Rushwa haina madhara yoyote ya maana kwa maendeleo ya nchi

San Abacha alikuwa Rais wa Nigeria. Alikuwa corrupt balaa. Aliiba karibu dola bilioni 5. Akatorosha pesa na kwenda kuwekeza Ulaya, leo hata hazijulikani ziliko. Mtoto wa Nguema ni corrupt san. Pesa ameenda kuwekeza Ulaya na Marekani.

Huyo Abacha au Nguema angewekeza hizo pesa nchini mwake ingeboost sana uchumi. Utoroshaji pesa ndiyo adui mkubwa kuliko rushwa na ufisadi. Tuwe na kampeni ya kupambana na utoroshaji pesa, kam tulivyo na kampeni za kupambana na rushwa.
 
Mwanao utakapo mleta shuleni tutahitaji utupe rushwa ya laki tano ndipo tumpokee
Mbona hii ipo sana. Nenda shule za serikali ambazo ni english medium.
 
hapa tumegusia mahakama,ambayo ni msingi wa kutoa haki ikiwemo business legal cases. Mwekezaji gani atakuja kwenye corrupt
wawekezaji wanaangalia faida. Tena wanapenda sana nchi zenye rushwa, hasa kama kuna bidhaa ina faida kubwa kama madini, mafuta, mazao ya misitu etc.
 
Tumia akili.hayo madeni yanalipwa Kwa kutumia Kodi ya watanzania.
Mimi ninachosema tule kwa urefu wa kamba zetu sio mpaka tuvimbiwe, kama mawaziri wameambia wajipimie na kila mtu akijipimia maisha yataenda...
 
Kupitia rushwa,hata watu wasio qualify,wanapata fursa!We fikiri wapanga maendeleo ya nchi wanakuwa vilaza kisa tu wamepata nafasi hizo Kwa rushwa!
Nchi zilizoendea kazi za sekta binafsi ndio nzuri zaidi, zenye kulipa vizuri na maslahi zaidi na ndizo zinasakwa zaidi na watu smart kuliko za serikali. Hapa kwetu udumavu wa sekta binafsi ndio inasababisha watu watoe rushwa na nepotism kupata ajira serikalini.
 
Uko sahihi mkuu kwa 90% japo wengi watakupinga.
 
Mimi ninamwelewa mtoa uzi, unajua mawazirii wameambiwa wale kwa urefu wa kamba zao, wasizidishe kwani wakizidisha wataharibu, polisi nae vivyo hivyo na watoa huduma kadhalika lakini watumie fedha hapa nchini wasiende kuzificha benki za Uswiss hapo uchumi utaendelea. Kama polisi akipokea Kita kisha akaenda kununua bodaboda akampa mtoto wa kaka yake huoni ametoa nafasi ya kazi kwa mtu mmoja. Au akijenga nyumba huoni mafundi kadhaa wamepata kazi ... ndio hivyo!
 
Kama yule askari
 
Utakapo hitaji kitu muhimu au huduma muhimu ambayo ni haki yako afu uulizwe umejipangaje . Ndo utakapo elewa
Mojawapo ya nchi yenye viwango vikubwa vya rushwa kubwa duniani ni Urusi ila bado ni mojawapo ya nchi kumi tajiri duniani ambazo wananchi wake wengi wana maisha mazuri ya maendeleo makubwa na raha mustarehe.
 
Russia ni mojawapo ya mataifa yenye viwango vikubwa vya Rushwa duniani ila bado ni Taifa Tajiri na lenye maendeleo makubwa sana.
 
Tufanye serikali inakopa trillions 6 kwa ajili ya barabara ya dar mpaka dodoma halafu mkandarasi ana jenga ya bajeti ya trillion moja baada ya miaka mitatu inaharibika unaenda kukopa tena ukarabati barabara ile ile iliyojengwa chini ya kiwango hapo si kutiana umasikini mkuu.

Kitu kimoja kinakopewa hela mara tatu na bado hakina ubora halafu unasema rushwa haina madhara we utakuwa askari bila shaka.
 
Mbona hata kununua bidhaa nje ya nchi NI sawa na kutorosha pesa nje...labda kabla ya masuala ya rushwa tupige Vita uagizwaji wa ndege,madawa,magari,n.k ili pesa zibaki hapa tu kuzunguka nchini [emoji1787][emoji1787]
Hawana huo ubavu vyoo tu wameshindwa kujenga leo hii ndege na madawa subutuu
 
Duuuh,kweli akili zetu zimechoka!Sioni shida kama mkibariki na wizi,kwamba ukimuona tajiri,mvamie muibie then nunua boda boda mpe nduguyo,utakuwa umetengeneza ajira!!!
Nikuleleze tu,ikifika huko kwamba kila mtu apige basi hata miradi ya maendeleo haitamalizika!Fikiri mradi labda wa maji wa Bilioni 1,kuanzia Waziri mpaka mtendaji mdogo idara ya maji alijinyofolea kutabaki Nini?Acheni kushabikia rushwa na ufisadi!
 
hapa tumegusia mahakama,ambayo ni msingi wa kutoa haki ikiwemo business legal cases. Mwekezaji gani atakuja kwenye corrupt
Tatizo kubwa la mhimili wa mahakama kwa nchi nyingi za bara la Africa ni kuingiliwa na mhimili wa Executive/serikali sio rushwa ndio maana unaona hata kwenye nchi yenye kiwango kikubwa cha rushwa kama Kenya wawekezaji wanamiminika tu, sababu ni uhuru wa mhimili wa mahakama sio kwa sababu hakuna rushwa.
 
Wee jamaa naona umekula maharage mabovu tuu na unaonekana umekata tamaa ya maisha mpaka huwezi kufikiria vizuri tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…