Ruge Mutahaba ndiye aliyeharibu tasnia ya uandishi habari hapa Tanzania

Hukunielewa nilichosema. Mimi nazungumzia zile media ethics nk. Wachana na habari zinahusu nini. Tanzania kuna mambo mengi ambayo yanafanyika ndivyo sivyo bila kulinda walaji kwa mfano watoto. Waandishi wamegeuka marketing officers na uchafu wa kila aina. Halafu unashishangaza kidogo... Hivi jambo kama linafanyika ndivyo sivyo Ulaya basi na sisi tulibariki?
 
Hukunielewa nilichosema. Mimi nazungumzia zile media ethics nk. Wachana na habari zinahusu nini. Tanzania kuna mambo mengi ambayo yanafanyika ndivyo sivyo bila kulinda walaji kwa mfano watoto.
Hizo Sheria zipo mfano kuna muda (watershed hours) matangazo ya pedi wakati wa asubuhi au dawa za nguvu za kiume au kamari hazitakiwi hilo lipo wazi ila kwenye Kamari Serikali inakula pesa kila mtu anavyopoteza; na Media zina njaa kwahio sponsor yoyote hata kama anatangaza mambo ya ajabu anaendelea (hilo ni kosa wala haliingiliani na mtangazaji bali chombo na njaa za vyombo vya habari)
Waandishi wamegeuka marketing officers na uchafu wa kila aina. Halafu unashishangaza kidogo...
Inategemea marketing officers kwenye jambo gani na wanamarket nini ? kama wewe unakula habari za ufugaji wa nyuki na jamaa muuza nyuki wadogo wa pale tabora ndio amefanikisha hizo habari wewe usikie basi you have to take the rough with the smooth (huyo mdau wa Tabora ndio amekuwezesha wewe kula unachopenda); ila kama ni matangazo potofu (kuna sheria za kumlinda mlaji zinaweza kuingia hapo) au ni kuhakikisha kunakuwa na Parental Guidance au kipindi fulani kirushwe mida ambayo watoto wamelala...
Hivi jambo kama linafanyika ndivyo sivyo Ulaya basi na sisi tulibariki?
Nimeongelea Ulaya kuonyesha kwamba hata kule sio Kosher sababu hata andiko linaonyesha kana kwamba Bongo ndio kuna aina fulani ya watoa habari (kumbe ni dunia nzima kutokana na barrier of entry imekuwa ndogo na every Shabani, Musa au Ali anaweza kurusha kitu chake (ila ndio hivyo kama unachotaka kipo popote basi una choice) kama hakipo unaweza kuleta andiko na kutafuta sponsor kikarushwa...
 
Inaonekana hujui maana ya media ethics wewe ndiyo maana unaandika haya. Na hilo hasa ndiyo analo-mention mwanzisha thread.
 
RUGE AMESEMWA NA KUSINGIZIWA KWA MENGI...
Kiongozi mmoja wa kidini aliwahi kunieleza kwamba,uliwahi kufanyika utafiti,ikagundulika Ruge ana madhara makubwa sana ktk mmomonyoko wa maadili ya vijana wa Kitanzania.

Hoja zao ni kwamba matamasha kama fiesta,yalikuwa yanaharibu vijana wengi nchi nzima. Yalikuwa yanaharibu vijana kimaadili kama kiafya kwa wengine kuambukizwa STDs kama gono,HIV nk..

RIP MWAMBA... HAKIKA ULIKUWA MUONGOZA NJIA..
 
Kwaio Mwijaku hawezi kufanya kazi BBC London Office akipata chaka ?
 
Kitenge siyo mchambuzi na sijaona akifanya uchambuzi au habari za uchunguzi.
Nimeona akifanya utangazaji kwenye michezo na usomaji wa taarifa ya habari akiwa ITV.
 
Superb analysis.
 
The end justifies the means, mwisho wa siku media ni franchise hivyo yule anayeweza kuvuta audience kubwa ndiye anayestahili nafasi regardless his/her level of education.
 

He was trying to survive and in deed he survived. The problem of other journalists is the lack of their own idenntity. The are among those in the crowd. They follow the crowd.
Whose problem is that? lack of your own identity? Tumuache Ruge apumzike salama. Huruma yake Mwenyezi Mungu, na toba aliyowahi kuifanya kwa makosa ya udhaifu wake wa kibinadamu, namuomba Mwenyezi Mungu, amrehemu na kumpa pumziko lenye amani.
 
Kuna combination ya sababu
1. Wenye media kuajiri vilaza
2. Serikali kushindwa kusimamia na kuongoza
3. Walaji kuwa na upeo mdogo na kutaka habari nyepesi.
Walaji wawe na upeo mdogo au la siyo issue, biashara inatakiwa iwavutie 'walaji' na yoyote anayewekeza kwenye media anapaswa kuliangalia hilo. It's a terribly stupid move uwekeze hela zako kwenye biashara ya habari halafu uajiri wanahabari ambao si 'likable'(wasio na uwasilishaji habari wenye mvuto) kwa majority ya 'walaji', your investment will definitely go down the drain.
Talent>Mavyeti.
 
Like hospital services, the main aim of the media is not profit. If you make profit your main objective, you are doomed to corrupt society. Infact ndicho tunachobishania hapa kwa sababu Tanzania media nyingi ni vijiwe vya tamaa ya kuingiza fedha za haraka haraka. Ndiyo maana media zimejaa machawa wasijua ethics za journalism ni nini.
 
Shida sio Ruge, Shida ni Serikali yako ndo inawalea hao wasio na taaluma ya uandishi. Kama serikali iko serious kweli bila kuangalia uchama waweke sheria kimaandishi na watu wachukuliwe hatua. Uone kama hiyo taaluma itachezewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…