupi, waliendaje bila baraka za chama chao na kama walipata baraka ni nani katika chama alitoa hizo baraka. Hayo mengine ya mbona hatukuambiwa makosa yetu hayana tija mbele ya Baraza la waliokuwa wanachama wenzao. Hasa kwa vile wengi wao bado wanauguza majeraha waliyoyapata kwenye uchaguzi uliopita. Wanachotaka kujua ni inakuaje viongozi walioamini kuwa ni wafia chama wenzao wageuke kuwa ni "wasiliti" wa chama ambacho wamekipigania kwa kiasi cha kukubali kufungwa, kupigwa na manyanyaso mengine kwa ajili yake? Wasipojibu hili kwa kisingizio kuwa hawakuulizwa itawathibiishia wajumbe kuwa hawajutii kilichotokea na nia yao ni kuwa wabunge kwa gharama yoyote ile, hata kama italeta mpasuko mkubwa kwenye chama ambacho wanadai wana mapenzi nacho. Kwa vile sidhani kama lengo lao ni kukivuruga chama walichokipigania kiasi kile ndio maana natilishia shaka uhalisia wa kilicholetwa humu maana nia yake ni kuhakikisha kuwa rufaa yao itatupwa mbali na kuondoa kabisa uwezekano wa wao kurudi kwenye chama chao cha awali. Wote tunajua ni upande upi utakaofaidika na hali hiyo.

Amandla...
 
TISs chini ya Diwani ovyo tu

Upuuzi gani huu
 
CHADEMA wasimamie msimamo wao sisi wafuasi tuendelee kuwaamini, ama wakubali hao wa mama waende bungeni tuwatose mazima. Kwa sasa chadema inabidi iangalie faida za muda mrefu kuwatosa hao wanawake, ama wawakubali wapoteze ushawishi kwetu wafuasi wao
Siku chadema wakifanya upuuzi tutawatosa
 

Bado una mashaka?
 
Nakubaliana na ulilolisema kuwa kuna haja ya kuheshimiana lakini iwe kwa wote sio wanawake peke yao. Aidha, kuna tofauti kati ya "bitch" na "whore". Sio lazima "bitch" ajiuze. Lakini ukweli unabaki kuwa sio vizuri kumuita mwenzako "bitch" au "whore".

Amandla...
 
Naam [emoji111]
 

Bado nina shaka. Kuwa na screenshot ya barua ya Mnyika sio uthibitisho kuwa ulichoandika ni kweli. Inawezekana ikawa ni kweli lakini mimi bado ninatia shaka. Inawezekana ikawa wewe ndie uliyeiandika, lakini bado nitatia shaka mpaka siku ikithibitishwa na waliopelekewa hiyo rufaa. Lakini hautapita muda mrefu ukweli utajulikana na Baraza litaamua litakaloamua. Mimi binafsi sijuiukweli uko wapi.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…