Rukwa: Wanafunzi waliofukuzwa shule kisa wazazi wao kuwa CHADEMA, warudishwa shuleni

Rukwa: Wanafunzi waliofukuzwa shule kisa wazazi wao kuwa CHADEMA, warudishwa shuleni

Hapa haijanyooka. Huku taarifa inatuonesha kuwa mwalimu kakosea. Halafu kuna uchunguzi unaendelea. Mbona sasa ipo kama kesi ishahukumiwa? Ndiyo presha ya umma nini?

Muwafundishe makada wawe wanajipanga kabla hawajapiga tukio.
 
Anarudi kitaa kivipi...?? Haiko ivo ndg sana sana watamhamisha tu??? Wakiona vip.. vipi watakitoa cheo cha mwl mkuu... yupo ajirani huyoioo
 
Samia ukimuona unaweza sema sio yeye anayefanya huu ujinga
Nyinyi wapumbavu si mlinibishia nilipo wa ambia ...yote niliyo waambia kuhusu samia bushiri na wahuni wenzake yanatimia .....tz hakuna wapinzani wa kisiasa bali kuna kundi la wahuni wanao jinasibu kuwa wapinzani ...
 
Ki uhalisia ni kuwa .wazazi ndio walitengwa..Tunaanza baguana kidogo kidogo mwisho inakuwa sera ya nchi baadae 1994Rwanda
 
Aiseee bado tunasafari ndefu sana.ukweli ni kwamba walimu wanatumika vibaya sana
 
Hii Nchi unaweza kudhani haipo duniani, Yaani ni Nchi iliyojaa Ujinga usiomithilika.

Hebu soma hii

View attachment 3169651View attachment 3169653

Yanayofanyika yamemfanya hata Mwovu Shetani kushika kiuno kwa mshangao.

Nashauri Wazazi wa watoto wawahamishe shule hiyo na naiagiza Chadema Kanda ya Nyasa kusimamia mchakato huo haraka, Iko siku Watoto wa Wanachama wa Chadema watapewa Sumu kwenye Chakula cha shule hiyo.
Hii haijaa kama sawa
 
Sasa ni Zamu ya kuwafukuza walio wafukuza wanafunzi hao.
 
Wanataka kuleta mambo ya Zanzibar, kule wakikugundua ni mpinzani sahau kuhusu kuajiriwa na SMZ Kuna vijana wanateseka sana kule kisa itikadi za kisiasa za wazazi wao
Inasikitisha sana
 
Elimu yetu iko hatarini. kuwa mwalimu itabidi a bar iwe raised juu sana.
Otherwise kama hawa ndio walimu, future ya nchi iko at risk
Kuhukumu kwa kusikiliza upande mmoja nao ni ujinga mkubwa sana nimesoma barua ya mwl mkuu nasubiri nisikie walicho sema hao wazazi wa hao watoto ili nipate cha kuchangia
 
Hiyo haifai ndugu yangu, tusitengeneze jamii yenye kuchukiana kwa sababu ya itikadi za kisasa. Huyu anataka kutuletea aina hii ya siasa anatakiwa kukemewa kwa nguvu zote. Siasa ni sera tu na tuifanye kama burudani tuzipatazo kwenye timu za Kariakoo (kushinda ama kushindwa hakuondoi urafiki na undugu)
Hiyo maneno anza kuishauri serikali inayo teka wapinzani
 
Jamaa anazidi kuwafanya walimu waonekane hamnazo
 
Hii Nchi unaweza kudhani haipo duniani, Yaani ni Nchi iliyojaa Ujinga usiomithilika.

Hebu soma hii

View attachment 3169651View attachment 3169653

Yanayofanyika yamemfanya hata Mwovu Shetani kushika kiuno kwa mshangao.

Nashauri Wazazi wa watoto wawahamishe shule hiyo na naiagiza Chadema Kanda ya Nyasa kusimamia mchakato huo haraka, Iko siku Watoto wa Wanachama wa Chadema watapewa Sumu kwenye Chakula cha shule hiyo.
Tatizo la kuendekeza uccm na uchawa. Na bado, huko tunakoelekea tutazalisha intarahamwe. Leo hii, viongozi wanakosa ubunifu na namna bora ya kimuhudumia Mtanzania badala yake, wakurugenzi, MaDAS, ma DC, MaRAS na MaRC wote akili zao zimejikita kuhakikisha namna CCM ina shinda Kwa kishindo maeneo yao. Na hicho eti ndo kipimo Cha kuonekana anatenda kazi Ili ateuliwe tena. Very pathetic.

Na hayo yaliyo fanywa na mwalimu huyo asiye na elimu ni MATOKEO ya maelekezo, mipango na hujuma zinazofanywa na wakurugenzi, DAS, DC, RAS hadi maRC.

What a shameful and disgusting state our country has reached!!!!!!!!!!!
 
Walimu wapo mabarabarani na madishi ya nyanya huyo anaweza akawa utauweza uwalimu kweli. Jiandae mwezi ujao uanze kazi.
 
Saa chache tangu taarifa ya kufukuzwa shule kwa wanafunzi 14 wa Shule ya Msingi Izinga kwa madai ya wazazi wao kukiunga mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Nkasi, Afraha Hassan amesema waliokumbwa na kadhia hiyo walikuwa tisa na tayari wamewarudisha.

Taarifa hiyo ya Mkurugenzi imetolewa leo Alhamisi Desemba 5, 2024, imesema wamebaini mwalimu mkuu aliwasimamisha shule wanafunzi hao na kuwataka wazazi watafute shule nyingine na siyo kufukuzwa shule kama ilivyoripotiwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

“Uamuzi wa kuwasimamisha wanafunzi hao haukufuata utaratibu wa miongozo ya wizara. Aidha wanafunzi waliosimamishwa shule hawakuwa na kosa lolote la kinidhamu,” amesema.

Akitaja hatua walizochukua Hassan amesema: “Wanafunzi wote tisa (9) waliosimamishwa shule wamerejeshwa shuleni bila masharti yoyote. Hatua za kiutawala na uongozi dhidi ya mwalimu mkuu wa shule hiyo zitachukuliwa pindi uchunguzi unaoendelea utapokamilika.”

Mapema leo asubuhi, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda aliagiza timu ya wataalamu udhibiti ubora kwenda kuchunguza taarifa ya wanafunzi 14 wa Shule ya Msingi Izinga, iliyopo Nkasi Kusini kufukuzwa shule kwa madai ya wazazi wao kuiunga mkono Chadema kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.
Pia, Soma:
Wazazi wasingelalamika humu walah ndo ingekuwa imetoka hiyo.

Mkuu wa Wilaya naye achunguzwe maana kimya chake kwenye hili ni jibu tosha la uhusika wake
 
Back
Top Bottom