Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

Umenikumbusha bar, nazo ziko kwenye makazi ya watu zinaachia mziki. Hivi tz hakuna sheria zinazofuatwa. Mfano nasikia eti vituo vya mafuta vinabidi viachiane 3 kms, lakini unakuta viko opposite eavh other, bar kwenye makazi ya watu
Usisahau na hawa wenye zinazoitwa studio. Wanaingiza movies na nyimbo. Wanafungulia music kwa sauti za juu kuanzia asubuhi hadi saa nne usiku. Tena kwenye makazi ya watu

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Mi naona waruhusu adhana kwa masaa ya mchana pekee, Ila kwa suala la alfajiri watu watumie alarm, dunia imeendelea sahv karibu Kila nyumba Kuna simu,,, na Hili liende sambamba kwa makanisa maana Kuna makanisa utasema Bora hata ya adhana ya dk2 maana huku kwetu Kuna kanisa la kkkt wanagonga kengele mfululizo km dkk5, halafu baada ya hapo yanaanza matumizi ya spika mpaka asubuhi, kiukweli Ni kero, ukizingatia binadamu anahitaji masaa 8 ya usingizi ili apate afya nzuri, kongole Rwanda, natamani Tanzania tuige bila ubaguzi wa dini
 
Abuu Hurayrah anasema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

(( Lau kama watu wangelijua fadhila zilizopo kwenye adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate njia ya kuzipata ila kwa kupiga kura, basi wangelipiga kura. Na lau wangelijua fadhila za kuwahi mapema (Msikitini), basi wangelishindania. Na lau wangelijua fadhila za ‘Ishaa na Alfajiri, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (615) na Muslim (437].
 
Mm ni mkristo but kitendo huyu jamaa kujimwamba fy ktk dini hizi mbili,zitampelekea vita nzito ambayo hataiweza na pengine ikamgarimu maisha.

Vita za kidini kati ya serkali na dini,
Huishia kuangusha dola,na ikifanikiwa kusimama dola bas kiongozi wa dola ndiye atakayeanguka.
Asivimbe sana ,muda huakoseagi target.
Hajakataza ili punguzeni mikelele.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ipo hivi dini inanguvu kwenye serikali hivyo tujue kwamba kama ikitokea tz waislam wana nguvu kubwa kuiwekea ugumu kwenye mambo yao ya kisiasa nk.

Pia kwa wafia dini au wajinga watakataza na watasema hizo ni kelele ila kwangu mimi hua sichagui dini bali nachagua kinachotolewa na dini mimi ni mkristo ila nasikiliza mawaidha ya masheikh na pia misaafu nasoma kawaida maana wanachofundisha havina tofauti na vya kwetu yena kuna muda vinazidi maana ukweli na unafiki ni vitu viwili tofauti.

Mfia dini utawasikia anawaita wakristo makafiri hawaelewi maana ya ukafiri wanajiona wapo sawa hatakama wanatenda mabaya kiasi gani alimradi ni waislam wanajiona wapo sawa.

Wafia dini utawasikia wakisema waislam ni magaidi hawaelewi kwamba nchi ambazo kuna % kubwa ya vita ni waislam sasa nashindwa kuelewa wangevaa rozari ili wasiwe magaidi?
Hata vatikani kukiwa na ugaidi watavaa kama tamaduni zao zilivyo na watatafuta mistari kwenye biblia ili kujipa ruhusa kufanya yao kama wengine wanavyofanya.

Kama wewe sio mfia dini utaelewa zaidi ya hawa watu wanao ng'ang'ania dini bila kua na imani yeyote na matendo yao yanakinzana na dini zote.

Mi jingependa ile adhana iwe kwa kiswahili na pia mafundisho mengine yawe kwa kiswahili maana kupaza sauti kwa watu wengi af wachache ndio wanaelewa naona ni kupaka kuku rangi.

Pia kama nia yao kama nikutaka watu waingie peponi basi wapaze kwa lugha inayoeleweka na watu wote ili waelewe zaidi

Kama nia yao ni kupaza uislamu na kiarabu watoe maspika yao tu maana yanafaida kwa wachache na kero kwa wengi

Kama unataka watu wasiibe sema watu wasiibe 95% ya watu watakao sikia wataelewa sasa ukisema dhdejwkwbdhdjsskbd 10% wakaelewa na hao walio baki wakaendelea kuiba utakua umafanya kazi kubwaaa faida ndogo.

Mtu huona kelele kwasababu kinachosemwa akielewi utakuta huyohuyo kanisani kwao wana maspika kama ya wasanii wakubwa kwenye viwanja lakini kelele azioni maana anaelewa.

Naona ligha rahisi ihusike maana kuna watu kama mm ambao hatuangaliii dini saaana bali tunachukua mafundisho ambayo yanatufanya tuishi na watu vyema .
 
Abuu Hurayrah anasema kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) anasema:

(( Lau kama watu wangelijua fadhila zilizopo kwenye adhana na safu ya kwanza, kisha wasipate njia ya kuzipata ila kwa kupiga kura, basi wangelipiga kura. Na lau wangelijua fadhila za kuwahi mapema (Msikitini), basi wangelishindania. Na lau wangelijua fadhila za ‘Ishaa na Alfajiri, basi wangeliziendea hata kwa kutambaa)). [Hadiyth Swahiyh: Imefanyiwa “ikhraaj” na Al-Bukhaariy (615) na Muslim (437].
Punguzeni kelele..kwani waumini wenu hawajui muda wa kuabudu mpaka wapigiwe mikelele kila siku kukumbuswa..

#MaendeleoHayanaChama
 
Mada kama hii ya "Adhana" ilimfukuzisha kazi Dada mmoja maarufu tu huko Twitter baada ya kukaa kwenye kipindi cha Televisheni alichokua akiendesha aka support hoja ya 'Mgeni Mualikwa' baada ya Mgeni kusema kwamba 'Adhana' ni Noise pollution!..Kipindi kikaisha saa 07:50, sijui wale jamaa wa Bakwata walitokea wapi..wakatwanga simu moja kwa 'Mmiliki' ...ndani ya Dakika chache walimiminika wale jamaa kwenye viunga vya studio wakitaka ufafanuzi wa hoja zilizoungwa mkono na 'Presenter'.....Flashback hiyo! Zamani kidogo imetokea..na Huyo Dada alirudi kwenye runinga baada kama ya 7 yrs hivi! [emoji23] [emoji23] [emoji23] Mada korofi sana hizi!
Ukitaka kuona fujo ya maana serikali iingilie mambo ya kidini yami itokee leo aseme hamna pasaka ,maandamano kwa wakristo, kutumia vipaza sauti ndio utaona

Au aseme amna iddi wala adhana ndio utajua kumbe hata raia wanamafunzo ya jeshi
 
kwanini ukerwe ukisia watu wanahubiriwa kutokuwa wezi, mashoga, mafisadi na watu wenye roho mbaya.


Elimu ya kodi hufaa zaid kuwafikia wasiolipa kodi kuliko walipa kodi

mawaidha ya umuhimu wa ibada inafaa zaid kuwafikia walio nje ya nyumba ya ibada kuliko walio ibadani

Kuna kitu kila ijumaa huku Kibaha kinaitwa mhadhara au mawaidha baada ya swala ya ijumaa.
Kwanini huyo sheghe hawaambii watu wake walio msikitini ?
Anaweka ma spika makubwa na kuwatangazia wananchi walio nje.
Kwanini asiwahabarishe wale walio ndani,?
 
Mm ni mkristo but kitendo huyu jamaa kujimwamba fy ktk dini hizi mbili,zitampelekea vita nzito ambayo hataiweza na pengine ikamgarimu maisha.

Vita za kidini kati ya serkali na dini,
Huishia kuangusha dola,na ikifanikiwa kusimama dola bas kiongozi wa dola ndiye atakayeanguka.
Asivimbe sana ,muda huakoseagi target.
P Kagame siyo wa kuogopa Jihad uchwara Rwanda.
 
KWELI AISEE HAWA MAAMUMA WANA MAKELELE SANA HASA UKIKAA JIRANI NA MSIKITI. NI KERO JA INABOA SANA.

KIBAYA ZAIDI MKIWA NA SPIKA KANISANI KWENU WATAANDAMANA MTAA MZIMA
 
Haki ya kuamshwa unayo. Mwombe mke wako akuamshe. Unaweza pia kutumia alarm. Usiamshe mji mzima saa 10 usiku. Rwanda oyeee... Haki zinazovunja haki za wengine ni haki za kishetani. Ni sawa na mwizi aseme ana haki ya kuiba kwa hiyo serikali kuzuia wizi, inavunja haki yake za kuiba. Huo ni ujinga.
Kwanini wewe uone ni haki yako kulala na usiamshwe,lakini usione haki ya wale wanaotaka kuamshwa!?
 
Back
Top Bottom