Rushwa haina madhara yoyote ya maana kwa maendeleo ya nchi

Russia ni mojawapo ya Taifa lenye viwango vikubwa vya Rushwa ya kila aina ila lina miondombinu bora na maendeleo makubwa kila nyanja.
Libya pia chini ya Gadaffi ilikuwa ni mojawapo ya mataifa yenye ufisadi sana ila lilikuwa na maendeleo pia.
Umaskini wetu umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kuwa na viongozi wasio na maono makubwa na wafahidhina sana.
 
Kwamba tukiruhusu rushwa na ufisadi basi taifa letu litawafikia hao Russia na Libya!!!
Wacha nicheke tu!
Angalia China,Wana Sheria Kali sana juu ya rushwa na ufisadi!Wananyongana kweli kweli,na taifa lao liko mbali kiuchumi!
Leo mtanzania anawaza kuhalallisha rushwa Ili maendeleo yapatikane,daaah nishushe aisee!🤣🤣🤣
 
Russia ni mojawapo ya mataifa yenye viwango vikubwa vya Rushwa duniani ila bado ni Taifa Tajiri na lenye maendeleo makubwa sana.
Hivi unajua resources alizonazo Russia ? Na Je unajua maisha ya mtu mmoja mmoja Russia kulinganisha labda na maisha ya other European Countries ?

Kwa kukudokeza tu Russia ni Nchi tajiri sana kwa resources.., Russia umafia ni mwingi Russia watu waligawana Keki ya Taifa ndio ukapata kina Abromavich wakati huo huo kuna watu wanashindia vodka na mikate mikavu, masikini wa kutupwa...
 
China bado ni mojawapo ya mataifa yenye viwango vya wastani vya Rushwa pamoja na sheria yao ya kunyonga watu.
Botswana, Rwanda, Tunisia na Senegal yana kiwango kidogo cha Rushwa ukilinganisha na China.
 
Sasa mbona taifa letu tumekataza rushwa lakini bado hatujawafikia?!
Mleta uzi amesema rushwa haina athari kubwa kiuchumi kiasi cha kulifanya taifa maskini, hajasema rushwa inasababisha utajiri. Madini hayajasababisha umaskini DRC bali utafutaji wake, Mafuta hayajaleta shida Iraq. Jinsi ya utafutaji na matumizi ndio yaliyoleta shida DRC, nchi kuwa au kutokuwa na madini au rasilimali nyingine yoyote haileti tofauti yoyote katika maendeleo take bali jinsi ya utafutaji na matumizi yake ndio inaweza kuleta maendeleo, migogoro, vita au dhiki.
 
China bado ni mojawapo ya mataifa yenye viwango vya wastani vya Rushwa pamoja na sheria yao ya kunyonga watu.
Botswana, Rwanda, Tunisia na Senegal yana kiwango kidogo cha Rushwa ukilinganisha na China.
Usiandike tu,leta evidence au source ya habari Yako!
Ili ikusaidie angalia nchi 10 zenye kiwango Cha juu Cha rushwa na nchi 10 zenye kiwango Cha chini Cha rushwa,halafu compare!
 
Hizo ni stori za vijiweni kusongesha muda tu.
Kiwango cha umaskini Russia ni 13%, Marekani(USA) ni 11%. Russia ni mojawapo ya nchi zenye maendeleo na huduma zote muhimu zilizo bora kwa watu wake wengi.
 
This is lack of critical thinking
 

CountryCorruption Score2021 Population
New Zealand884,860,643
Denmark885,813,298
Finland855,548,360
Singapore855,896,686
Switzerland858,715,494
Sweden8510,160,169
Norway845,465,630
Netherlands8217,173,099
Luxembourg80634,814
Germany8083,900,473
Hong Kong777,552,810
Australia7725,788,215
Canada7738,067,903
United Kingdom7768,207,116
Austria769,043,070
Belgium7611,632,326

Mbona unakuja palepale,unadhani hao viongozi wakila rushwa na kuingia mikataba ya hovyo ya madini na rasilimali Kwa makampuni,uchumi wa nchi utakuwaje?Au huelewi rushwa ni Nini?
Rushwa Ina uhusiano wa Moja Kwa Moja na maendeleo na uchumi wa nchi!Angalia hizo nchi chache tu zinazoongoza Kwa kutokuwa na rushwa,angalia zikoje kimaendeleo!
 
Ujinga mwingiii na upumbafu vimechanganyika
Mods ondoeni hili takagumu
 
Correlation sio sawa na causation.
Japan haina madini yoyote ila ni mojawapo ya mataifa tajiri duniani. Uingereza ni taifa dogo sana lisilokuwa na vito vyovyote vya thamani lakini ni taifa tajiri duniani na kuna wakati lilitawala robo ya dunia. Maendeleo ni matoke ya akili zaidi kuliko jambo lingine lolote.
 
Japan alitumia opportunity vizuri baada ya kuangushiwa nuclear bomb!Akanifaika na makubaliano yake na USA!
Sasa kama viongozi wa Japan wangekuwa na tamaa,wangeweza kupewa rushwa na kuingia makubaliano ya kimkataba ambayo hayana tija!
Ukiwa na maarifa na ukajaliwa rasilimali basi taifa litapiga hatua Kwa Kasi!Rushwa ni kikwazo kikubwa Cha maendeleo,na hoja yangu Iko hapo!
 
Makubaliano ya USA na Japan ni stori tu za matangopori za vijiweni. Japan lilikuwa ni dola kubwa lenye maendeleo na nguvu za kiuchumi na kijeshi kabla ya vita vya pili vya dunia na hata kabla ya kuangushwa kwa mabomu ya nyuklia 1945. Kabla ya WWII Japan ilikuwa ikitawala sehemu kubwa ya China na Korea yote.
 
Unachopinga ni kipi?At some point hata hueleweki!Japan imekuja kukua Kwa kasi kiteknolojia baada ya WW2!Japan na Israel ndio nchi ambazo kila mwaka zinapata fungu kutoka USA!
Turudi kwenye rushwa,nasema hivi rushwa ni adui wa maendeleo na ustawi uwa nchi!Ndipo hapo mada ilipo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…