Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

Rwanda wanaelekea pabaya
Hawa sasa ndiyo wanaelekea kuzuri. Tena kwenye nchi ya wastaarabu. Kiufupi noise pollution inakera sana. Ifikie wakati watu watumie saa kujiongoza, badala ya vipaza sauti na kengele.

Na kama kuna baa na makanisa nayo yanaendesha shughuli zao kwa sauti ya juu, nao waweke Sound proof! Na siyo kuwapigia kelele wasio husika.

Haiwezekani ibada/starehe yako, iwe mateso kwa mwingine. Yaani saa 10 alfajiri unaamshwa na vipaza sauti vya watu wakikemea mapepo! Wengine wanafanya hiyo adhana sijui! Hiki jambo halikubaliki hata kidogo.
 
Ila tu msiende kujilipua,
Acheni Mungu ajipiganie yeye na dini yake mwenyewe.
Mungu hawezi kujilipua

Maana hayupo

Ndiyo hujawahi "kumuona" Mungu akijipigania

Ni binadamu,wafuasi wa dini ndiyo hupumbana kumpigania wakati yupo "mbinguni"
 
Ishu siyo nani anafanya jambo baya. Ishu ni yeyote anayefanya jambo baya, anafanya jambo baya.
ndio inavyotakiwa, naona mleta mada kaegemea upande mmoja tu wakati kelele ya adhana ni dkka 2 tu. Msala upo kwa haya makanisa ya kipentekoste, wanaabudu kwa fujo sana!!! makusudi ili kila mtu awasikie
 
Kwa sababu tu unafanya mazoezi saa 10 usiku, haina maana kuwa kila mtu afanye mazoezi ya 10 usiku. Wengine wanafanya jioni. Huwezi kupangia dunia muda wa kuamka. Unaweza kusali bila kuamsha wenzio, tena muda ambao kwa kawaida ni wa kulala. Tena wasio wa imani yako. Nasali kila siku jioni kabla ya kwenda kulala na ninapoamka asubuhi. Wala majirani zangu hawajui hili jambo kwa vile nalifanya kimya kimya ndani kwangu.
adhana ni wito wa kukuamsha asubuhi kuabudu

kama huabudu basi amka ufanye mazoezi usiwe mvivu
 
Mungu haabudiwi kwa makelele
Mliongea na Mungu yupi hivyo? .Mungu yupi alikwambia hivyo sababu kuna Miungu tofauti na kila mtu huabudu Mungu wake huyo Mungu wake atakavyo
Wewe uliongea na miungu yote watu wanayoiabudu wakakwambia hilo? Sababu Mungu wako sio wangu na nisimtambui na wewe wangu humtambui
 
Hawa sasa ndiyo wanaelekea kuzuri. Tena kwenye nchi ya wastaarabu. Kiufupi noise pollution inakera sana. Ifikie wakati watu watumie saa kujiongoza, badala ya vipaza sauti na kengele.

Na kama kuna baa na makanisa nayo yanaendesha shughuli zao kwa sauti ya juu, nao waweke Sound proof! Na siyo kuwapigia kelele wasio husika.

Haiwezekani ibada/starehe yako, iwe mateso kwa mwingine. Yaani saa 10 alfajiri unaamshwa na vipaza sauti vya watu wakikemea mapepo! Wengine wanafanya hiyo adhana sijui! Hiki jambo halikubaliki hata kidogo.
Ni wanafiki,wanajua bila ya hayo makelele hakuna hatakayejua kuwa wapo
 
Rwanda waislamu ni wachache mno wengi kule ni wakristu, sio kama huku kwetu ambapo tuko karibu nusu kwa nusu jambo linalofanya tuvumiliane na tuishi vzr kwa amani, sisi tunawavumilia mambo yao na wao wanatuvulia sisi mambo yetu...asietaka kumvumilia mwenzake hata ndoa haiwezi.
 
Mawazo yako ndio yako upande mmoja. Mleta mada ameleta habari aliyoipata BBC. Usimsingizie. Hata Kagame naye hajalalia upande mmoja.

1650040077911.png

ndio inavyotakiwa, naona mleta mada kaegemea upande mmoja tu wakati kelele ya adhana ni dkka 2 tu. Msala upo kwa haya makanisa ya kipentekoste, wanaabudu kwa fujo sana!!! makusudi ili kila mtu awasikie
 
Kupiga marufuku adhana ya kwenye spika siyo mwisho wa sala ya subhi kwa wa islam wa rwanda.

Na ukimuona mkristo anachukia adhana ya subhi ujue kazaliwa kijijiji sana na bado ana ushamba.

Mkristo aliye zaliwa na kukulia mjini, adhana kwake ni kitu ya kawaida.
 
Sauti ya Adhana ikitolewa bila yale maspika sioni shida.
Tatizo ni yale maspika wanayofunga pande 4 za msikiti kwa kweli ile ni noise pollution unakuta yana dB200 hadi dB500 lazima usingizi ukate. Hata mbele ya Allah siyo sahihi.

Laiti wangefanya kama enzi za kina Bilal (rehema ziwe juu yaje) bila kutumia maspika hakuna tatizo.
 
Kuna makanisa yanafanya amzoezi ya kwaya mpaka saa nne. Kuna mikesha na tena yako maeneo ya makazi
Mengine yana-record maombezi Yao ya mchana kutwa na kwaya zao halafu wakisepa Ile usiku wanaachia Yale maombezi Yao kwa hewa kwny Yale maspika yao, zinapigwa usiku kucha huku wamefunga kanisa Lao na kufuli.Asubuhi wanakuja kufungua kanisa na Maisha yanaendelea 😄😄😄.
 
Back
Top Bottom