RUGE tuamuangalie upande wa pili

RUGE tuamuangalie upande wa pili

Jeff bezzos CEO wa Amazon ndio tajiri namba moja duniani ana miaka 54 na yupo single na huyo ndio mfano wa kuigwa sasa kwenye jamii
Jeff alikuwa na ndoa kwa takribani miaka 25 iliyopita. Ametengana na mkewe mwaka huu. Ila alikuwa ameowa kabla hata hajaanzisha Amazon.
 
Steven foundries Apples 🍏
Edward Heath waziri mkuu wa Uingereza miaka ya 70
Steven Job alikuwa na familia. At least yeye ali-spend muda wake kwenye kufanya invention. Ingawa alipitia up and down nyingi, but hastahili kulinganishwa with crook like Edward Heath na wengineo wengi....
 
TheChoji Mimi nimekuelewa, lakini sidhani kama watu wengine watakuelewa.
Mtu kuwa Role mode na mfano wa Kuigwa sio lazima aoe aisee... Kuna watu wapo busy na maisha kiasi kwamba anaona famili kuishi nayo ni nomaa lakini pia Hatujui nini kilifanya yeye Binafsi asioee na kama wanawake zake pengine walifata Pesa zake na jina bhasi so Akaona isiwe shidaa nitalitumikia Taifa tu inatoshaa.. Mwanaume hata akifika miaak 70 kama Kapuya ili mradi pesa unayo unaoaa tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Eti jamaa wanamwita modal wao wakati hata familia tu hakuwa nayo, ukweli ni kuwa alikuwa anaishi kihuni full stop


Sent using Jamii Forums mobile app
Mtu kuwa kijana sio Umrii ni Pesa mkuu..[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Watu wanazeeka hata wakiwa na miaka 30 tayari wazee kabisa... Ila Wenye pesa miaka 55 kijana sana tuu yani sanaa..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyie wadamu kazi yenu imekwisha, mlikuwa na Ruge for 49 years, sasa muacheni maana yupo ndani ya mipaka ya Mungu, ambapo hamuhusiki na lolote huko alipo now.
Kama ni kweli acha waseme, hili la kuwaomba watoto wa kiume nyuma sio kabisa.
 
Ruge aliwekeza mda wake mwingi katika kutafta pesa na sio familiya
Kwa upande mmoja na Ukigeuza upandea wa pili aliwekeza kwenye anasa pia.Pumzika ulipojiandalia ukiwa hai bro Ruge sie tuliobaki hating maamuzi ya kuamua uende wapi.
 
Alikuwepo, hakuwa malaika, ila aliwawezesha wengi tu, alijituma kwenye fani yake zaidi ya 110%, alitunza watoto wake fresh kabisa, kuhusu kuoa ua la sidhani kama yanatuhusu hayo, yako "personal", mno, ni hiari ya mtu na siyo kulazimishana, kama aliwafyeka madada basi walitaka wenyewe na tamaa zao..
RIP Ruge, wote tutakuja huko pia, iwe tuwe na familia au la, au tuwe mfano wa jamii au vinginevyo...
Let him rest in peace please...
 
Sema mimi nashangaa jambo moja eti wanauita kijana? Kijana gani ana miaka 49?

Ndiyo!
Ni sahihi kabisa kwa umri huo kuitwa kijana hadi mtu atakapotimiza miaka 50 ujana unaisha na kuanza kuingia utu wa makamo na wala siyo uzee kama watoto wa siku hizi mnavyoita!

Hata ukienda angalia kanuni zetu za UVCCM kijana ni kama nikivyokwambia!

Muache kuzeesha watu wakati umri wao bado wadogo sana!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imeandikwa “ apataye mke apata kitu chema!
Tena apata jambo la kumpatia kibali!
Ni kheri kuwa wawili kuliko kuwa mmoja!

Mjadala huu uwe ni somo kwa sisi tulio hai tujirekebishe kwa yale mapungufu tuliyonayo!
Ni kheri kuoa kuliko kuwaka tamaa.
Ukiamua kutokuoa maana yake ukae kama ukivyo kama Mtume Paulo.
Lakini kama hujaoa na ukaishi maisha ya uzunzi basi fahamu kuwa ;

Maisha ya uzinifu ni machikizo machoni pa Mungu!

Ingawa kuna kuna watu watu wameoa na hawajatulia na wake zao , bado wanafanya uasherati tena imekuwa kawaida yao hiyo nayo inamchukiza Mungu!



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ni mtazamo duni sana. Yaani mtu ambaye anaishi bila kuoa au kuolewa anakua mhuni!!!!
Yesu hakuoa na Mtume Paulo wote hawa hawakuoa kwa sababu hiyo tuwaite wahuni? Si sawa.
Jiulize kwa nini wewe umeoa? Hayo mambo unayoyapata baada ya kuoa uwezi kuyapata ukiwa haujaoa...kama ni watoto Ruge Kawabata na kama ni burudani amekua akipata kama kawa.
Tofauti ni kwamba yeye aliamua kutofungamana na upande mmoja ambao ungemfanya awe mtumwa...[emoji2][emoji2]
Kwa hiyo ulitaka Mungu aoe "Yesu"

mvujajasho nguli
 
Back
Top Bottom