Rukwa: Wanafunzi waliofukuzwa shule kisa wazazi wao kuwa CHADEMA, warudishwa shuleni

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Saa chache tangu taarifa ya kufukuzwa shule kwa wanafunzi 14 wa Shule ya Msingi Izinga kwa madai ya wazazi wao kukiunga mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nkasi, Afraha Hassan amesema waliokumbwa na kadhia hiyo walikuwa tisa na tayari wamewarudisha.

Taarifa hiyo ya Mkurugenzi imetolewa leo Alhamisi Desemba 5, 2024, imesema wamebaini mwalimu mkuu aliwasimamisha shule wanafunzi hao na kuwataka wazazi watafute shule nyingine na siyo kufukuzwa shule kama ilivyoripotiwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

“Uamuzi wa kuwasimamisha wanafunzi hao haukufuata utaratibu wa miongozo ya wizara. Aidha wanafunzi waliosimamishwa shule hawakuwa na kosa lolote la kinidhamu,” amesema.

Akitaja hatua walizochukua Hassan amesema: “Wanafunzi wote tisa (9) waliosimamishwa shule wamerejeshwa shuleni bila masharti yoyote. Hatua za kiutawala na uongozi dhidi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo zitachukuliwa pindi uchunguzi unaoendelea utapokamilika.”

Mapema leo asubuhi, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda aliagiza timu ya wataalamu udhibiti ubora kwenda kuchunguza taarifa ya wanafunzi 14 wa Shule ya Msingi Izinga, iliyopo Nkasi Kusini kufukuzwa shule kwa madai ya wazazi wao kuiunga mkono Chadema kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.
Your browser is not able to display this video.
Pia, Soma:
 
Hii Nchi unaweza kudhani haipo duniani, Yaani ni Nchi iliyojaa Ujinga usiomithilika.

Hebu soma hii



Yanayofanyika yamemfanya hata Mwovu Shetani kushika kiuno kwa mshangao.

Nashauri Wazazi wa watoto wawahamishe shule hiyo na naiagiza Chadema Kanda ya Nyasa kusimamia mchakato huo haraka, Iko siku Watoto wa Wanachama wa Chadema watapewa Sumu kwenye Chakula cha shule hiyo.
 
Nchi ngumu sana hii 😔 🚮🚮
 
Mwalimu mkuu na maamuzi ya kipimbavu, ime ku cost kazi, now unarudi kitaa kwa mihemko
 
Baadae unashangaa mbona vijana wanatoka shuleni weupe kumbe wanafundishwa na walimu wasio na ubongo wa fikrankabisa. N huyu ni mwalimu mkuu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Baadae unashangaa mbona vijana wanatoka shuleni weupe kumbe wanafundishwa na walimu wasio na ubongo wa fikrankabisa. N huyu ni mwalimu mkuu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Elimu yetu iko hatarini. kuwa mwalimu itabidi a bar iwe raised juu sana.
Otherwise kama hawa ndio walimu, future ya nchi iko at risk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…