Prosper Habona Eliti
Member
- Apr 8, 2016
- 7
- 3
Mungu ndiye ajuaye siri hii, Katika Mwanzo 2:7 Biblia inasema, "Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. " Pia katika Yohana 6:63, "Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu ..." Vilevile katika Kumbukumbu 29:29, "Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele ..."
Ukisoma maandiko hayo vizuri utaona mambo yafuatayo:-
1. Mungu ndiye aliyempulizia mwanadamu pumzi ya uhai (Roho) puani.
2. Ni kweli kabisa kuwa roho ndio inayoutia uzima mwili.
3. Sehemu ambayo roho ya mwanadamu hukaa, ni siri ya Mungu mwenyewe, na kwa kuwa Mungu hajaamua kutufunulia; hivyo yatupasa tumwachie yeye mwenyewe. Na hii ndio sababu ya KUFELI kwa majaribio yote ya kisayansi yahusuyo kuchunguza roho ya mwanadamu sehemu ilipo ndani ya mwili wa binadamu, au namna kuitengeneza ili waweze na wao kuumba [maana mpaka sasa wameweza kuumba maroboti (watu wasio na roho ndani)].
Hivyo ndugu, kwa sasa kitu cha muhimu zaidi kwako, sio kujua mahali ambapo roho yako ilipo ndani ya mwili wako; bali cha muhimu zaidi unapaswa ujue roho yako itakwenda wapi baada ya muda wa uhai aliokupangia Mungu kuisha. Nakushauri, kama hujampa Yesu Kristo maisha yako, basi uamuzi wa busara kwako ni kumpa Yesu maisha yako uokoke (Warumi 10:9), ili siku ya mwisho roho yako isipotelee kwenye moto wa milele. Lakini kama tayari umeokoka, hongera kwa hilo, nakushauri tu uendelee kuishi maisha matakatifu, ili siku ya mwisho tuwe na sehemu kwenye uzima wa milele.
Mungu akubariki sana ndugu.