Ruhusa ya mikutano ya kisiasa ni pigo kwa vyama uchwara

Nzelu za bwino

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2020
Posts
400
Reaction score
484
Salaam wana jf.baada ya rais Dr Samia suluhu Hassan kutengua zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa ,nikama kufunga dirisha lakuingiza hewa Safi ndani ya taifa.

Nimeona watu wakifurahia sana Jambo hili si wana siasa tu hata wasiokua wanasiasa pia. Lakini kwa upande wa pili hili ni pigo kubwa sana kwa wanasiasa uchwara na vyama vyao, kwao hili nipigo kwakua hii nafasi inaenda kuonyesha rangi halisi ya vyama vyao.

~ Je, ni ipi ajenda yao kwa Watanzania?
~ Ni kwa kiasi gani wana kubalika na watanzania?
~ Ni maeneo gani wanayokubalika?
~ Ni kwanini yawe maeneo hayo tu?

Kupitia maswali na sababu hizo hapo juu naliona anguko la vyama uchwara vingi sana, maana kushawishi watu waache shughuli zao waje wahudhurie mikutano yako ya hadhara sio jambo dogo kwenye siasa; na hicho ndio kipimo halisi cha namna unavyokubalika na jammii.

Nawatakia kila la kheri ya Mwaka Mpya 2023 wenye mambo mapya ya kisiasa na maendeleo.

Ni vyama vipi unaona vinaweza kuwa vya kwanza kupotea kwenye ulingo wa siasa?

Nawasiliana.
 
Hakuna cha maana kitakachopatikana kwa kuruhusu kampeni zisizokwisha. Kuruhusu mikutano ya vyama vya upinzani ni sawa na kuruhusu kampeni zisizokwisha.

Chama tawala kitajikuta kinapoteza muda wa kutawala na kutekeleza ilani yake kulumbana na watu ambao hawakuchaguliwa.
 
Lakini kwa upande wa pili hili ni pigo kubwa sana kwa wanasiasa uchwara na vyama vyao,
Naunga mkono hoja haswa kwa kuzingatia Tanzania tuna chama kweli cha siasa ni kimoja tuu ambapo pia ni chama dola, CCM, kimezingukwa na vyama uchwala 4, Chadema, ACT Wazalendo, NCCR Mageuzi na CUF, na vyama makapuku 14 ambayo vipo tuu kwenye daftari la Msajili lakini havina ofisi, havina diwani, wala mbunge hata mmoja na havipati Suzuki hata senti moja!.

Kiukweli JPM sio tuu aliinyoosha nchi... Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani Makini? - Prof. Kitila Mkumbo na Upinzani wa Tanzania ni Upinzani Makini wa Kweli, au ni Upinzani Uchwala?. Kasi ya JPM Itaua Upinzani Uchwala na Kuibua Upinzani Makini wa Kweli Au..? na
The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja na Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?
P
 
Vyama ambavyo vitapata mwitikio chanya toka kwa wananchi ni vile vyama vitakavyokuja na majibu sahihi na njia sahihi za utatuzi wa changamoto zinazoikabili jamii yetu kwa sasa:

-UKOSEFU WA AJIRA

-KUPANDA MNO KWA GHARAMA ZA MAISHA

-KUPANDA MNO KWA GHARAMA ZA MIKOPO YA MABANK

-ELIMU YETU KUENDELEA KUWA DUNI

-KUTOPANDA KWA MISHAHARA YA WATUMISHI

-KUKOSEKANA KWA UMEME WA UHAKIKA

-KUWEPO KWA UPIGAJI NA UFUJAJI WA HELA ZA SERIKALI

-VIONGOZI KUWA MIUNGU WATU

-UKIUKAJI NA UVUNJWAJI WA KATIBA NK.
 
ACT na wenzake wameshapotea.

Chadema wata ng'aa kama wataheshimu na kuenzi kazi za hayati Magufuli.

Kinyume na hapo watapotea infinity.

Zingatia maneno yangu.
Lakini ngumu kumeza hiyo ila kupotea?! Mmhh ! Nakumbuka pale mwanzoni mwa utawala wa marehemu Magufuli Chadema walisema Magufuli anafuata sera za Chadema !
 
Hakuna cha maana kitakachopatikana kwa kuruhusu kampeni zisizokwisha. Kuruhusu mikutano ya vyama vya upinzani ni sawa na kuruhusu kampeni zisizokwisha.

Chama tawala kitajikuta kinapoteza muda wa kutawala na kutekeleza ilani yake kulumbana na watu ambao hawakuchaguliwa.

Mbona mikutano haipo miaka saba na Deni la taifa limefika Trilioni 92, mfumuko wa Bei, ajira hakuna, nk
 
Shaka na Chongolo nao wanatekeleza ilani ya chama??
Hakuna cha maana kitakachopatikana kwa kuruhusu kampeni zisizokwisha. Kuruhusu mikutano ya vyama vya upinzani ni sawa na kuruhusu kampeni zisizokwisha.

Chama tawala kitajikuta kinapoteza muda wa kutawala na kutekeleza ilani yake kulumbana na watu ambao hawakuchaguliwa.
 
Naunga mkono hoja haswa kwa kuzingatia Tanzania tuna chama kweli cha siasa ni kimoja tuu ambapo pia ni chama dola, CCM, kimezingukwa na vyama uchwala 4, Chadema, ACT Wazalendo, NCCR Mageuzi na CUF, na vyama makapuku 14 ambayo vipo tuu kwenye daftari la Msajili lakini havina ofisi, havina diwani, wala mbunge hata mmoja na havipati Suzuki hata senti moja!.

Kiukweli JPM sio tuu aliinyoosha nchi... Je, Kasi ya Magufuli itaua Upinzani Uchwara na Kuimarisha Upinzani Makini? - Prof. Kitila Mkumbo na Upinzani wa Tanzania ni Upinzani Makini wa Kweli, au ni Upinzani Uchwala?. Kasi ya JPM Itaua Upinzani Uchwala na Kuibua Upinzani Makini wa Kweli Au..? na
The Economist: Rais Magufuli ametangaza kufuta Upinzani ifikapo 2020 na kuirudisha Tanzania kuwa Nchi ya chama Kimoja na Wanaohamia CCM wasibezwe! Wanaona mbali, 2020 Majimbo yote kurejeshwa. Je, tunarejea nchi ya chama kimoja?
P

Sio uchwala ni uchwara. Unajifanya kuidharau CHADEMA lakini ndio chama kilichoshambuliwa na mahakama, bunge na serikali. Katafute sababu za Mikutano kuzuiliwa ndio ulete dharau zako hapa. Wewe uwezo wa kukonvince wajumbe huna unaambulia kura moja, ila dharau zimekujaa.

Vingekuwa vyama uchwara mikutano isingepigwa marufuku. Hiyo CCM unayoiabudu Ina lipi la maaana. Mfumuko wa Bei, Hali ngumu ya kiuchumi, rushwa, Deni la njee kuongezeka, nk. Punguza dharau
 
Lakini ngumu kumeza hiyo ila kupotea?! Mmhh ! Nakumbuka pale mwanzoni mwa utawala wa marehemu Magufuli Chadema walisema Magufuli anafuata sera za Chadema !

Ni kweli alichukua sera za CHADEMA na kuzifanyia kazi. Kama elimu bure, madini etc
 
Hizo zote ni sera za CCM. Pakua na usome ilani ya CCM ya 2015-2020.

Tena Magufuli mzee wa kanda ya ziwa, Geita kwenye dhahabu unadhani anahitaji kufundishwa na CHADEMA kuhusu sera ya madini?

CHADEMA wao ndo walitisha kwa kumsimamisha Lowassa, ambaye walishamtangaza katika List of Shame kuwa ni fisadi, kugombea uraisi.
 
Mbona mikutano haipo miaka saba na Deni la taifa limefika Trilioni 92, mfumuko wa Bei, ajira hakuna, nk
Pitia hii video utaelewa zaidi.

Mfumo wa pesa za kutoka hewani ndo unasababisha hayo. Pesa za hewani zina shida moja, kila noti inayochapishwa ni deni. Noti ya Tshs. 10,000/- ni deni la Tshs. 10,000/-.

Ni mpaka tutakapoamua kutumia pesa za asili ndo tutamaliza deni la taifa na mfumuko wa bei.
 
Hizo zote ni sera za CCM. Pakua na usome ilani ya CCM ya 2015-2020.

Tena Magufuli mzee wa kanda ya ziwa, Geita kwenye dhahabu unadhani anahitaji kufundishwa na CHADEMA kuhusu sera ya madini?

CHADEMA wao ndo walitisha kwa kumsimamisha Lowassa, ambaye walishamtangaza katika List of Shame kuwa ni fisadi, kugombea uraisi.

Acha uongo, CHADEMA ndio walikuwa na ajenda ya Elimu bure kuanzia primar mpaka chuo kikuu. Tena kipindi Cha kampeni wana CCM walipinga Sana hili, CHADEMA waliahidi kumtoa babu seya, nashangaa CCM walipinga Sana. Ila walipoingia Magufuli akawatoa. Magufuli alifanya hivyo ili kuwanyima CHADEMA Cha kuongea.

Pia kuhusu lowassa, kwa Sasa amerudi CCM kwenye mafisadi Wenzake, asingeweza kukaa CHADEMA. Mshughulikieni humo CCM Kama mnaweza.
 
Pitia hii video utaelewa zaidi.

Mfumo wa pesa za kutoka hewani ndo unasababisha hayo. Pesa za hewani zina shida moja, kila noti inayochapishwa ni deni. Noti ya Tshs. 10,000/- ni deni la Tshs. 10,000/-.

Ni mpaka tutakapoamua kutumia pesa za asili ndo tutamaliza deni la taifa na mfumuko wa bei.

Video ya Nini?. Acheni kukopa hovyo. Miaka nenda rundi CCM ni kukopa kwa mabeberu.
 
Pia kuhusu lowassa, kwa Sasa amerudi CCM kwenye mafisadi Wenzake, asingeweza kukaa CHADEMA. Mshughulikieni humo CCM Kama mnaweza.
Lowassa kuondoka CHADEMA ni aibu kubwa sana kwa CHADEMA. Yaani amewafanya kama kademu ka kukojolea tu. Kaja kawalambisha matapishi yenu halafu huyo akasepa.
 
Back
Top Bottom