Kwa hili Rwanda nawapongeza sana, zile kelele za alfajiri zinakera sana.
Hii ni Taharifa ya BBC...
Waislamu wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Rwanda hawasikii adhana wakati wa swala ya asubuhi, na huenda wasisikie tena, kutokana na marufuku iliyowekwa na mamlaka nchi humo.
-
Mwezi uliopita mamlaka ilipiga marufuku matumizi ya vipaza sauti kwenye misikiti asubuhi na mapema, ikisema kuwa ilikiuka sheria za uchafuzi wa kelele ambazo zinakataza kelele zaidi ya decibel 55 wakati wa mchana na decibel 45 usiku katika maeneo ya makazi.
-
Mamlaka ya Rwanda inasema kuwa wakaazi walilalamika kuhusu mwito wa mapema wa maombi - ambao hufanyika majira ya alfajiri na huchukua kama dakika mbili au tatu.
View attachment 2188599
Sent from my Redmi Note 9S using
JamiiForums mobile app