Ruto anaonyesha kila dalili za kuja kuwa Kama Magufuli

Huyu Jamaa atawasaidia sana Wakenya Kama alivyotusaidia sisi Mjomba Magu.
 
Nimemsikia akisema ataondoa bajeti ya IGP na (jeshi la polisi) kutoka ikulu na kuwapelekea wao ili kiwe chombo huru. Sasa, utamkejeli vipi huyu mwamba?!

Mimi namuona kama mtu mtendaji zaidi, kitu ambacho waafrika tunataka. Zaidi ya yote, ni kiongozi mwenye charisma kubwa na tunamtakia kila la kheri!
 
Atakuwa dictator zaidi ya Magufuli. Nimesikiliza hotuba zake, naona viashiria vyote vya tabia za Magufuli. Wakenya watajuta kutomchagua Raila kwani ndio hasa baba wa demokrasia ya Kenya.
Lkn kwa kuwa Kenya Kuna taasisi na mifumo imara atabanwa na hizo taasisi Kama Trump alivyobanwa kule Marekani akashindwa kufurukuta.
 
Tathmini yako iko kinyume kabisa. Jana hiyo hiyo wakati anahutubia baada ya kuPapishwa amechukua hatua ambazo ni kinyume cha hayo unahotabiri. Ametangaza kuteua majaji ambao walipitisbwa na Tu.me ya mahakama lakini Kenyatta akamute. Ameiongezea bajeti mahakama , amepiga marufuku serikali kuingilia polisi kwa kulazimisha wapinzani wa serikali kutengenezewa makosa ya jinai na polisi; pia ameipa autonomy katika masuala ya pesa ipate mgao wake inaotakiwa kupata bila kuhusisha ofisi ya Rais . Hizi sio dalili za mtu mwenye maamuzi ya, kiimla. Kumbuka polisi ndio tool kubwa ya watawala madikteta.
 
Ikiwa ni Ivo, basi kama ilivyokua Kwa Wakenya kumlilia Magufuli awe Rais wao, mpaka anakufa, Wakenya walijaa Bongo

Basi ni zamu ya Watanzania Kumlilia Ruto kua Rais wao
Kabisa!

Siyo kwa hizi takataka za sasa hivi
 
Atakuwa dictator zaidi ya Magufuli. Nimesikiliza hotuba zake, naona viashiria vyote vya tabia za Magufuli. Wakenya watajuta kutomchagua Raila kwani ndio hasa baba wa demokrasia ya Kenya.
Laila ni fungu la kukosa kama kwa Lisu na chama chake tu
 
We jamaa naanza kuwa na wasiwasi na wewe, hivi unadhani Kenya ni Tanzania?

Wakenya wapo mbali kimifumo kutushinda sisi...

Kwa taarifa yako Wakenya wamempata Hichilema wao waliyekuwa wanamsubiri kwa hamu.

Kenya Rais hawezi kuiweka mihimili mingine ya serikali mfukoni mwake...

Mahakama ziko huru..... Wewe imagine mshindi wa urais ameamuliwa mahakamani kiuwazi kabisa.

Bunge liko huru, tena lina uwiano mzuri wa chama tawala na chama pinzani..

Baraza la Seneti, hili nalo lina uwiano mzuri wa chama tawala na ponzani...

Sasa mpaka hapo utasemaje Rais atakuwa dikteta? Kwa jinsi mifumo yao ilivyo thabiti ni ngumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…