Rukwa: Wanafunzi waliofukuzwa shule kisa wazazi wao kuwa CHADEMA, warudishwa shuleni

Rukwa: Wanafunzi waliofukuzwa shule kisa wazazi wao kuwa CHADEMA, warudishwa shuleni

Wamemwaga mboga tu mwage ugali
Hiyo haifai ndugu yangu, tusitengeneze jamii yenye kuchukiana kwa sababu ya itikadi za kisasa. Huyu anataka kutuletea aina hii ya siasa anatakiwa kukemewa kwa nguvu zote. Siasa ni sera tu na tuifanye kama burudani tuzipatazo kwenye timu za Kariakoo (kushinda ama kushindwa hakuondoi urafiki na undugu)
 
Walimu wengi wa hii nchi ni kikwazo cha Maendeleo! Siwapendi !
Kikwazo wakati ndio walio kufundisha !? Wewe pia ni kikwazo maana hujui unacho ongea , mwalimu hakusanyi kodi sasa anakwamishaje maendeleo unaufahamu mzuri wa mambo kweli wewe!
 
Hii Nchi unaweza kudhani haipo duniani, Yaani ni Nchi iliyojaa Ujinga usiomithilika.

Hebu soma hii

View attachment 3169651View attachment 3169653

Yanayofanyika yamemfanya hata Mwovu Shetani kushika kiuno kwa mshangao.

Nashauri Wazazi wa watoto wawahamishe shule hiyo na naiagiza Chadema Kanda ya Nyasa kusimamia mchakato huo haraka, Iko siku Watoto wa Wanachama wa Chadema watapewa Sumu kwenye Chakula cha shule hiyo.
Napendekeza Mwalimu mkuu huyo na DC aliyemtuma kufanya upumbavu huo wote waadhibiwe na wahamishwe huko kwani chuki waliyoonyesha ni kubwa na watakuwa na visasi na watoto hao.
 
Wawafukuze tu. Raia tungejichanga na kuwasomesha shule nzuri zaidi. Kenge nyie ccm
 
Uchunguzi upi sasa? Shule walisimamishwa, sababu mkaijua, mkaona haina mashiko, mkawarudisha sasa huo uchunguzi ni upi unaohitajika ili kuchukua hatua za kinidhamu kwa hao walimu?
 
Saa chache tangu taarifa ya kufukuzwa shule kwa wanafunzi 14 wa Shule ya Msingi Izinga kwa madai ya wazazi wao kukiunga mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nkasi, Afraha Hassan amesema waliokumbwa na kadhia hiyo walikuwa tisa na tayari wamewarudisha.

Taarifa hiyo ya Mkurugenzi imetolewa leo Alhamisi Desemba 5, 2024, imesema wamebaini mwalimu mkuu aliwasimamisha shule wanafunzi hao na kuwataka wazazi watafute shule nyingine na siyo kufukuzwa shule kama ilivyoripotiwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

“Uamuzi wa kuwasimamisha wanafunzi hao haukufuata utaratibu wa miongozo ya wizara. Aidha wanafunzi waliosimamishwa shule hawakuwa na kosa lolote la kinidhamu,” amesema.

Akitaja hatua walizochukua Hassan amesema: “Wanafunzi wote tisa (9) waliosimamishwa shule wamerejeshwa shuleni bila masharti yoyote. Hatua za kiutawala na uongozi dhidi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo zitachukuliwa pindi uchunguzi unaoendelea utapokamilika.”

Mapema leo asubuhi, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda aliagiza timu ya wataalamu udhibiti ubora kwenda kuchunguza taarifa ya wanafunzi 14 wa Shule ya Msingi Izinga, iliyopo Nkasi Kusini kufukuzwa shule kwa madai ya wazazi wao kuiunga mkono Chadema kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.
Pia, Soma:
Kuwasimamisha na kuwaambia watafute shule nyingine si ndio kuwafukuza huko?
 
Huyo fara sasa huko sindiyo kufukuzwa shule ?
 
Napendekeza Mwalimu mkuu huyo na DC aliyemtuma kufanya upumbavu huo wote waadhibiwe na wahamishwe huko kwani chuki waliyoonyesha ni kubwa na watakuwa na visasi na watoto hao.
Hao wanatakiwa kufutwa kabisa kwenye serikali na siasa wasiruhusiwe kuwa wanasiasa wala wafanyakazi wa serikali....
 
Yaani TANZANIA hapa tumefika sasa sio pazuri kabisa tunauana Kila siku kisa ni siasa... Leo tena unaskia wanafunzi wamefukuzwa Kwa sababu wazazi wao ni CADEMA inasikitisha sana na inaogopesha na pia inaleta picha mbaya sana ya kule tunapoelekea kama nchi yaani viongozi wengi wa serikali wamekuwa mazombi serikali imekuwa kama Haina kichwa ...

Kikubwa ninachotaka nishauri hapa ni kuwaambia watawala yaani hwa vegetables wajitathini sana waheshimu katiba ya nchi wasivunje Sheria Kwa mabavu ya utawala huo ni upimbi na kukosa uzalendo wa kweli kwenye nchi Yako
 
Shida siyo mwalimu mkuu, shida ni mifumo ya utawala, jueni kwamba mwalimu ni mwajiriwa wa serikali. Kwa mfumo huu mkurugenzi ndio mwajiri, hivyo automatically mwalimu huyo hawezi kwenda kinyume na mwajiri wake ukizingatia haya utaona kwamba mkurugenzi anaweza kutoa maigizo hata kama yapo kinyume na Sheria atataka yatekelezwe na mwalimu hatoweza kuyapinga. Ukweli ni kwamba hata walimu Hawaipendi CCM nao wanahitaji kukombolewa kutoka kwenye makucha ya watawala
 
Wanatuona wajinga huyo mwalimu hatukumuajiri kwa ajili ya siasa ila kufundisha wanafunzi tu hajaajiriwa na ccm bali serikali/wanainchi walipakodi sio kuisemea cdm au ccm hio sio sahihi inatakiwa atuachie ofisi yetu
 
Samia ukimuona unaweza sema sio yeye anayefanya huu ujinga
 
Back
Top Bottom