Allah anasema hakuna kilicho mzuia ila kaamua kutoshusha , sasa wewe nani unasema Muhammad alikuwa na muujizaKatika majibu yako ya awali ulisema eti Allah kasema hakuna muujiza kwa Muhammad maana amezuia miujiza , wewe nani unamrekebisha ?
Nilipokutaka uoneshe wapi imeandikwa umekuja na hicho kipande hapo cha surat bani Israil 17 .ambacho hata japo hukumalizia aya yote lakini bado hicho ulichoandika hakizungumzii kwamba Allah alizuia muujiza kwa vile Muhammad s.a.w alizuia miujiza mwengine..Yeye Muhammad s.a.w kwa Mwenyezi Mungu ni nani hata azuie muujiza.Kama angekuwa na uwezo huo basi angezuia kuisoma ile aya katika surat Abbasa iliyomkaripia yeye mwenyewe pale alipompuuza kipofu ili awalinganie matajiri wa Makkah kwanza.
Tukirudi kwenye hiyo aya hapo juu 17:59 kwa urefu wake wote iko hivi,na nakuletea kwa Kiswahili kwani yawezekan kiingereza kinakuchanganya kwani hata hapo juu umetafsriri kimakosa.
Hakuna kilichotuzuia kuteremsha miujiza ambayo washirikina waliitaka isipokuwa ni kwamba ummah waliowatangulia waliikanusha, Allah Mtukufu Aliwajibu kwa waliyotaka wakakanusha na wakaangamia. Na tuliwapa Thamûd, nao ni watu wa Ṣãlih, miujiza iliyo wazi, nayo ni ngamia, wakaikanusha na tukawaangamiza. Na huku kutuma kwetu Mitume wakiwa na alama, mazingatio na miujiza tuliyoipitisha kwenye mikono yao, hakukuwa isipokuwa ni kuwatisha waja wapate kuzingatia na wakumbuke.
Allah s.w. katika aya hii alikuwa anamsimulia mtume Muhammad s.a.w juu ya jeuri walizofanya umma zilizopita maelfu ya miaka nyuma walipokuwa wakiletewa miujiza mara kwa mara halafu wanaleta jeuri ya kuongeza maneno badala ya kusadiki na kutekeleeza.Mwishowe Allah s.w akaamua dawa yao awaangamize.Ndio pale ikatajwa baadhi ya adhabu walizopoata baadhi ya Qaumu hizo mfano watu wa Thamud ambao ni watu wa nabii Saalih a.s. Hebu angalia hiyo aya na uongo wako uliotoa hapo juu.Jeuri zako kama hizi unapewa dalili halafu unapindisha maneno kujifurahisha nafsi yako ungekuwepo wakati wa Qaumu hizo ungeonja hizo adhabu.Lakini si neno hata leo Allah s.w aliyewaangamiza Qaumu hizo yuhai na anakuona.