Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

Rwanda wamepiga marufuku "Adhana" Alfajiri

hio ebony umeitoa wapi wewe? mada imekuja na habari ya BBC acha uhuni!
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Screenshot_20220415-194856.jpg
 
Kwa hili Rwanda nawapongeza sana, zile kelele za alfajiri zinakera sana.

Hii ni Taharifa ya BBC...

Waislamu wanaoadhimisha mwezi mtukufu wa Ramadhani nchini Rwanda hawasikii adhana wakati wa swala ya asubuhi, na huenda wasisikie tena, kutokana na marufuku iliyowekwa na mamlaka nchi humo.

-

Mwezi uliopita mamlaka ilipiga marufuku matumizi ya vipaza sauti kwenye misikiti asubuhi na mapema, ikisema kuwa ilikiuka sheria za uchafuzi wa kelele ambazo zinakataza kelele zaidi ya decibel 55 wakati wa mchana na decibel 45 usiku katika maeneo ya makazi.

-

Mamlaka ya Rwanda inasema kuwa wakaazi walilalamika kuhusu mwito wa mapema wa maombi - ambao hufanyika majira ya alfajiri na huchukua kama dakika mbili au tatu. View attachment 2188599

Sent from my Redmi Note 9S using JamiiForums mobile app
Nonsense
 
Huyu Kagame anapoelekea sipo katiba yao haina kipengele cha Uhuru wa kuabudu [emoji2959][emoji2959][emoji2959]
 
ukishakaa kwny jamii kuna mambo madogo madogo lazima uwe mvumilivu

tunavumilia kelele za ndege Airport kila Alfajiri

tunavumilia siku ya ibada ya wengine kuwa mapumziko na wengine kutokuwa mapumziko

kuna Baniani siku zao za sikukuu za kidini sio mapumziko lakin kwa waislam na wakristo ni mapumziko

kuna kelele bar tunavumilia japo sie sio walevi

kuna sauti za juu za ibada za makanisa usiku kucha bado tunavumilia

kama huwezi kuvumilia kelele za adhana ya dakika tatu nenda kaishi porini au kaa mbali na jamii ya waislam
Kwa sababu tu unafanya mazoezi saa 10 usiku, haina maana kuwa kila mtu afanye mazoezi ya 10 usiku. Wengine wanafanya jioni. Huwezi kupangia dunia muda wa kuamka. Unaweza kusali bila kuamsha wenzio, tena muda ambao kwa kawaida ni wa kulala. Tena wasio wa imani yako. Nasali kila siku jioni kabla ya kwenda kulala na ninapoamka asubuhi. Wala majirani zangu hawajui hili jambo kwa vile nalifanya kimya kimya ndani kwangu.
 
Mm ni mkristo but kitendo huyu jamaa kujimwamba fy ktk dini hizi mbili,zitampelekea vita nzito ambayo hataiweza na pengine ikamgarimu maisha.

Vita za kidini kati ya serkali na dini,
Huishia kuangusha dola,na ikifanikiwa kusimama dola bas kiongozi wa dola ndiye atakayeanguka.
Asivimbe sana ,muda huakoseagi target.
 
Imani ya mtu isipangiwe cha kufanya Serikali yetu haina dini mkikataza adhana,basi madebe yanayopigwa makanisani,nyakati zote yapigwe marufuku
 
Kongolee kwa mgunduzi wa alarm [emoji354] Sasa zitatumika vizuri Rwanda.
Hongera Kagame kwa maamuzi magumu yenye uthubutu
Ajitahidi apige marufuku na kengele. Kwani kama ilivyo adhana ni kero kwa wengine,hata kengele nayo ni kero kwa wengine.
Wote tutumie alarm

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
ukishakaa kwny jamii kuna mambo madogo madogo lazima uwe mvumilivu

tunavumilia kelele za ndege Airport kila Alfajiri

tunavumilia siku ya ibada ya wengine kuwa mapumziko na wengine kutokuwa mapumziko

kuna Baniani siku zao za sikukuu za kidini sio mapumziko lakin kwa waislam na wakristo ni mapumziko

kuna kelele bar tunavumilia japo sie sio walevi

kuna sauti za juu za ibada za makanisa usiku kucha bado tunavumilia

kama huwezi kuvumilia kelele za adhana ya dakika tatu nenda kaishi porini au kaa mbali na jamii ya waislam
Usiutetee uislamu kwa kuhalalisha makelele ya makanisa na sehemu za starehe

Serikali ikiamua mbona inaweza

Kama sheria ipo utekelezaji udanyike

Kama haipo itungwe

Adhana hazitakatazwa wala yale maspika ya wakristo

Ila sheria iseme tu mwisho wa sauti ni decibel kadhaa

Automatically hayo makelele yatajifia tu

Mbona Serikali imweza Zumaridi

Ikiamua haitashindwa
 
Hata Wakristo kupiga muziki na matumizi ya vipaza sauti ambavyo vinapeleka sauti mbali kwa watu ambao siyo sehemu ya hadhara iliyopo, siyo uungwana. Lakini afadhali hayo yafanyike mchana kuliko kuamsha watu saa 10 usiku tena kwa maneno jeuri kabisa, "amka, amka, amka... kumekucha".
Sio kufanyika mchana,wapo wanaojiita wameokoka hukesha wakiimba tena kwenye nyumba za kupanga zenye watu wengi. Wapo wanaokesha wakiomba huku wakitumia vipaza sauti na muziki wa kutisha. Tena sio makanisani bali nyumbani kwa mmoja wao. Tena katikati ya makazi ya watu.
Haya mambo ni kuvumiliana. Sio kuongozwa na mihemko

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Sheria nikuwa Bar, Makanisa, Misikiti katika miji inatakiwa itengewe maneo yake maalum.
Na sio maeneo ya makazi ya watu.

Adhana ilianzisha enzi za Kale ambapo mawasiliano yalikuwa duni.

Katika Makazi holela, ya hapa Msikiti hapa Bar hapa kanisa ni vurugu tupu na kunasababisha usumbufu mkubwa kwa wasiohusika.

Adhana kwa sasa haina mashiko kwakuwa ipo hata kwenye simu ni kuitega tu.

Kagame yuko sahihi.

Hakuna kuanzisha Kanisa kama huna sifa.
Hakuna kusumbua watu wasio husika kwa kelele za adhana.

Safi sana Kagame.
 
Rwanda wanajali sana suala zima la mazingira..nawapongeza..ibada yako isiwe kero kwa wengine..kwanza kusali kwa utulivu Mungu ndio anapokea maombi..sio mikelele iso na maana...nakuleta kero kwa jamii.



#MaendeleoHayanaChama
 
Kwa hiyo ukiamshwa saa 10-11 alfajiri kwa dk 5, unalala tena? Acheni kubudhuni wenzenu, jamani. Fikirieni wenzenu pia. Hamuishi kisiwani. Unaweza kuabudu bila kubughudhi wanaokuzunguka.
Kwanini wewe uone ni haki yako kulala na usiamshwe,lakini usione haki ya wale wanaotaka kuamshwa!?
Muhimu kuvumiliana.

Jambo ambalo mimi nikiwa muislamu nasisitiza ni kufuata mafundisho sahihi ya dini zetu. Tuache madoido. Adhana imefundishwa mwanzo wake hadi mwisho wake. Haya maneno mengineyanayoongezwa ni makosa. Mtu anawasha kipaza sauti anaanza kuhubiri halafu ndio anaadhini. Hayo ni kuzidisha mambo kwenye dini. Na dini inakataza. Adhana sahihi haichukui dakika tano

Sent from my SM-G5500 using JamiiForums mobile app
 
Kuna kitu kila ijumaa huku Kibaha kinaitwa mhadhara au mawaidha baada ya swala ya ijumaa.
Kwanini huyo sheghe hawaambii watu wake walio msikitini ?
Anaweka ma spika makubwa na kuwatangazia wananchi walio nje.
Kwanini asiwahabarishe wale walio ndani,?
 
Usiutetee uislamu kwa kuhalalisha makelele ya makanisa na sehemu za starehe

Serikali ikiamua mbona inaweza

Kama sheria ipo utekelezaji udanyike

Kama haipo itungwe

Adhana hazitakatazwa wala yale maspika ya wakristo

Ila sheria iseme tu mwisho wa sauti ni decibel kadhaa

Automatically hayo makelele yatajifia tu

Mbona Serikali imweza Zumaridi

Ikiamua haitashindwa
chuki zenu ni kwa uislam ila mnajificha kwenye kichaka cha adhana

kuna kelelel nyingi sana kwny miji kuliko za adhana ya dakika 3

nakukumbusha tu katika vita kubwa ilizopigwa uislam basi hii adhana ni ndogo sana na inazidi kukata mbuga tu
 
Back
Top Bottom