Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,713
- 6,121
Hayo Rwanda walisha deal nayo longtimeSio kila kitu cha kuiga, wakipiga marufuku adhana wasisahau na utitiri wa makanisa yanayopiga mziki weekdays kwenye makazi ya watu tena kwa maspka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hayo Rwanda walisha deal nayo longtimeSio kila kitu cha kuiga, wakipiga marufuku adhana wasisahau na utitiri wa makanisa yanayopiga mziki weekdays kwenye makazi ya watu tena kwa maspka
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]hio ebony umeitoa wapi wewe? mada imekuja na habari ya BBC acha uhuni!
NonsenseKwa hili Rwanda nawapongeza sana, zile kelele za alfajiri zinakera sana.
Hii ni Taharifa ya BBC...
Waislamu wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Rwanda hawasikii adhana wakati wa swala ya asubuhi, na huenda wasisikie tena, kutokana na marufuku iliyowekwa na mamlaka nchi humo.
-
Mwezi uliopita mamlaka ilipiga marufuku matumizi ya vipaza sauti kwenye misikiti asubuhi na mapema, ikisema kuwa ilikiuka sheria za uchafuzi wa kelele ambazo zinakataza kelele zaidi ya decibel 55 wakati wa mchana na decibel 45 usiku katika maeneo ya makazi.
-
Mamlaka ya Rwanda inasema kuwa wakaazi walilalamika kuhusu mwito wa mapema wa maombi - ambao hufanyika majira ya alfajiri na huchukua kama dakika mbili au tatu. View attachment 2188599
Sent from my Redmi Note 9S using JamiiForums mobile app
Kwa sababu tu unafanya mazoezi saa 10 usiku, haina maana kuwa kila mtu afanye mazoezi ya 10 usiku. Wengine wanafanya jioni. Huwezi kupangia dunia muda wa kuamka. Unaweza kusali bila kuamsha wenzio, tena muda ambao kwa kawaida ni wa kulala. Tena wasio wa imani yako. Nasali kila siku jioni kabla ya kwenda kulala na ninapoamka asubuhi. Wala majirani zangu hawajui hili jambo kwa vile nalifanya kimya kimya ndani kwangu.
Adhana si maombi. Ni mwito. Kama wengine wanavyotumia kengele.Mnatuboa kusema ukweli. Mungu anasikia hata unayowaza moyoni. Hahitaji kipaza sauti.
Ajitahidi apige marufuku na kengele. Kwani kama ilivyo adhana ni kero kwa wengine,hata kengele nayo ni kero kwa wengine.Kongolee kwa mgunduzi wa alarm [emoji354] Sasa zitatumika vizuri Rwanda.
Hongera Kagame kwa maamuzi magumu yenye uthubutu
Usiutetee uislamu kwa kuhalalisha makelele ya makanisa na sehemu za stareheukishakaa kwny jamii kuna mambo madogo madogo lazima uwe mvumilivu
tunavumilia kelele za ndege Airport kila Alfajiri
tunavumilia siku ya ibada ya wengine kuwa mapumziko na wengine kutokuwa mapumziko
kuna Baniani siku zao za sikukuu za kidini sio mapumziko lakin kwa waislam na wakristo ni mapumziko
kuna kelele bar tunavumilia japo sie sio walevi
kuna sauti za juu za ibada za makanisa usiku kucha bado tunavumilia
kama huwezi kuvumilia kelele za adhana ya dakika tatu nenda kaishi porini au kaa mbali na jamii ya waislam
Sio kufanyika mchana,wapo wanaojiita wameokoka hukesha wakiimba tena kwenye nyumba za kupanga zenye watu wengi. Wapo wanaokesha wakiomba huku wakitumia vipaza sauti na muziki wa kutisha. Tena sio makanisani bali nyumbani kwa mmoja wao. Tena katikati ya makazi ya watu.Hata Wakristo kupiga muziki na matumizi ya vipaza sauti ambavyo vinapeleka sauti mbali kwa watu ambao siyo sehemu ya hadhara iliyopo, siyo uungwana. Lakini afadhali hayo yafanyike mchana kuliko kuamsha watu saa 10 usiku tena kwa maneno jeuri kabisa, "amka, amka, amka... kumekucha".
Uhuru uwe na mipaka.Mimi ni mkristo! Lakini siungi mkono kuminya uhuru wa kuabudu!
Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
Kwanini wewe uone ni haki yako kulala na usiamshwe,lakini usione haki ya wale wanaotaka kuamshwa!?Kwa hiyo ukiamshwa saa 10-11 alfajiri kwa dk 5, unalala tena? Acheni kubudhuni wenzenu, jamani. Fikirieni wenzenu pia. Hamuishi kisiwani. Unaweza kuabudu bila kubughudhi wanaokuzunguka.
chuki zenu ni kwa uislam ila mnajificha kwenye kichaka cha adhanaUsiutetee uislamu kwa kuhalalisha makelele ya makanisa na sehemu za starehe
Serikali ikiamua mbona inaweza
Kama sheria ipo utekelezaji udanyike
Kama haipo itungwe
Adhana hazitakatazwa wala yale maspika ya wakristo
Ila sheria iseme tu mwisho wa sauti ni decibel kadhaa
Automatically hayo makelele yatajifia tu
Mbona Serikali imweza Zumaridi
Ikiamua haitashindwa